- Uongozi wa Simba SC rasmi umemtangaza raia wa Afrika Kusini, Steve Barker kuwa kocha wao mkuu mpya.
- Kocha mpya Simba SC Steve Barker anakuwa Mwalimu wa tatu kuiongoza Simba SC msimu huu.
- Kocha huyu anakuja kuchukua mikoba ya Dimitar Pantev aliyefungashiwa virago.
- Je, unajua CV ya kocha Barker? Soma Makala hii ujue kila kitu.
Uongozi wa Simba SC rasmi umemtangaza raia wa Afrika Kusini, Steve Barker kuwa kocha wao mkuu mpya. Kocha huyo anatarajiwa kuanza rasmi majukumu ya kukinoa kikosi hiko, akichukua mikoba ya Dimitar Pantev aliyefungashiwa virago. Makala hii inaangazia wasifu (CV), ya kocha huyo mpya.
SOMA HII PIA: Kocha mpya Simba SC jina mezani/ Kocha Yanga SC CV zake zatua Msimbazi, utambulisho wapangwa
Hujashinda pesa? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa
Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Wasifu binafsi wa kocha mpya Simba SC Steve Barker

Kuzaliwa: 23/12/1967 (57)
Mahali alipozaliwa: Lesotho Maseru
Uraia: South Africa
Mfumo anaopenda kutumia

Kocha huyu anapendelea soka la kushambulia na hutumia zaidi mfumo wa 4:3:3. Kwa kawaida amekuwa na wastani wa miaka 4.2 katika timu ambazo amewahi kufundisha. Barker ni mzoefu wa soka la nchi za Kusini mwa Afrika, ambapo alitumia muda mwingi nchini Afrika Kusini. Kocha huyu amejiunga Simba SC akitokea kikosi cha Stellenbosch aliyoifikisha nusu fainali ya kombe la Shirikisho msimu uliopita.
SOMA HII ZAIDI: Unamfahamu, Dimitar Pantev kocha mpya Simba SC? Hizi hapa rekodi zake, mifumo na mafanikio
Takwimu zake msimu huu
Kwa mujibu wa mtandao maarufu wa kutunza takwimu za michezo wa Transfermarkt, msimu huu Barker ameiongoza Stellenbosch katika michezo 24. Ameshinda mechi 8, sare mechi 6 na kupoteza mechi 10. Katika michezo hiyo amekusanya pointi 30, hii inamfanya awe na wastani wa pointi 1.25 kwa mchezo.
Total: 24 8 6 10 30 1.25
Rekodi ya timu alizowahi kupita

Stellenbosch kuanzia mwaka 2017 ameifundisha michezo zaidi ya 300
Alexandra Black Aces 2016-2017
AmaZulu FC 2014-2016
University of Pretoria FC U. Pretoria 2008-2014.
SOMA HII PIA: Dimitar Pantev kocha mpya Simba SC anapenda kushambulia | Mkataba wake, orodha ya wachezaji wapya
Hitimisho

Uteuzi wa kocha mpya Simba SC Steve Barker umekamilika, swali kubwa sasa ni ikiwa ataweza kufikia matarajio ya Wanasimba. Hii ni baada ya kuwa na mwenendo usioridhisha tangu walipoachana na kocha Fadlu Davis. Barker anakuwa kocha wa tatu kuifundisha Simba SC msimu huu, mara baada ya Fadlu Davis na Dimitar Pantev.

