- Moto unawaka Afrika kwa sasa, ni juu ya Taarifa ya CAF kuwavua ubingwa wa AFCON 2025 Senegal, na kuwapa Morocco.
- Maamuzi hayo yamezua maoni mseto miongoni mwa wadau wa michezo. Maswali yamekuwa mengi na Makala hii inakuletea majibu ya baadhi ya maswali hayo.
- Je, Sheria inasemaje? Waliobeti watarudishiwa hela? Nini kitatokea?
Gumzo kubwa Afrika kwa sasa ni juu ya Taarifa ya CAF kuwavua ubingwa wa AFCON 2025 Senegal, na kuwapa Morocco. Maamuzi hayo yamezua maoni mesto miongoni mwa wadau wa michezo. Maswali yamekuwa mengi na Makala hii inakuletea majibu ya baadhi ya maswali hayo, na kuangazia Je, nini kitatokea?
SOMA HII PIA: AFCON 2025 final Senegal vs Morocco: Ratiba, Live score, lineups, h2h, prediction, Habari za timu
Hujashinda mamilioni ya SportPesa?
Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Bashiri na SportPesa uvune mkwanja sasa hivi kwa kubonyeza picha hapo chini.

Kuhusu Senegal kuvuliwa ubingwa wa AFCON 2025

Ni takribani miezi miwili imepita baada ya fainali ya aina yake, iliyojaa matukio mengi yenye utata kati ya Senegal vs Morocco kumalizika. Senegali wakitawazwa mabingwa kwa ushindi wa bao 1-0 kwenye mchezo wa fainali, uliolazimika kuchezwa kwa dakika 120 kufuatia Suluhu ya dakika 90. Katika mchezo huo yalikuwepo baadhi ya matukio tata, yaliyofanya mchezo huo kusimama kwa zaidi ya dakika 15 huku Segal wakitishia kususia mchezo kutokana na maamuzi ya mwamuzi Jean Jacques. Baadae CAF walitoa adhabu kwa kila timu na baadhi ya wachezaji.
Maamuzi ya bodi ya Rufaa kuhusu bingwa wa AFCON 2025
Bodi ya Rufaa ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), imetoa taarifa kuwa ilibaini kuwa Senegal walikiuka kanuni za AFCON kwa kuondoka uwanjani wakati wa fainali iliyochezwa Januari 18. Hii ni baada ya Morocco kupewa penalti yenye utata. Wachezaji wengi wa Senegal walitoka uwanjani wakiongozwa na kocha wao Pape Thiaw. Hii ilisababisha mchezo huo kusimama kwa takriban dakika 17, kabla ya nahodha Sadio Mane kuwashawishi kurudi.
Kifungu cha 82 cha kanuni za AFCON kinaeleza kuwa timu itakayokataa kucheza, au kuondoka uwanjani bila ruhusa ya mwamuzi itachukuliwa kuwa imepoteza na itaondolewa mashindanoni. Kifungu cha 84 kinaongeza kuwa timu itakayokiuka kifungu hicho itapoteza kwa mabao 3-0. Na vifungu hivi ndivyo vilitumiwa na Uongozi wa Shirikisho la soka la Morocco kupitia rufaa yao.
CAF wamejichanganya? Je, hili linakinzana na sheria za IFAB?

IFAB ndiyo taasisi inayotunga sheria za mpira wa miguu duniani. Sheria ya 5.2 inasema: “Maamuzi ya mwamuzi kuhusu matukio ya mchezo, ikiwemo kama bao limefungwa au matokeo ya mechi, ni ya mwisho.” Lakini kwa kubadilisha matokeo miezi miwili baadaye, inaonekana CAF imeenda kinyume na kanuni za IFAB.
SOMA HII ZAIDI: AFCON 2025: Matokeo, hawa hapa wafungaji bora kabla ya Ratiba ya 16 bora, Feisal na Msuva wamo?
Kwa nini imechukua miezi miwili?
CAF haijatoa maelezo kwa nini kanuni hazikutumika mara moja wakati wa tukio. Baada ya rufaa ya Morocco, CAF ilichambua upya kanuni zake, kuhusu matukio ya utata yaliyotokea fainali. Hatimaye, bodi ya rufaa ilichukua hatua isiyo ya kawaida ya kubadilisha matokeo na kumpa Morocco ushindi wa 3-0.
Senegal watakiwa kurudisha medali na kombe

Kufuatia maamuzi hayo Shirikisho la soka la Senegal, wamepewa taarifa ya kutakiwa kurudisha kombe hilo Pamoja na medali. Hapa ndipo panapoonekana kuwa sehemu ngumu zaidi, hili bado halijulikani, hasa kutokana na mchakato wa rufaa unaotarajiwa kuanza kwa upande wa Senegal. Baadhi ya wachezaji wa Senegal wamebeza uamuzi huo mitandaoni, wakichapisha picha za sherehe zao na kombe.
Morocco watoa tamko
Morocco kupitia Shirikisho lao la soka walisema hawakulenga kupinga kiwango cha wapinzani wao, ila walitaka kanuni za mashindano zitumike ipasavyo. Swali ni je, maamuzi hayo yako sahihi kwa asilimia 100 au, kuna mapungufu? Jibu ni kuna mapungufu ambayo Shirikisho la Senegal wanaweza kuyatumia.
Hadi sasa, hakuna mchezaji maarufu wa Morocco aliyeonyesha kusherehekea wazi uamuzi huo. Achraf Hakimi na Brahim Diaz walikuwa kwenye mechi za Ligi ya Mabingwa wakati tangazo lilipotolewa. Video moja inaonyesha Brahim Diaz akicheka na kushangilia kwa utani, baada ya kuambiwa kuhusu uamuzi huo.
Ni kwa kiasi gani hadhi ya AFCON imechafuliwa?

Kupitia taarifa yao, Shirikisho la Senegal limeuita uamuzi huo kuwa “usio wa haki, wa ajabu na usiokubalika,” likisema umeharibu sifa ya soka la Afrika. Katibu mkuu wa shirikisho hilo aliuita “aibu kwa Afrika.” Kwasasa, Morocco wanahesabiwa rasmi kama washindi wa fainali kwa mabao 3-0, wakimaliza kusubiri kwa miaka 49 kushinda taji lao la pili la AFCON.
Bila kujali matokeo ya mwisho, AFCON 2025 tayari imechafuliwa na namna suala hili lilivyoshughulikiwa, na mabingwa wapya watabeba doa hilo mbele ya mashabiki.
SOMA HII PIA: AFCON 2025: Mabingwa Senegal wapewa mapokezi ya Kihistoria Dakar
Hitimisho: Waliobeti je watarusha na kurudishiwa fedha zao?
Kampuni ya kubashiri ‘kubeti’ ya Paddy Power imesema fedha zote za ubashiri zilizowekwa kwa Morocco kushinda zitalipwa. Hakuna marejesho yatakayotolewa kwa walioweka dau kwa Senegal.
Sky Bet pia imelipa dau kwa Morocco kama washindi, huku Betfair wakirekebisha dau zote za mashindano kwa kuzingatia matokeo mapya.

