- Mo Salah kuiongoza Misri AFCON 2025 wakiwa kundi B,mashindano yaanza Desemba 21,2025-Januari 18,2026.
- AFCON 2025 Morocco vs Comoros mchezo wa ufunguzi kwa wenyeji kuanza safari leo Desemba 21,2025
- Timu 24 zinapambania taji kubwa Afrika zikiwa kwenye hatua ya makundi, fainali kupigwa Januari 18, 2026
AFCON 2025 Morocco vs Comoros saa 4:00 usiku mchezo wa ufunguzi. Hii hapa ratiba kamili ya mashindano hayo makubwa Afrika. Fainali inatarajiwa kuchezwa Januari 18 2026, Uwanja wa Prince Moulay Abdellah saa 1:00 usiku. Ikumbukwe kwamba mchezo wa ufunguzi utachezwa hapo pia kwa wenyeji kufungua pazia kusaka bingwa mpya.
SOMA HII: Tanzania vs Nigeria mchezo wa kwanza AFCON 2025 Morocco/ Orodha ya wachezaji, kazi imeanza

AFCON 2025 Morocco vs Comoros utakuwa ni mchezo wa aina gani?

Ipo wazi kuwa AFCON 2025 Morocco vs Comoros huu ni mchezo unaoashiria kuanza kwa mashindano haya makubwa. Kila timu katika kundi lake itacheza mechi tatu kusaka tiketi ya hatua ya robo fainali. Wenyeji Morocco wanapewa nafasi kubwa kufanya vizuri kwenye mashindano haya.
Hivyo mchezo wa leo utakuwa na taswira nzima namna mashindano yatakavyokuwa. Wachezaji walioitwa kwenye timu za taifa watakula sikukuu ya Christmas na mwaka mpya 2026 wakiwa nchini Morocco kwenye majukumu ya kupeperusha bendera za mataifa yao.
Ratiba ya AFCON 2025, Morocco
Jumapili, Desemba 21, 2025
Morocco vs Comoros saa 4:00 usiku
Jumatatu, Desemba 22,2025
Mali vs Zambia, saa 11:00 jioni
Afrika Kusini vs Angola saa 2:00 usiku
Misri vs Zimbabwe, saa 5:00 usiku
Jumanne, Desemba 23, 2025

Congo Dr vs Benin, saa 9:30 alasiri
Senegal vs Botswana, saa 12:00 jioni
Nigeria vs Tanzania, saa 2:30 usiku
Tunisia vs Uganda, saa 5:00 usiku.
SOMA HII: AFCON 2025: Umeona? Timu zatambiana Morocco kwa mavazi makali

Desemba 24,2025, Jumatano
Burkina Faso vs Equatorial Guinea, saa 9:30 alasiri
Algeria vs Sudan, saa 12:00 jioni
Ivory Coast vs Msumbiji, saa 2:30 usiku
Cameroon vs Gabon, saa 5:00 usiku
Ijumaa, Desemba 26,2025
Angola vs Zimbabwe saa 9:30 alasiri
Misri vs Afrika Kusini, saa 12:00 jioni
Zambia vs Comoros, saa 2:30 usiku
Morocco vs Mali, saa 5:00 usiku
Jumamosi, Desemba 27,2025
Benin vs Botswana, saa 9:30 alasiri
Senegal vs Congo Dr, saa 12:00 jioni
Uganda vs Tanzania, saa 2:30 usiku
Nigeria vs Tunisia, saa 5:00 usiku.
Jumapili, Desemba 28, 2025
Gabon vs Msumbiji, saa 9:30 alasiri
Equatorial Guinea vs Sudan, saa 12:00 usiku
Algeria vs Burkina Faso, saa 2:30 usiku
Ivory Coast vs Cameroon, saa 5:00 usiku.
Desemba 29, Jumatatu

Angola vs Misri
Zimbabwe vs Afrika Kusini
Comoros vs Mali
Zambia vs Morocco
Jumanne, Desemba 30,2025
Tanzania vs Tunisia
Uganda vs Nigeria
Benin vs Senegal
Botswana vs DR Congo
Jumatano, Desemba 31, 2025
Equatorial Guinea vs Algeria
Sudan vs Burkina Faso
Gabon vs Ivory Coast
Msumbiji vs Cameroon
SOMA HII: Hawa hapa wachezaji 5 wa kuchungwa AFCON 2025 Morocco

Makundi ya AFCON 2025
Kundi A: Morocco, Mali, Zambia, Comoros
Kundi B: Misri, Afrika Kusini, Angola, Zimbabwe
Kundi C: Nigeria, Tunisia, Uganda, Tanzania
Kundi D: Senegal, DR Congo, Benin, Botswana
Kundi E: Algeria, Burkina Faso, Guinea ya Ikweta, Sudan
Kundi F: Ivory Coast, Cameroon, Gabon, Msumbiji
Hitimisho
AFCON 2025 Morocco vs Comoros ni kete ya ufunguzi ndani ya 2025 na fainali inatarajiwa kuchezwa 2026. Dunia inafuatilia mashindano haya makubwa yenye mvuto na wachezaji wakiwa sokoni. Nani atatwaa ubingwa huu? Endelea kufuatilia SportPesa site tutakupa matokeo na ratiba zinazofuata.

