Vurugu Fainali AFCON ----Vurugu Fainali AFCON ----
  • Shirikisho la Soka Afrika (CAF), kupitia Kamati yake ya nidhamu limechukua hatua kali za kinidhamu dhidi ya timu ya Taifa ya Senegal na Morocco na mastaa wao.
  • Hii ni baada ya mfululizo wa matukio ya kutatanisha, wakati wa mchezo wa fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2025), iliyopigwa mjini Rabat.
  • Maamuzi haya yamekuja baada ya ukaguzi kamili wa Bodi ya Nidhamu ya CAF, kufuatia matukio hayo yaliyotokea kwenye fainali ya Januari 18, mwaka huu.
  • Baadhi ya Mastaa wakiwemo Hakimi na Ndiaye wamefungiwa

Shirikisho la Soka Afrika (CAF), kupitia Kamati yake ya nidhamu limechukua hatua kali za kinidhamu dhidi ya timu ya Taifa ya Senegal na Morocco na mastaa wao. Hii ni baada ya mfululizo wa matukio ya kutatanisha, wakati wa mchezo wa fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2025), iliyopigwa mjini Rabat. Maamuzi haya yamekuja baada ya ukaguzi kamili wa Bodi ya Nidhamu ya CAF, kufuatia matukio hayo yaliyotokea kwenye fainali ya Januari 18, mwaka huu.

SOMA HII PIA: AFCON 2025: Matokeo na Ratiba ya Robo Fainali, hizi hapa timu zilizofuzu

Je, Unataka kushinda pesa? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa

Ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege kupitia kampuni bora ya kubashiri ya SportPesa. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

image

Hizi hapa adhabu kufuatia vurugu za Fainali ya AFCON 2025

Adhabu kwa Senegal

AFCON 2025
Mane akiwarudisha wenzake

Timu ya taifa ya Senegal ndio waliibuka mabingwa kwa ushindi wa bao 1-0, katika muda wa ziada baada ya sare ya muda wa kawaida ziada. Katika hekaheka hii, Senegal wameshushiwa Rungu zito zaidi kufuatia ukiukaji kadhaa wa kanuni za CAF. Kocha mkuu, Pape Bouna Thiaw amefungiwa mechi tano na kutozwa faini ya dola 100,000 za Marekani kwa utovu wa nidhamu nah atua zisizokuwa za kiuanamichezo zilizopelekea mchezo huo kuchafuka.

Wachezaji wawili wa kimataifa wa Senegal, Iliman Cheikh Baroy Ndiaye na Ismaïla Sarr, wamefungiwa kila mmoja mechi mbili za CAF kwa utovu wa nidhamu dhidi ya mwamuzi. Wakati huo huo, Shirikisho la Soka la Senegal (FSF), limetozwa faini ya dola 615,000 za Marekani. Jumla hiyo ni pamoja na $300,000 kwa vurugu za mashabiki wao, $300,000 nyingine ni kwa utovu wa nidhamu wa wachezaji na wafanyikazi wa benchi la ufundi wakati wa fainali. $15,000 za ziada kwa utovu wa nidhamu wa timu wakati wa fainali.

Adhabu kwa Morocco

Hakimi na Gueye
Hakimi na Gueye

Morocco nao wamekumbana na Rungu hilo ambapo beki, Achraf Hakimi amepewa adhabu ya kufungiwa mechi mbili. Kiungo, Ismaël Saibari amepewa adhabu ya kutocheza mechi tatu na kutozwa faini ya $100,000 kwa utovu wa nidhamu. Shirikisho la Soka la Kifalme la Morocco (FRMF), limetozwa faini ya $315,000 kwa uvunjaji wa sheria nyingi.

Hizi zilijumuisha mwenendo usiofaa wa wavulana wa kuokota mipira ‘ball boys’, wachezaji na maofisa wengine kuingilia eneo la ukaguzi wa VAR, na matumizi ya viashiria vya taa za leza kwa mashabiki wao. Vitendo vyote vinavyoonekana kama ukiukaji wa kanuni za michezo.

Morocco ilikuwa inajipanga kukata rufaa ya kutaka kutengua matokeo, ambayo kwa sehemu yalihusiana na Senegal kuondoka uwanjani. Hata hivyo, bodi ya nidhamu ya CAF ilikataa rufaa hiyo na kuthibitisha kwamba ushindi na taji la Senegal bado ni halali. Bado kumekuwa na mvutano katika hilo.

SOMA HII ZAIDI: AFCON 2025 final Senegal vs Morocco: Ratiba, Live score, lineups, h2h, prediction, Habari za timu

Hitimisho: Kuhusu adhabu za CAF

Nahodha wa Senegal na mwamuzi
Nahodha wa Senegal na mwamuzi

Adhabu za CAF zinaangazia umuhimu uliowekwa katika nidhamu, na heshima ndani ya mashindano kuu ya kandanda barani Afrika. Vitendo vinavyohusisha maafisa, wachezaji, wafanyakazi na wafuasi vinavyokiuka kanuni za uchezaji wa haki sasa vinakabiliwa na madhara makali. Hii haina msamaha hata vinapotokea kwenye jukwaa kubwa zaidi.

Adhabu hizo zinatumika kwa mashindano ya CAF pekee, kumaanisha kuwa yataathiri mashindano ya Bara la Afrika yajayo. Hivyo adhabu hizi sio lazima ziathiri mashindano ya kimataifa kama vile Kombe la Dunia, isipokuwa kanuni tofauti zitatumika. Hatua hizi za kinidhamu zinalenga kuimarisha viwango vya soka barani Afrika, pia kuwa ukumbusho kwamba mwenendo ndani na nje ya uwanja unaangaliwa huku mchezo ukiendelea kukua barani kote.

AFCON 2025: Mabingwa Senegal wapewa mapokezi ya Kihistoria Dakar

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.