- Hawatanii, ndivyo unavyoweza kusema baada ya Uongozi wa Yanga kutoa majibu mazito juu ya ujenzi wa Uwanja.
- Rais wa Yanga SC, Injinia Hersi Said siku ya Jumamosi aliongoza Mkutano Maalum, wa Kamati Tendaji kujadili kuhusu mradi wa ujenzi wa Uwanja wa Yanga SC.
- Kikao hicho kimefikia maamuzi ya kuichagua na kuitangaza Kampuni ya GSM Tanzania Limited iliyo chini ya Bilionea GSM kushinda tenda ya ujenzi huo.
- Tayari uongozi wa Yanga SC ulitenga kiasi cha Shilingi Bilioni 1 kwa maandalizi ya ujenzi.
Suala la mchakato wa ujenzi wa Uwanja wa Yanga SC limezidi kushika kasi, ambapo mara baada ya kukamilisha mchakato wa hati ya eneo la Jangwani. Uongozi wa Yanga SC umefikia maamuzi ya kuitangaza Kampuni ya GSM Tanzania Limited, iliyo chini ya Bilionea GSM kushinda tenda ujenzi huo. Tayari uongozi wa Yanga SC ulitenga kiasi cha Shilingi Bilioni 1 kwa mchakato wa maandalizi ya ujenzi.
SOMA HII PIA: Ujenzi Uwanja wa Yanga SC balaa! Injinia Hersi afanya kikao Kizito
Cheza na ushinde sasa na ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni muda huu
Bado hujashinda na kindege cha SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kupitia Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa bonyeza picha hii chini.

Kuhusu ujenzi Uwanja wa Yanga SC

Taarifa rasmi kutoka Yanga SC iliyotolewa na Ofisa Habari wa Yanga SC, Ali Kamwe ni kuwa Rais wa Klabu ya Young Africans SC, Eng. Hersi Said siku ya Jumamosi ya Januari 31, mwaka huu aliongoza Mkutano Maalum. Mkutano huu ni wa Kamati ya Utendaji ulikuwa na agenda moja pekee. Ajenda hiyo ilikuwa kujadili kuhusu mradi wa Uwanja.
Mkutano huo ulihudhuriwa ana kwa ana na wajumbe wa Kamati ya Utendaji, pamoja na wengine kufuatilia kupitia njia ya mtandao.
SOMA HII ZAIDI: Mkutano mkuu wa Yanga SC 2025: Mambo 10 yaliyotikisa ‘Super Dome’ leo
Ali Kamwe atoa mrejesho wa Kikao

Ofisa Habari wa Yanga SC, Ali Kamwe amesema: “Siku ya Jumamosi uongozi wetu ulikaa kikao cha kamati ya Utendaji inayoongozwa na Rais Eng. Hersi Ally Said. Katika kikao hicho kulikuwa na agenda moja ya Msingi ya Mchakato wa ujenzi wa uwanja wa Young Africans Sports Club. Kikao kile kilikwenda kutoa majibu ya kampuni, au Taasisi iliyoshinda tenda ya kushirikiana na Yanga SC kwenye ujenzi wa uwanja wa Yanga.
“Kabla hatujamtaja mshindi wa Tenda hii naomba niwapitishe kwenye mchakato mzima wa Ujenzi wa Uwanja huu, Mchakato huu umepita kwenye hatua mbali mbali. Hatua ya kwanza ilikuwa kufanya Tathmini ya eneo la ujenzi wa uwanja, baadae tukagundua kuwa kuna Eneo la ziada linahitajika kwenye kukamilisha ujenzi huo. Baadae tukashirikiana na Serikali kuomba eneo la ziada.
Yanga wamshukuru Rais Dkt. Samia
“Hapa nichukue Fursa hii kuishukuru Serikali chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia Eneo la ziada. Nichukue fursa hii kuwatangazia Watanzania, Kampuni ya GSM TANZANIA LIMITED ndiyo iliyoshinda tenda ya Ujenzi wa Uwanja wa Young Africans Sports Club. Taratibu za ujenzi zinatarajiwa kuanza mara moja pale maandalizi yatakapokamilika,” amesema Kamwe.
Sakata la uwanja ni ahadi ya muda mrefu ya Rais Hersi ambayo bado haijatimizwa. Hivi karibuni kupiti mkutano mkuu wa mwaka uliofanyika Super Dome mwaka jana, Serikali ilitoa ahadi ya kukamilisha mchakato wa hati ya Uwanja huo ndani ya wiki 2. Jambo hilo lilitimia katika kilele cha Tamasha la wiki ya Mwananchi kwenye Uwanja wa Mkapa. Katika tukio ambalo limevuta hisia za mashabiki wengi wa Yanga, ni kukabidhiwa kwa hati yao ya eneo la uwanja. Tukio hilo lilifanyika kwenye kilele cha wiki yam wananchi, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.
SOMA HII PIA: Yanga SC vs AS FAR 22/11/2025: Kazi imeanza, Wananchi watoa tamko zito
Bilioni 1 yatengwa kuanza hatua za awali za ujenzi

Yanga SC kupitia kwa makamu mwenyekiti wao, Arafat Haji kwemye mkutwno mkuu wa mwaka jana waliweka wazi kuwa kwa kuanza wameandaa Bilioni 1 kwa ajili za hatua za awali za ujenzi. Ikumbukwe mradi huo wa ujenzi wa Uwanja wa Yanga SC, unafanywa kwa mashirikiano na Serikali, ambayo ina mradi mkubwa wa mto Msimbazi.
Miradi tanzu ya baadaye, inayoendana na ujenzi wa uwanja Yanga SC

Ukiachana na mradi wa ujenzi wa uwanja, uongozi wa Yanga SC umetangaza mipango yao mizito ya baadae. Kati ya miradi hiyo ni suala la kukuza soka la vijana na Wanawake. Kwa sasa uongozi umesema unatazama hilo kama fursa ya kibiashara kuuza wachezaji nje ya nchi. Pamoja na hayo uongozi wa timu hiyo pia umeweka wazi mipango ya kuimarisha timu hiyo kiuchumi. Hii ni katika mkakati wa kuongeza mapato kupitia usajili wa wanachama na wateja wapya, pamoja na wadhamini wapya.
Hitimisho
Mipango hii ya muda mrefu ya Ujenzi Uwanja wa Yanga SC inadhihirisha uthabiti wa Yanga SC kuwa klabu bora na iliyojipanga kufanya maendeleo endelevu. Pia hii inaelezea utashi wa kuhakikisha wanachama wanashirikishwa, usawa wa kifedha na kuwa mstari wa mbele kwa miundombinu. Hii ni katika kukuza soka la bongo.

