- Vita ni vita! Huko Morocco ambapo mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), yanazidi kutimua vumbi.
- Katika Matchday 2 leo Jumamosi kuna chezo mkali wa Nigeria vs Tunisia AFCON 2025.
- Mchezo huu wa Kundi C unatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Fez majira ya saa 5 za usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
- Makala hii inaangazia dondoo muhimu za mtanange huo.
Vita ni vita! Huko Morocco ambapo mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2025), yanazidi kutimua vumbi. Katika Matchday 2 leo Jumamosi kuna chezo mkali wa Nigeria vs Tunisia. Mchezo huuunatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Fez majira ya saa 5 za usiku kwa saa za Afrika Mashariki. Makala hii inaangazia dondoo muhimu za mtanange huo.
SOMA HII PIA: AFCON 2025 matokeo na ratiba hii hapa/ Msimamo, live scores
Je, hujashinda pesa? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa
Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.]

H2H, Nigeria vs Tunisia
Timu hizi zimekutana katika michezo 11 ya mashindano tofauti, ambapo Nigeria wamekuwa na rekodi nzuri zaidi. Katika michezo 11, Nigeria wamefanikiwa kushinda mechi 3, huku Tunisia wakiibuka na ushindi katika mechi 2 na michezo 6 iliyosalia ikimalizika kwa matokeo ya sare. Ushindi kwa yoyote kati ya timu hizi, utashuhudia aliyeshinda akifuzu moja kwa moja hatua ya 16 bora.
Mechi 5 zilizopita za Nigeria
Nigeria 2-1 Tanzania
Nigeria 2-1 Egypt
Nigeria 1-1 Congo DR
Nigeria 4-1 Gabon
Nigeria 4-0 Benin
Mechi tano zilizopita za Tunisia
Tunisia 3-1 Uganda
Tunisia 2-1 Botswana
Tunisia 0-3 Qatar
Tunisia 2-2 Palestine
Tunisia 0-1 Syria
Vikosi tarajiwa Nigeria vs Tunisia AFCON 2025

Nigeria
Kipa: Nwabali
Walinzi: Osayi-Samuel, Ajayi, Bassey, Sanusi
Viungo: Ndidi, Iwobi, Dele-Bashiru
Washambuliaji: Chukwueze, Osimhen, Lookman.
Tunisia
Kipa: A. Dahmen
Walinzi: Y. Valery, D. Bronn, M. Talbi, A. Abdi
Viungo: F. Sassi, E. Skhiri, H. Mejbri
Washambuliaji: E. Achouri, H. Mastouri, E. Saad
Habari za timu

Kocha wa Nigeria, Eric Chelle anatarajiwa kufanya mabadiliko kadhaa ya kikosi chake, katika mchezo huu wa pili wa Nigeria. Mabadiliko hayo yanatarajiwa kuwa ya kimfumo na kikosi. Kocha huyo amekuwa akitumia zaidi mfumo wa Diamond (Almasi), wa 4-4-2. Lakini mara kadhaa amekuwa akibadilika na kutumia 4-3-3, hasa kipindi cha pili walipoichapa Tanzania 2-1 katika mechi yao ya kwanza ya AFCON.
Akizungumzia hilo, Chelle amesema: “Katika mawazo yangu nina chaguzi mbili, kwanza labda tuwaache Tunisia wamiliki mpira na kushambulia kwa kushtukia au kumiliki mchezo. Kama tunavyojua Tunisia ni timu nzuri na labda tutabadilisha kitu. Tulifanya mazoezi yetu baada ya mchezo wa kwanza na katika vikao tulijaribu kuongeza nguvu zaidi. Tuna mchezo dhidi ya timu kubwa”
SOMA HII ZAIDI: AFCON 2025 Mahrez, Jackson, Achouri watikisa: Hawa hapa wafungaji bora wa Raundi ya 1
Taarifa ya majeruhi

Kikosi cha Nigeria kinatarajiwa kuwa kamilifu. Lookman, ambaye alifunga bao moja katika ushindi huo anatarajia kuendelea kuwa na mchezo mzuri. Victor Osimhen atataka kuimarisha umaliziaji wake baada ya kukosa nafasi kadhaa kwenye mchezo wa mwisho. Alex Iwobi alitoa pasi mbili za mabao dhidi ya Tanzania na anasalia kuwa kitovu cha ubunifu katika safu ya kiungo. Nahodha Wilfred Ndidi anatarajiwa kuendelea kuimarisha ulinzi.
Tunisia pia iliripoti hali safi ya afya, ikimwacha kocha mkuu Sami Trabelsi sababu ndogo ya kubadilisha mbinu yake. Hivyo watarajie 4-3-3 tena, huku Hazem Mastouri akiongoza safu hiyo. Tayari miongoni mwa wafungaji bora katika michuano hiyo, Achouri anatarajiwa kuwa tishio tena kutoka maeneo mengi huku akiendelea kutafuta Kiatu cha Dhahabu.
SOMA HII PIA: Uganda vs Tanzania AFCON 2025: Live score, lineups, h2h, prediction, Habari za timu
Hitimishio
Nigeria vs Tunisia AFCON 2025 ni vita nyingine ambayo inatarajiwa kuusimamisha maelfu ya wapenda soka. Ikumbukwe mshindi wa mchezo huu atakuwa amefikisha pointi 6, na hivyo anafuzu moja kwa moja hatua ya 16 bora. Hii pia ni vita ya nani ataongeza rekodi bora dhidi ya mpinzani.

