- Moto utawaka Jumapili hii nchini Morocco kwenye mashindano ya Kombe la Mataifa Afrika AFCON 2025.
- Ni pale timu mwenyeji Morocco vs Tanzania, mchezo ambao una thamani ya tiketi ya Robo Fainali.
- Makala hii inaangazia baadhi ya dondoo muhimu za mchezo huo.
Hatumwi mtoto dukani! Moto utawaka Jumapili hii nchini Morocco kwenye mashindano ya Kombe la Mataifa Afrika AFCON 2025. Ni mechi ya Morocco vs Tanzania inayotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa. Makala hii inaangazia baadhi ya dondoo muhimu za mchezo huo.
SOMA HII PIA: AFCON 2025: Matokeo, hawa hapa wafungaji bora kabla ya Ratiba ya 16 bora, Feisal na Msuva wamo?
Bado hujashinda pesa? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa
Changamka! sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

H2H, Morocco vs Tanzania

Katika historia ya soka la ushindani Tanzania na Morocco zimekutana katika michezo 7. Tanzania imeshinda mchezo mmoja tu, dhidi ya Morocco huku Morocco wao wakishinda mechi 6. Hakuna mchezo kati ya timu hizi ulioisha kwa sare.
SOMA HII ZAIDI: AFCON 2025 hatua ya makundi matokeo na ratiba/ Msimamo, tarehe
Mechi 5 zilizopita za Tanzania
Tanzania 1-1 Tunisia
Uganda 1-1 Tanzania
Nigeria 2-1 Tanzania
Kuwait 4-3 Tanzania
Iran 2-0 Tanzania
Mechi 5 zilizopita za Morocco
Zambia 0-3 Morocco
Morocco 1-1 Mali
Morocco 2-0 Comoros
Jordan 2-3 Morocco
Morocco 3-0 UAE
Vikosi vinavyotarajiwa kuanza
Kikosi cha Morocco
Kipa: Bono
Walinzi: A. Hakimi, N. Aguerd, A. Masina, N. Mazraoui
Viungo: N. El Aynaoui, A. Ounahi, B. Díaz, I. Saibari, A. Ezzalzouli
Mshambuliaji: A. Kaabi
Tanzania

Kipa: Foba
Walinzi: Kapombe, Mwamnyeto, Hamad, Hussein
Viungo: Mirishi, Msanga, Msuva, M’Mbobwa, Allarkhia
Mshambuliaji: Samatta
Habari za timu

Tanzania ilianza vibaya kwa kupoteza kwa mabao 2-1 mbele ya Nigeria, katika mchezo wa kwanza wa mashindano hayo. Lakini vijana wa kocha Miguel Gamondi wakafanya kweli katika michezo miwili iliyosalia, ambapo wamefanikiwa kuvuna pointi 2 dhidi ya Uganda na Tunisia. Hii imewafanya kuandika rekodi ya kufuzu hatua ya mtoano kwa mara ya kwanza katika mashindano hayo.
Tanzania haijawa kwenye fomu nzuri hivi karibuni, kwani hawajapata ushindi wowote ndani ya michezo 8 mfululizo iliyopita. Wamepoteza michezo 6 na kutoa sare mechi 4 na za michuano yote (D4, L6), huku mechi zao tano mfululizo zilizopita wakipata vipigo vitatu na sare 2.
Sare yao dhidi ya Tunisia kwenye mechi iliyopita kumefanya waandikishe mechi 12 bila ushindi kwenye mashindano ya AFCON. wamefungwa mara 7 na kutoa sare 5.
SOMA HII PIA: AFCON 2025 Mahrez, Jackson, Achouri watikisa: Hawa hapa wafungaji bora wa Raundi ya 1
Taarifa za majeraha
Kuhusu majeraha, Morocco wana wasiwasi juu ya Romain Saiss ambaye alipata majeraha ya misuli kwenye mchezo wa Comoros. Huyu ndiye mchezaji pekee ambaye anaweza kuukosa mchezo na wengine wapo fiti. Kwa Tanzania kipa wao, Foba alionekana kujifua na wenzake baada ya majeraha aliyopata kwenye mechi dhidi ya Uganda.
Hitimisho
Morocco vs Tanzania ni zaidi ya mchezo kwa Watanzania na Wamorocco. Wmamorocco wanacheza nyumbani mbele ya mashabiki wao, hivyo watapambana wasifanye makosa. Lakini Tanzania ya kizazi kipya inaweza kuushangaza Umma wa soka, kikosi chao kimekuwa na maendeleo makubwa siku za karibuni.

