- Kibabage Day yawapa ushindi mnono Simba SC NBC Premier League.
- Simba SC 3-0 TRA United, Meja Isahmuyo Machi 22,2026.
- Seleman Mwalimu, Ellie Mpanzu na Yusuph Kagoma wang’ara.
Simba SC 3-0 TRA United matokeo rasmi mchezo wa NBC Premier League. Magoli yamefungwa na Seleman Mwalimu dakika ya 12, Neo Maema dakika ya 67 na Yusuph Kagoma dakika ya 89. Uwanja wa Meja General Isahmuyo, Machi 22, 2026 saa 1:00 usiku.
SOMA HII: Ratiba ya Simba SC 2025/26 Machi dakika 450 za kazi/ Msimamo, matokeo
Je bado hujashinda mamilioni ya SportPesa? Cheza Aviator ushinde muda huu
Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Bashiri na SportPesa uvune mkwanja sasa hivi kwa kubonyeza picha hapo chini.

Simba SC 3-0 TRA United, wafungaji wa magoli

Ni Simba SC 3-0 TRA United furaha kwa wenyeji kuvuna pointi mbele ya wapinzani wagumu. Magoli ya mnyama yalifungwa na wachezaji watatu. Mshambuliaji Seleman Mwalimu kwa mkwaju wa penati iliyosababishwa na Nikson Kibabage aliyekuwa mgeni rasmi.
Goli la pili lilifungwa na Neo Maema kipindi cha pili na Yusuph Kagoma alipachika goli la tatu katika dakika za lala salama. Ushindi huo unamfanya mnyama kupanda kutoka nafasi ya tatu mpaka ya pili NBC Premier League.
Ellie Mpanzu wa Simba SC alikuwa kwenye mwendelezo wa ubora. Alitoa pasi ya goli kwenye mchezo huo wakati wakivuna pointi tatu muhimu.
H2H Simba SC vs TRA United

Februari 2,2025, TRA United 0-3 Simba SC, Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.
Agosti 18,2024- Simba SC 3-0 TRA United, Uwanja wa KMC Complex
Mei 6,2024- Simba SC 2-0 TRA United, Uwanja wa Azam Complex
Februari 6,2024- TRA United 0-4 Simba SC, Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.
Machi 22,2026- Simba SC 3-0 TRA United, Uwanja wa Meja General Isahmuyo.
SOMA HII: TRA United vs Simba SC umeahirishwa/ TPLB kuamua/ Kamishna Mussa Nyamandege athibitisha

Msimamo wa Simba SC vs TRA United
| POS | MP | W | D | L | PTS |
| 2. Simba SC | 14 | 9 | 4 | 1 | 31 |
| 10.TRA United | 16 | 5 | 5 | 6 | 20 |
Mwalimu arejea na goli lake
Seleman Mwalimu mshambuliaji wa Simba SC alikuwa nje kwa muda kutokana na adhabu ya kufungiwa mechi 3. Mchezo wake dhidi ya TRA United unakuwa ni wa kwanza baada ya adhabu kuisha. Kurejea kwake uwanjani kumeongeza nguvu katika eneo la ushambuliaji kwa kuwa alifunga goli kwa mkwaju wa penati.
Simba SC yaishusha Azam FC
Pointi tatu ambazo Simba SC imezivuna zimeishusha Azam FC kutoka nafasi ya pili.Ni pointi 31 Simba SC inafikisha huku Azam FC ikiwa na pointi 29 baada ya mechi 15. Vinar ani Yanga SC wenye pointi 38 baada ya kucheza mechi 16.
SOMA HII: Simba SC yajivunia ubora wa kikosi 2025/26/ Fixture, Standings

Hitimisho
Simba SC 3-0 TRA United yanazidi kumrejesha mnyama kwenye makali taratibu. Pointi 7 kwa sasa anadaiwa ili kumfikia mpinzani wake mkuu Yanga SC. Je ataweza kutoboa akiwa na mechi moja mkononi?

