- Timu ya Taifa ya Senegal imeandika rekodi kwenye mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2025).
- Hii ni baada ya kuwa timu ya kwanza kufuzu hatua ya Robo Fainali ya mashindano hayo.
- Makala hii inakuletea matokeo na Ratiba yah atua ya 16 bora na timu zipi zinatarajia kuvaana kwenye Robo Fainali.
Taifa la Senegal limeandika rekodi mpya, ya mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2025). Hii ni baada ya kuwa timu ya kwanza, kufuzu hatua ya Robo Fainali ya mashindano hayo ya mwaka huu.Makala hii inakuletea matokeo na Ratiba ya hatua ya 16 bora, na timu zipi zinatarajia kuvaana kwenye Robo Fainali.
SOMA HII PIA: AFCON 2025: Matokeo, hawa hapa wafungaji bora kabla ya Ratiba ya 16 bora, Feisal na Msuva wamo?
Hujashinda pesa? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa
Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

AFCON 2025 Senegal haoo Robo Fainali

Timu ya Taifa ya Senegal muda mchache uliopita imefanikiwa kutinga hatua ya Robo Fainali ya AFCON 2025. Hii ni baada ya kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Sudan. Shukrani kwa mabao mawili ya Pape Gueye, ambayo yalitoa mchango mkubwa katika mchezo huo.
Senegal sasa anasubiri mshindi wa mchezo wa Mali vs Tunisia kuona nani atakuwa mpinzani wake wa Robo Fainali. Ikumbukwe mchezo huo wa Mali vs Tunisia unapigwa usiku huu. Timu hizo zote mbili zinaingia katika mchezo huu zikiwa zimetoka kupata matokeo ya sare, kwenye mechi zao za mwisho hatua ya makundi.
SOMA HII ZAIDI: AFCON 2025 matokeo na ratiba hii hapa/ Msimamo, live scores
Ratiba kamili ya mechi zilizobaki za hatua ya 16 bora AFCON 2025 ni kama ifuatavyo;

Jumamosi, Januari 3, 2026
Mali vs Tunisia saa
Jumapili, Januari 4, 2026
Morocco vs Tanzania
Afrika Kusini vs Cameroon
Jumatatu, Januari 5, 2026
Misri vs Benin
Nigeria vs Msumbiji
Jumanne, Januari 6, 2026
Algeria vs Dr Congo
Ivory Coast vs Burkina Faso
Nani na nani kukutana Robo Fainali AFCON 2025


Ratiba ya mechi kuelekea Fainali AFCON 2025
Wakati mashabiki wakisubiri kwa hamu timu zitakazofuzu Robo Fainali, swali ni timu zipi zitakutana katika hatua hiyo? Hapo juu ni maelezo kwa picha ya timu zipi zitakutana katika vita ya kuisaka Fainali ya mwaka huu.
SOMA HII PIA: AFCON 2025: Matokeo na Ratiba, hizi hapa timu zilizofuzu hatua ya mtoano (16 bora)
Hitimisho
Mashindano ya AFCON 2025 yamekuwa na msisimko mkubwa. Punde baada ya kuanza yameshafika hatua ya 16 bora, hapa kila timu inabidi kupambana kusaka tiketi ya Robo Fainali. Wengi wanapima uzito wa bingwa mtetezi Ivory Coast kuona je, ataweza kutetea ubingwa wake?

