- Barker ameanza kwa sare mchezo wa kwanza akiwa na kikosi cha Simba SC
- Simba SC 1-1 Mtibwa Sugar NBC Premier League
- Ellie Mpanzu afunga goli la kwanza 2025/26 Meja Isahmuyo
Simba SC 1-1 Mtibwa Sugar ni matokeo kamili mchezo wa NBC Premier League 2025/26. Kocha Mkuu Steve Barker ameanza kwa kugawana pointi moja akiwa nyumbani. Ellie Mpanzu alifunga goli la utangulizi ikiwa ni mara ya kwanza kufunga kwenye ligi. Ni baada ya ligi kurejea kutokana na kusimama kwa muda kupisha AFCON 2025.
SOMA HII: Mechi za Simba SC 2025/26 CAF Champions League, NBC Premier League ni moto| Matokeo na wafungaji
Unasubiri nini? Vuna mamilioni sasa hivi
Kuna jambo umekwama kwa sasa kuhusu mkwanja? Usiogope, rubani ni jasiri na kazi yake ni kupaisha kindege cha SportPesa. Cheza sasa hivi Aviator uvune mamilioni bofya hapa chini.

Simba SC 1-1 Mtibwa Sugar, NBC Premier League

Burudani iliyokuwa imesimama kwa muda imerejea na matokeo ilikuwa Simba SC 1-1 Mtibwa Sugar, NBC Premier League. Ni Mpanzu alianza kufunga goli la utangulizi dakika ya 19. Goli hilo lilidumu mpaka muda wa mapumziko.
Kipindi cha pili, Mtibwa Sugar waliongeza mashambulizi kwa wapinzani Simba SC. Dakika ya 61 walipachika goli la kuweka usawa. Ni Magata Fredrick alifunga goli hilo. Lilidumu mpaka mwisho wa mchezo.
Unakuwa ni mchezo wa kwanza kwa timu hizi mbili msimu wa 2025/26 kukutana Uwanja wa Mej Isamuhyo mapema saa 10:00 jioni. Goli la kwanza kwa Mpanzu ndani ya ligi limeipa Simba SC pointi moja.
Msimamo wa Ligi Kuu Bara 2025/26
| Timu | P | W | D | L | P | GF |
| 4. Simba SC | 6 | 4 | 1 | 1 | 13 | 12 |
| 8. Mtibwa Sugar | 9 | 2 | 5 | 2 | 11 | 5 |
Barker ameanza na pointi moja
Kocha Mkuu wa Simba SC, Steve Barker mchezo wake wa kwanza kwenye ligi ameambulia pointi moja. Hakuna mbabe ambaye ameondoka na pointi tatu zote. Mtibwa Sugar walikuwa nyuma wakazawazisha goli kutokana na makosa ya safu ya ulinzi.
Ikumbukwe kwamba Barker alianza kazi na kikosi kwenye NMB Mapinduzi ambapo waliishia hatua ya nusu fainali. Simba SC ilipoteza kwa kufungwa goli 1-0 dhidi ya Azam FC ambao walikwenda kucheza na Yanga SC hatua ya fainali.
SOMA HII: NBC Premier League table 2025/26

Kikosi cha Simba SC
Hussen Abel
Shomari Kapombe
Anthony Mligo
Mohamed Bajaber
Yusuph Kagoma
Rushine De Reucky
Naby Camara
Wilson Nangu
Ellie Mpanzu
Neo Maema
Seleman Mwalimu

Kikosi cha Mtibwa Sugar
Costantine Malimi
Datius Peter
Haroun Evod
Ezekia Mwashilindi
Said Mkopi
Chikwuemeka Collins
Twalibu Muhenga
Omary Manga
Kassim Shaibu
Andrea Simchimba
Magata Charles
Hitimisho
Simba SC 1-1 Mtibwa Sugar NBC Premier League kazi imeanza kwa mara nyingine tena. Nyota Haroun Evody alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo. Matokeo na ratiba za ligi utaendelea kuzipata hapa.

