Arsenal vs ChelseaArsenal vs Chelsea
  • MOTO utawaka katika jiji la London, England leo Jumapili ambapo kunapigwa mchezo mkubwa wa ‘London Derby’.
  • Arsenal vs Chelsea mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Emirates unasubiriwa kwa hamu.
  • Huu ni mchezo mwingine muhimu, ambao unakwenda kutoa mwelekeo wa ubingwa.

MOTO utawaka katika jiji la London, England leo Jumapili ambapo kunapigwa mchezo mkubwa wa ‘London Derby’. Ni Arsenal vs Chelsea mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Emirates. Huu ni mchezo mwingine muhimu, ambao unakwenda kutoa mwelekeo wa ubingwa.

SOMA HII PIA: Arsenal vs Chelsea: Preview, Team News, H2H & Prediction

Je, unataka kushinda mamilioni ya SportPesa?

Ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Bashiri na SportPesa uvune mkwanja sasa hivi kwa kubonyeza picha hapo chini.

image

Kuhusu Arsenal vs Chelsea

Mfululizo wa Chelsea kutopoteza mchezo katika Ligi Kuu ya England chini ya kocha, Liam Rosenior utajaribiwa vilivyo leo Jumapili kwenye Uwanja wa Emirates. Hii ni pale kocha huyo atakapokutana na Arsenal, ambao ndiyo timu pekee iliyowashinda chini ya utawala wake il ani kwenye mashindano mengine. Arsenal wanarejea Emirates wakiwa na furaha kubwa, baada ya kuichapa Tottenham Hotspur mabao 4–1 ugenini.

H2H, Arsenal vs Chelsea

Palmer
Palmer

Arsenal wamekuwa na nyakati bora zaidi dhidi ya Chelsea ambao wamecheza dhidi yao katika michezo 214. Arsenal wameshinda mechi 87, Chelsea wao wameshinda mechi 66. Mechi 61 kati ya makutano yao zimemalizika kwa sare.

Fomu ya hivi karibuni

Katika michezo 6 ya Ligi Kuu England iliyopita Arsenal wameshinda mechi 3, sare 2 na kupoteza mchezo mmoja pekee. Kwa upande wa Chelsea wao katika mechi 6 zilizopita wamefanikiwa kushinda mechi 4 na kutoa sare mechi 2. Hivyo mchezo huu unakuja kuandika historia mpya.

SOMA HII ZAIDI: arsenal vs Chelsea- Ni Dabi ya London.

Vikosi vinavyowezekana kuanza Arsenal vs Chelsea

Arsenal:

Kipa: Raya

Walinzi: Timber, Saliba, Gabriel, Hincapie

Viungo: Zubimendi, Rice, Saka, Eze, Trossard

Mshambuliaji: Gyokeres

Chelsea:

Kikosi cha Chelsea (-)
Kikosi cha Chelsea

Kipa: Sanchez

Walinzi: James, Adarabioyo, Chalobah, Gusto

Viungo: Caicedo, Santos, Palmer, Fernandez, Neto

Mshambuliaji: Pedro

Habari za timu

Arsenal vs Chelsea
Big wins against the Blues &#x a; (-)

Staa wa Arsenal, Eberechi Eze amekuwa kwenye kiwango tangu usajili wake wa kipindiu cha majira ya joto. Miezi michache baada ya kufunga hat-trick ya kishujaa nyumbani Emirates, Eze wiki iliyopita alifunga tena mabao mawili dhidi ya Spurs na kuipa Arsenal ushindi wa mabao 4-1. Kikosi cha Mikel Arteta kimeonyesha kuanza kurudi kwenye kasi, baada ya kuangusha pointi saba katika michezo yao 6 iliyopita.

Ushindi huo uliifanya Arsenal kurejesha pengo la pointi tano kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu. Pengo hili linaweza kupungua ikiwa Manchester City walio na mechi mkononi wataifunga Leeds United leo Jumamosi.

Kikosi cha Arteta kinajitahidi kujenga tena uimara wao wa Uwanja wa nyumbani Emirates, mara baada ya kipigo cha kushangaza kutoka Manchester United Januari. Mpaka sasa wameshinda mechi nne mfululizo nyumbani, na kutoruhusu bao katika mechi zao tatu zilizopita. Katika michezo hiyo pia Arsenal wamefunga mabao 8.

Kwa upande wa takwimu za hivi karibuni, Chelsea wanaonekana kuwa bora zaidi. Wamekusanya pointi 14 kati ya 18 wakiangusha pointi 4 tu. Licha ya mafanikio hayo, dalili za udhaifu zimeanza kuonekana katika mradi wa Rosenior.

Mpaka sasa Chelsea walio katika nafasi ya tano, wamezidiwa pointi 3 na Manchester United walioko nafasi ya nne. Sare ya wiki iliyopita ina maana kwamba Blues bado hawajapoteza mechi yoyote ya ligi, tangu Rosenior achukue nafasi ya kocha. Swali ni je, anaweza kuwa meneja wa kwanza Mwingereza tangu Tim Sherwood msimu wa 2013–14, kushinda mechi zake tatu za kwanza za ugenini katika Ligi Kuu England?

SOMA HII PIA: Arsenal Fixtures: Men’s, Women’s and Academy Football in England

Taarifa ya majeruhi

Arsenal walipata hofu kuhusu jeraha la Bukayo Saka baada ya kuumia kifundo cha mguu dhidi ya Spurs, lakini Arteta hakutoa taarifa ya wasiwasi mkubwa na anatarajiwa kucheza. Kai Havertz anatarajiwa kurejea na huenda akajumuishwa, lakini Ben White bado ana hatihati ya kuwepo. Eze anatarajiwa kuanza, huku Odegaard akianzia benchi.

Kwa upande wa Chelsea, Rosenior atalazimika kufanya mabadiliko katika safu ya ulinzi baada ya Wesley Fofana kutolewa kwa kadi nyekundu dhidi ya Burnley. Fofana atakosa mechi moja, Tosin Adarabioyo anatarajiwa kuchukua nafasi yake. Marc Cucurella na Estevao Willian bado ni majeruhi, lakini pia hali za Dario Essugo na Filip Jorgensen bado hazijulikani.

Saka (-)
Saka

Hitimisho: Utabiri

Licha ya ugumu wa mchezo wenyewe bado derby ya Arsenal vs Chelsea inampa nafasi kubwa Arsenal ya ushindi. Nyota wa zamani wa Arsenal, Thierry Henry, amekiri kuwa ana wasiwasi zaidi na Chelsea kuliko Spurs. Hata hivyo, kama Chelsea watafunga bao la kwanza, huenda isiwe rahisi kwa Arsenal kushinda.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.