Pamba Jiji FC vs Simba SC NBC Premier League. Machi 19 2026 mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa CCM Kirumba. Rekodi zinaonyesha wamekutana mara mbili ushindi ukiwa ni upande wa mnyama.
SOMA HII: Simba SC yajivunia ubora wa kikosi 2025/26/ Fixture, Standings
Bado hujashinda mamilioni ya SportPesa?
Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Bashiri na SportPesa uvune mkwanja sasa hivi kwa kubonyeza picha hapo chini.

Pamba Jiji FC vs Simba SC NBC Premier League rekodi itavunjwa?

Ni Pamba Jiji FC vs Simba SC NBC Premier League. Msimu wa 2024/25 katika mechi mbili Simba SC ilipata ushindi. Je Pamba Jiji FC atavunja rekodi na kupata ushindi mchezo wa nyumbani? Dakika 90 zitaamua.
Simba SC kwenye ligi imepoteza mchezo mmoja dhidi ya Azam FC. Pamba Jiji FC ni mechi tatu ilichapwa ndani ya NBC Premier League. Mbele ya Azam FC kiungo Kelvin Nashon wa Pamba Jiji FC alichaguliwa kuwa Man Of The Match atarudia rekodi yake ni swali ambalo litajibiwa mwisho wa mchezo.
Maoni ya Francis Baraza, Kocha Mkuu wa Pamba Jiji FC
“Wachezaji wanatambua umuhimu wa mchezo wetu uliopo mbele yetu. Tunatambua umuhimu wa kupata pointi tatu na hilo tunalihitaji. Ninapenda kuona tunakuwa huru kwenye kucheza mpira hasa kwa mbinu ambazo nitawapa tunaamini utakuwa ni mchezo mzuri,”.
SOMA HII: NBC Premier League ratiba na CAF Champions League robo fainali

Steve Barker Kocha Mkuu wa Simba SC akiri ugumu
“Si mechi rahisi kulingana na ratiba yetu ilivyo.Tumecheza mechi mfululizo ugenini ila hata ukiangalia mpinzani alivyo ugumu utaongezeka. Nimewaandaa wachezaji wangu vya kutosha kuhakikisha tunatimiza malengo ya kupata pointi tatu,”.
H2H Pamba Jiji FC vs Simba SC

08/05/2025, Simba SC 5-1 Pamba Jiji FC
22/11/2024, Pamba Jiji FC 0-1 Simba SC
Pamba Jiji FC vs Simba SC utabiri
Kulingana na rekodi za wapinzani hawa, mnyama anepewa nafasi kubwa kushinda. Ndani ya dakika 180 Simba SC ilishinda mechi zote. Licha ya mnyama kupewa nafasi kubwa bado Pamba Jiji FC sio timu yakubeza.

Msimamo wa Pamba Jiji FC vs Simba SC
| POS | MP | W | D | L | PTS |
| 4.Simba SC | 12 | 8 | 3 | 1 | 27 |
| 5.Pamba Jiji FC | 15 | 6 | 6 | 3 | 24 |
Hitimisho
Pamba Jiji FC vs Simba SC NBC Premier League ni kituo kinachofuata. Wenyeji wametoka kupata ushindi wa magaoli 2-1 Transit Camp kwenye CRDB Federation Cup. Pamba Jiji FC 2-2 Azam FC mchezo uliopita kwenye NBC Premier League. Je watavunja rekodi? Endelea kufuatilia blog ya SportPesa kwa matokeo zaidi.

