Jonathan Sowah na Allasane Kante kuikosa Yanga SC vs Simba SCJona
  • Yanga SC wapigwa rugu la adhabu na TPLB kutokana na kosa la shabiki kuingia uwanjani mchezo dhidi ya Coastal Union.
  • Jonathan Sowah na Allasane Kante wa Simba SC wafungiwa mechi 5, utovu wa nidhamu chanzo cha yote.
  • Khalid Aucho kiungo wa Black Stars kwenye orodha ya waliopigwa faini na kufungiwa kisa kumpiga Adam Adam wa TRA United.

Jonathan Sowah na Allasane Kante wa Simba SC wafungiwa mechi 5. Kwa mujibu wa taarifa kutoka Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania, (TPLB) wachezaji hao walifanya makosa yasiyo ya kinadhamu.Ilikuwa ni kwenye mchezo namba 031, Simba SC 0-2 Azam FC.

SOMA HII: Beki Ibrahim Bacca wa Yanga SC amefungiwa mechi 5 na TPLB

Vuna mamilioni sasa hivi ukipaisha Kindege cha SportPesa

Ni sasa hivi unavuna mamilioni ukipaisha Kindege cha SportPesa. Ni rahisi sana hasa ukizingatia Marubani wapo makini. Cheza Aviator upate mgao wako kwa kubonyeza link hapa chini, ushindi unakusubiri.

image

Jonathan Sowah na Allasane Kante wa Simba SC wafungiwa mechi 5 walifanyaje?

Jonathan Sowah na Allasane Kante wa Simba SC wafungiwa mechi 5
Kante Allasane kiungo wa Simba SC. Source: Simba SC.

Nyota Jonathan Sowah na Allasane Kante wa Simba SC wafungiwa mechi 5 kwa makosa tofautitofauti kwenye mchezo mmoja. Kwa mujibu wa taarifa kutoka Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania, (TPLB) Sowah alimpiga kiwiko mchezaji Himid Mao wakati wa mchezo huo.

Mbali na kufungiwa mechi 5 nyota huyo ametozwa faini ya milioni moja kutokana na kosa hilo adhabu ikitolewa Desemba 16,2025. Taarifa hiyo imeeleza kiungo wa Simba SC, Allasane Kante naye amefungiwa mechi 5 kutokana na kucheza mchezo usio wa kiungwana kwenye mchezo dhidi ya Azam FC.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania, (TPLB) Kante alimpiga teke kwa makusudi mchezaji Feisal Salum wakati wa mchezo huo. Mbali na kufungiwa mechi 5 nyota huyo ametozwa faini ya milioni moja kutokana na kosa hilo.

Taarifa imeeleza kuwa mwamuzi wa kati Abdallah Mwinyimkuu kutoka Singida ameondolewa kwenye orodha ya waamuzi. Mwinyimkuu atakosekana kwenye mechi tano kwa kushindwa kutafsri sheria za mpira wa miguu. Mwamuzi huyo alishindwa kuchukua hatua kwa vitendo vya ukiukwaji  wa sheria kwenye mchezo huo.

SOMA HII: Simba SC yawatoa mashaka mashabiki yabainisha Kariakoo Dabi itachezwa Juni 15 2025

image

Singida Black Stars 1-3 TRA United, Aucho afungiwa

Aucho BS
Aucho Khalid kiungo wa Singida Black Stars. Source: SBS.

Mchezaji Khalid Aucho wa Singida Black Stars ya Singida amefungiwa michezo mitano na fainali ya milioni moja. Sababu ya adhabu hiyo ni kosa la kumchezea mchezo usio wa kiungwana mchezaji wa TRA United Adam Adam kwa kumpiga na kumsukuma.

Wakati Aucho akifungiwa mechi 5, mwamuzi wa kati wa mchezo huo Alex Pancras kutoka Dar amepewa onyo kali kwa kushindwa kutafsri tukio hilo.

Yanga SC yapigwa rungu la faini milioni 5

Dubee
Dube mshambuliaji wa Yanga SC. Source: Yanga SC.

Mchezo namba 046 kati ya Coastal Union 0-1 Yanga SC mabingwa watetezi wamepigwa rugu la fainali. Ni kiasi cha milioni 5 kwa kosa la shabiki wat imu hiyo kuruka uzio na kuingia uwanjani. Shabiki huyo alionekana kufika hadi kwenye goli la Coastal Union na kuinama kama ishara ya kutafuta, kuchukua ama kuweka kitu.

Katika mchezo huo goli la ushindi lilifungwa na Prince Dube. Ilikuwa Dodoma katika Uwanja wa Jamhuri. Pointi tatu zilibebwa na wageni kwenye mchezo.

Championship hakujapoa adhabu zimetembea

Mechi namba 061: African Sports 0-2 Transit Camp

Klabu ya Transit Camp ya Dar imetozwa fainali ya milioni moja kwa kosa la kuwakilishwa na maofisa wanne badala ya watano kwenye kikao cha maandalizi ya mchezo, (MCM). Hiyo ilikuwa ni kuelekea mchezo wao dhidi ya African Sports.

SOMA HII: Yanga SC wametoa matakwa manne yakitimizwa Kariakoo Dabi kuchezwa, Juni 15 2025 yakataliwa

image

First League

Mechi namba 7A: Alliance FC vs Biashara United

Klabu ya Alliance ya Mwanza imepewa ushindi wa mabao matatu na pointi tatu katika mchezo huo. Biashara United imepoteza mchezo huo kwa mujibu wa kanuni ya 17:31 ya First League kuhusu taratibu za mchezo.

Hitimisho

Jonathan Sowah na Allasane Kante wa Simba SC wafungiwa mechi 5 ni pigo kwa mnyama kutokana na mechi za ushindani zinazofuata. TPLB imesisitiza kuwa ni muhimu kwa timu kuwakumbusha wachezaji umuhimu wa mchezo wa kiungwana. Matendo hayo yamekuwa hayaleti picha nzuri kwenye ligi ya Tanzania.

Share this: