- Ellie Mpanzu tetesi zilikuwa zinaeleza kuwa anakwenda Yanga SC
- Usajili Simba SC umeanza mapema 2025/26
- Kauli ya Rushine De Reuck raia wa Afrika Kusini mara baada ya kuongeza mkataba mpya
- Yusuph Kagoma bado yupoyupo sana mitaa ya Msimbazi miaka miwili
Usajili Simba SC umeanza mapema kwa kumalizana na nyota watatu muhimu. Ellie Mpanzu, Yusuph Kagoma na Rushine De Reuck wataendelea kusalia. Hii ni baada ya kufikia makubaliano kuongeza kandarasi mpya mitaa ya Msimbazi.
SOMA HII: Simba SC yatambulisha mbeba mikoba ya Zimbwe Jr 2025/26 Antony Mligo | Sekeseke lake la usajili
Vuna mamilioni sasa hivi ukipaisha Kindege cha SportPesa
Ni sasa hivi unavuna mamilioni ukipaisha Kindege cha SportPesa. Ni rahisi sana hasa ukizingatia Marubani wapo makini. Cheza Aviator upate mgao wako.

Usajili wa Simba SC umeanza mapema kwa nini?

Usajili Simba SC umeanza mapema kutokana na makosa yaliyopita. Msimu wa 2024/25 Simba SC ilipishana na beki Mohamed Hussen Zimbwe Jr aliyesajiliwa Yanga SC. Beki huyo mkataba wake ulifika mwisho hivyo aliondoka bure unyamani.
Kutokana na pigo hilo mabosi wa Simba SC wameanza mapema kuongeza mikataba kwa wachezaji. Taarifa zinaeleza wachezaji wote muhimu mikataba yao inaboreshwa. Lengo ni kurejesha makali ya timu hiyo.
Yusuph Kagoma
Yusuph Kagoma ni kiungo mkabaji mwenye miaka 29. Amejiunga na Simba SC akitokea Fountain Gate alipokuwa msimu wa 2023/24. Aliwahi kucheza Geita Gold 2023/24.
Awali kabla ya kusajiliwa na Simba SC alikuwa anatajwa kuwa katika rada za Yanga SC. Sakata lake la kusaini Yanga SC lilizuia gumzo na mwisho mchezaji akasalia Msimbazi.
Kutokana na kiwango bora anachonyesha akiwa uwanjani, Machi 8,2026 aliongeza kandarasi nyingine. Hivyo bado ataendelea kusalia ndani ya kikosi cha Simba SC baada ya kuongeza kandarasi ya miaka miwili hadi 2028.
Mbali na kukaba ana uwezo wakufunga magoli. Katika mchezo wa Simba SC 3-0 TRA United, Kagoma alifunga goli moja. Magoli mengine yalifungwa na Seleman Mwalimu na Neo Maema.
SOMA HII: Simba SC 3-0 TRA United highlights, H2H, standings, twakimu | Matokeo ya NBC Premier League

Rushine De Reuck

Rushine De Reuck ni beki wa kati alipendekezwa na Fadlu Davids aliyekuwa kocha wa Simba SC 2024/25. Ana miaka 30. Ni raia wa Afrika Kusini ameongeza kandarasi ya mkataba wa mwaka mmoja mpaka 2027.
Beki huyo alijiunga na Simba SC akitokea Mamelodi Sundowns. Ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Steve Barker. Katika mchezo dhidi ya TRA United alichaguliwa kuwa mchezaji bora ikiwa ni tuzo yake ya 3.
Marchi 8 2026 taarifa rasmi ya kuongeza mkataba wake ilikuwa wazi. Baada ya mechi 14 safu ya ulinzi iliruhusu magoli. Ni pointi 31 imekusanya ikiwa nafasi ya pili kwenye msimamo.

Kauli ya kwanza ya Rushine unyamani
“Nimefurahi kuendelea kuwa ndani ya kikosi cha Simba SC. Bado tutaendelea kushirikiana na wachezaji ili kupata matokeo. Mashabiki waendelee kuwa nasi,”.
Ellie Mpanzu

Winga Ellie Mpanzu ni raia wa DRC Congo alikuwa anatajwa kuwa katika rada za Yanga SC. Ametengeneza jumla ya pasi 5 za magoli. Alifunga goli la ushindi mchezo dhidi ya Singida Black Stars akitokea benchi.
Machi 23,2026 taarifa zilitolewa kuhusu mkataba wake. Rais wa Simba SC, Mohammed Dewji alihusika kwa asilimia kubwa kufanikisha jambo hilo. Ni miaka wa miaka miwili Mpanzu alisaini.
SOMA HII: Usichokijua kuhusu usajili wa Mpanzu: Je, ni kweli Yanga SC walimpa mkataba?

Hitimisho
Usajili Simba SC umeanza mapema ikiwa bado dirisha la usajili halijafunguliwa. Mpaka sasa mnyama amemalizana na nyota watatu. Wengine akiwemo Morice Abraham wanatajwa kufuata.

