- Hatua ya Nusu Fainali ya Mashindano ya AFCON 2025, itaanza kutimua vumbi rasmi kesho Jumatano.
- Mechi zote zinasubiriwa kwa hamu huku wenyeji Morocco wakikabiliwa na kibarua kigumu kwenye mechi ya Nigeria vs Morocco.
- Licha ya kuwa wenyeji wa mashindano, Morocco kesho watakuwa wageni katika mchezo unaotarajiwa kuwa mgumu sana.
Kesho ndiyo kesho! Kinanawaka huko Morocco katika mashindano ya AFCON 2025. Mashindano hayo yameingia katika hatua ya Nusu Fainali, ambapo timu nne zitashuka uwanjani kusaka wanafainali wapya. Nigeria vs Morocco ndio mchezo unaotajwa kuvuta hisia za watu wengi zaidi. Makala hii inakuletea dondoo muhimu, kuhusu mchezo huo was aa 5 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
SOMA HII PIA: AFCON 2025: Matokeo na Ratiba, hizi hapa timu zilizofuzu hatua ya mtoano (16 bora)
Bado hujashinda pesa? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa
Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

H2H, Nigeria vs Morocco

Rekodi ya historia ya soka la ushindani kati ya Nigeria na Morocco inaonyesha timu hizi zimekutana mara 11. Nigeria imeshinda mechi 4 tu, huku Morocco wakiwa wababe kwa kushinda mechi 6. Mechi 1 zilizosalia zilimalizika kwa matokeo ya sare.
Fomu ya Nigeria kwenye mechi 5 zilizopita
WWWWW
Fomu ya Morocco katika mechi 5 zilizopita:
WDWWW
Vikosi tarajiwa Nigeria vs Morocco

Nigeria
Kipa: Nwabali
Walinzi: Osayi-Samuel, Ajayi, Bassey, Onyemaechi
Viungo: Onyeka, Onyedika, Iwobi
Washambuliaji: Lookman, Adams, Osimhen
Morocco
Kipa: Bono
Walinzi: Hakimi, Aguerd, Masina, Mazraoui
Viungo: El Khannouss, El Aynaousi, Saibari
Washambuliaji: Diaz, Ezzalzouli, El Kaabi
SOMA HII ZAIDI: AFCON 2025: Matokeo, hawa hapa wafungaji bora kabla ya Ratiba ya 16 bora, Feisal na Msuva wamo?
Habari za timu

Mechi hii inatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa, Prince Moulay Abdellah mjini Rabat. Hii ni moja ya nusu fainali mbili zinazoshirikisha baadhi ya wachezaji bora wa Afrika. Baadhi ya mastaa hao ni washindi wa hivi karibuni wa tuzo ya Mchezaji Bora wa CAF amba oni; Mohamed Salah, Sadio Mane, Victor Osimhen, Ademola Lookman na Achraf Hakimi, wote waliwakilishwa kati ya mataifa manne yaliyosalia.
Nigeria imekuwa moja ya timu bora katika mashindano hayo, hasa baada ya kukatishwa tamaa kwa kukosa kufuzu kwa Kombe la Dunia la FIFA la 2026. Hii ni kufuatia kichapo cha mchujo kutoka kwa DR Congo mwezi Novemba. Wakisimamiwa na kocha raia wa Mali, Eric Chelle, Super Eagles wanaendelea kubeba uzito wa matarajio unaokuja na historia ya kuwa mabingwa mara tatu wa Afrika.
Katika mashindano yam waka huu Nigeria ilifungua dimba kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Tanzania. Ikafuatiwa na ushindi wa 3-2 dhidi ya Tunisia na kujihakikishia kufuzu mapema, kabla ya kuifunga Uganda 3-1 katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi. Kwenye hatua ya mtoano waliifunga Msumbiji 4-0 na kuichapa Algeria 2-0 kwenye robo fainali.
Safari ya Morocco ilishuhudia wakiongoza Kundi A wakiwa na pointi saba baada ya ushindi dhidi ya Comoro (2-0) na Zambia (3-0) na sare dhidi ya Mali (1-1). Katika hatua ya mtoano Morocco iliwatoa Tanzania na kuichapa Cameroon mabao 2-0 kwenye Robo Fainali. Nyota wa Real Madrid, Brahim Diaz ameendelea kuwa na kiwango bora kwenye mashindano hayo.
Diaz amefunga katika mechi tano mfululizo na kuwa mchezaji wa kwanza katika miaka 15 kufunga katika mechi tano za kwanza za AFCON. Tofauti na mbinu ya Nigeria ya kufunga mabao, nguvu ya Morocco imejengwa katika uimara wa safu ya ulinzi. Mpaka sasa wamefungwa bao moja pekee. Bao hilo lilikuwa la mpira wa kutenga.
Taarifa ya majeruhi

Nigeria imepata pigo kubwa kabla ya nusu fainali baada ya nahodha Ndidi kupata adhabu ya kufungiwa, hivyo ataendelea kukosekana. Pia kuna wasiwasi kuhusu utimamu wa mwili wa, Bright Osayi-Samuel baada ya kulazimishwa kutoka dakika za lala salama dhidi ya Algeria. Straika wa Panathinaikos, Cyriel Dessers ameondolewa kikosini kutokana na jeraha la paja.
Kwa kurejea kwa nahodha Hakimi kumeinua kikosi hicho, ingawa kiungo Azzedine Ounahi yuko nje ya uwanja baada ya kupata majeraha. Romain Saiss bado hajapatikana baada ya kuumia dhidi ya Comoro. Diaz, ambaye alikuwa na mchango mkubwa katika kuwapeleka wenyeji katika nusu-fainali, anatarajiwa kuongoza safu ya ushambuliaji dhidi ya Nigeria.
SOMA HII PIA: AFCON 2025 hatua ya makundi matokeo na ratiba/ Msimamo, tarehe
Hitimisho
Nigeria inaonekana kuwa na hasira ya kusaka ushindi na tiketi ya fainali, huku Morocco wakijivunia faida ya mashabiki wao. Nusu Fainali ya AFCON 2025 inatarajiwa kuwa yamoto sana hasa kutokana na ubora wa kila timu. Nigeria vs Morocco utakuwa kivutio kikubwa huku Nigeria wakipewa nafasi kubwa kushinda.

