- Muda mchache, mambo ni mengi ndivyo unavyoweza kusema kuihusu Ligi Kuu England EPL mwezi huu wa Desemba.
- Ratiba ina mechi nyingi na za mfululizo. Alhamisi hii vita itaendelea kwa mchezo mkali wa Manchester United vs West Ham.
- Mbungi hii itapigwa Uwanja wa Old Trafford, huku United wakiingia na jeuri ya kurejea kwa staa wao raia wa Brazil, Matheus Cunha.
Muda hautoshi kwenye Ligi Kuu England EPL mwezi huu wa Desemba. Mechi ni nyingi na zinachezwa kwa mfululizo. Alhamisi hii vita itaendelea kwa mchezo mkali wa Manchester United vs West Ham. Katika mchezo huu utakaopigwa kwenye Uwanja wa Old Trafford, United wataingia na jeuri ya kurejea kwa staa wao raia wa Brazil, Matheus Cunha.
SOMA HII PIA: Tottenham vs Manchester United EPL 08/11/2025: Vita ya ‘Top Four’, Live Score, h2h, vikosi, Utabiri
Cheza sasa ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa
Hujashinda na SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

H2H, Manchester United vs West Ham

Katika historia ya mechi za ushindani, timu hizi mbili zimekutana katika michezo 58. Man United wameshinda mechi 34, West Ham wameshinda mechi 14, huku mechi 10 zikiisha kwa matokeo ya sare. Mchezo huu unakwenda kutoa taswira mpya katika rekodi za timu zote mbili na vita ya ubingwa.
Matokeo ya mechi 5 zilizopita za Man United
30 Nov Crystal Palace 1-2 Manchester United
24 Nov Manchester United 0-1 Everton
8 Nov Tottenham 2-2 Manchester United
1 Nov Nottingham Forest 2-2 Manchester United
25 Oct Manchester United 4-2 Brighton
Matokeo ya mechi 5 zilizopita za West Ham
30 Nov West Ham 0-2 Liverpool
22 Nov Bournemouth 2-2 West Ham
8 Nov West Ham 3-2 Burnley
2 Nov West Ham 3-1 Newcastle United
24 Oct Leeds 2-1 West Ham
SOMA HII ZAIDI: Premier League Table & Standings 2025-2026 Season
Kikosi tarajiwa cha Manchester United vs West Ham

Kipa: Lammens
Walinzi: Mazraoui, De Ligt, Shaw
Viungo: Diallo, Casemiro, Fernandes, Dalot; Mbeumo,
Washambuliaji: Mount; Zirkzee
Kikosi tarajiwa cha West Ham vs Man United

Kipa: Areola
Walinzi: Wan-Bissaka, Todibo, Kilman, Diouf
Viungo: Potts, Soucek, Bowen, Fernandes
Washambuliaji: Guilherme, Wilson
Cunha arejea, wengine wawili United hatarini kuukosa mchezo
Mshambuliaji wa Manchester United, Mbrazil Matheus Cunha yuko tayari kucheza mechi hiyo amethibitisha kocha, Ruben Amorim. Kocha huyo ameweka wazi pia kuna wachezaji wawili, ambao huenda wakakosa mchezo huo kutokana na majeraha. Ingawa alikataa kuwataja, lakini inafahamika kuwa, beki Harry Maguire na mshambuliaji Benjamin Sesko wanauguza majeraha.
“Kuna wachezaji wawili walio hatarini kuukosa mchezo huu, lakini sitawataja leo. Ni wazi hii itabadilisha njia tutakavyoukaribia mchezo, tutaona kama wanaweza kucheza. Wengine wako vizuri na Matheus amerudi. Harry na Sesko bado wanauguza majeraha,” amesema Amorim.
Kurudi kwa Cunha ambaye alikosa mechi mbili kutokana na jeraha la kichwa, kunakiongezea nguvu kikosi cha United. Cunha mwenye umri wa miaka 26, ameonekana kufurahi sana kurejea. Nyota huyo amechapisha picha yake kwenye mitandao ya kijamii akiwa mazoezini.
Ishu ya Mbeumo, Amad, Mazraoui kuna taarifa njema kutoka FIFA

Amorim amepokea habari njema kutokana na tangazo la FIFA kwamba, kipindi cha kuachia wachezaji kuelekea Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), kimepunguzwa. Hii ina maana kuwa, kipindi hiko kimepunguzwa kutoka siku 14 kabla ya mechi ya kwanza ya timu hadi siku saba. Hii ina maana mastaa Amad Diallo (Ivory Coast) na Bryan Mbeumo (Cameroon), ambao nchi zao zinacheza Desemba 24, watakuwa huru kucheza mechi ya United ya nyumbani dhidi ya Bournemouth tarehe 15 Desemba.
SOMA HII PIA: Liverpool vs Manchester United: Live Scores, Utabiri, vikosi, h2h, Takwimu na taarifa mpya za vikosi
Hitimisho
Manchester United vs West Ham ni zaidi ya mchezo, hii inatarajiwa kuwa vita ya kuisaka nne bora ‘Top Four’. United wanatamani kupata matokeo ya ushindi, hasa kwa kuwa watacheza nyumbani mbele ya mashabiki wao. Ikumbukwe mechi ya mwisho wakicheza nyumbani walipoteza mbele ya Everton kwa bao 1-0. Ni wazi West Ham pia hawataruhusu kuporwa pointi kirahisi.

