- Moto unazidi kuwaka ndani ya kikosi cha Simba SC.
- Wakati timu hiyo leo ikitangaza kuingia makubaliano ya mkataba wa kuandaa kadi za Wanachama, Mfadhili wao Mohammed Dewji ‘MO Dewji Simba’ amechafua hali ya hewa.
- Hii ni baada ya kuibuka na swali zito kwa uongozi wa Murtaza Mangungu.
Moto unazidi kuwaka ndani ya kikosi cha Simba SC. Wakati timu hiyo leo ikitangaza kuingia makubaliano ya mkataba wa kuandaa kadi za Wanachama, Mfadhili wao Mohammed Dewji ‘MO Dewji Simba’ ameibuka na swali zito kwa uongozi wa Simba SC. MO ametoa hayo yake ya moyoni kupitia ujumbe alioweka kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram.
SOMA HII PIA: Usajili wa Simba SC dirisha dogo balaa! Gueye, Kibabage, Loemba
Cheza na ushinde sasa na ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni muda huu
Kumbuka unaweza kuwa mshindi mpya wa mamilioni ya SportPesa muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kucheza kupitia Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa bonyeza picha hii chini.

Nini kimetokea leo kwa viongozi na MO Dewji Simba?

Uongozi wa Simba SC leo Februari 10, 2026 ulitoa taarifa ya kufanya mkutano na waandishi wa Habari ili kutoa taarifa kwa Umma. Kupitia mkutano huo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba SC, Crescentius Magori alisema: “Leo tumekusanyika hapa kwa jambo la muda mrefu, ambalo limesubiriwa sana. Tulikuwa tunatafuta kampuni ya uhakika kutengeneza kadi za Simba, kadi ambazo zinafanana na timu kubwa kabisa Afrika.
“Bodi ya Wakurugenzi inapenda kuitangaza kampuni ya Mainstream Group kuwa ndio itatengeneza mfumo wa kileo na za kisasa na imeichagua kampuni ya Nexus kutoa kadi hizi za wanachama. Kadi hizi zitakuwa aina ya VISA, pamoja na kukutambua kwamba ni mwanachama wa Simba lakini pia unaweza kuweka pesa, ukafanya malipo na miamala.”
Mangungu naye afunguka

Naye, Murtaza Mangungu ambaye ni mwenyekiti wa Simba na Makamu mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi alisema: “Tumeingia mkataba na wenzetu Mainstream Group na Nexus Pesa, utoaji wa kadi utafata katiba ya Simba kuanzia ngazi ya matawi hadi ngazi ya makao makuu ya klabu. Ni wakati muafaka kwa wanachama, hasa kwenye ngazi ya matawi na tutaanza usajili wa matawi hivi karibuni. Tumepanga kuanza kutoa kadi Machi 27, 2026. Tunafanya hivyo sababu kuna mambo mengi na kuna taasisi nyingi, zinahusika katika maandalizi ya utoaji wa hizo kadi.”
“Zoezi hili kwetu lina faida kwa sababu litahuisha wale waliokuwa na kadi na wakapoteza, wale ambao walikuwa wanahitaji lakini pia kuboresha taarifa. Hii itatusaidia sana kuboresha, kuwa na rekodi na taarifa sahihi kuhusu wanachama. Kadi zetu za uanachama zitafata utaratibu unaotakiwa kwenye katiba kwamba maombi yatawasilishwa kwenye matawi. Tutakuwa pia na matawi kwa watu ambao wapo nje ya nchi. Utaratibu wa kupata kadi ni uleule ambao ulikuwepo awali.”
SOMA HII ZAIDI: Ishu ya Chama kurudi Simba SC ukweli huu hapa! Kipa mpya atambulishwa: Tetesi za usajili mpya Ligi Kuu Bara 2025/26
Mfumo wa upatikanaji wa kadi hizo utakuwaje?
Naye Mkurugenzi Mwendeshaji wa Mainstream Group, Deogratius Mosha amesema: “Tumeingia makubaliano kwa ajili ya kutengeneza mfumo wa kuwezesha, wanachama kutambulika na kupewa kadi zao za uanachama. Jambo moja ambalo tunaahidi, utakuwa ni mfumo rafiki ambao utatumika na mtu yeyote. Kupitia kwenye mfumo huu wa Simba tutawezesha wanachama kujisajili, na kuiwezesha Simba kupata taarifa mbalimbali.
“Mifumo tayari tumeshaitengeneza kwa mahitaji hayo na lengo ni kila Mwanasimba popote alipo, bila gharama za ziada apate kadi yake. Tutatoa kadi za aina mbili, virtual card na kadi za kawaida. Ni mfumo wa kipekee kuwahi kutokea kwenye ukanda wa Afrika.”
Naye Mkurugenzi wa Nexus, Rajab Thabit amesema: “Kazi yetu ya msingi sisi ni kuunganisha mfumo ambao unatengenezwa na Mainstream Group na Simba, na kuhakikisha mwanachama anapata kadi pale alipo. Kitu cha msingi ni kadi ambazo zitaenda kwa wanachama, hazitakuwa na makato ya mwezi. Kadi ya Simba ambayo inakwenda kwa wanachama ni za Visa na wataweza kutoa pesa kwenye ATM.”
MO Dewji aibuka na swali zito

Kufuatia machapishio hayo, Mwekezaji na Rais wa heshima wa Simba SC, Mohammed Dewji kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Instagram alijibu kwa kuandika ujumbe uliosomeka: “Transformation mmefikia wapi.” Hali hii ilizua mjadala mkubwa miongoni mwa mashabiki, na wadau wa timu hiyo walioendelea kutoa maoni yao.
SOMA HII PIA: Usajili wa Chama Simba SC washtua! Mayele, Kagere, Okwi wafunguka Mazito
Hitimisho
Ni wazi kuna Sintofahamu kubwa ndani ya kikosi cha Mnyama kwa sasa, viongozi wa upande Wanachama wakiongoza na Mwenyekiti wao, Murtaza Mangungu wanapishana mtazamo na MO Dewji Simba SC. Hii haileti afya ya soka letu n ani wakati wa kila upande kutumia hekima na kuamua kwa faida na maslahi mapana ya timu hiyo. Pande hizi zinapaswa kutambua Simba SC ni taasisi yenye heshima kubwa sio tu, Tanzania lakini kimataifa.

