- Stade Mallien 2-1 Simba SC ni matokeo ya mchezo wa mwisho kukaa kwenye benchi la ufundi.
- Dimitar Pantev wa Simba SC kibarua kimeota nyasi muda mfupi baada ya kupoteza mchezo wa pili.
- Seleman Matola kubeba mikoba kwa mechi zijazo wakati timu ikimtafuta kocha mpya.
RASMI Dimitar Pantev kibarua kimeota nyasi Simba SC mara baada ya makubaliano ya pande zote mbili. Meneja huyo alichukua mikoba ya Fadlu Davids ambaye kwa sasa anakinoa kikosi cha Raja Casablanca ya Morocco. Kuwa na matokeo mabovu katika CAF Champions League kunatajwa kuwa sababu kusitishiwa mkataba wake.
SOMA HII: Dimitar Pantev kocha mpya Simba SC anapenda kushambulia | Mkataba wake, orodha ya wachezaji wapya
Vuna mamilioni sasa hivi
Kuna jambo umekwama kwa sasa kuhusu mkwanja? Usiogope, rubani ni jasiri na kazi yake ni kupaisha kindege cha SportPesa. Cheza sasa hivi Aviator uvune mamilioni bofya hapa chini, muda ni wako na nafasi ya ushindi inakusubiri

Dimitar Pantev kibarua kimeota nyasi Simba SC matokeo ya mwisho yalikuaje?

Meneja Dimitar Pantev kibarua kimeota nyasi Simba SC huku mwendo wa timu hiyo ukiwa bado haujawa bora. Kwenye mechi mbili za hatua ya makundi timu hiyo ilipoteza pointi tatu. Ilianza mchezo wa nyumbani na ule wa ugenini. Kutokana na kuanguka mara mbili kwenye mechi muhimu inatajwa kuwa sababu kuvunja mkataba.
SOMA HII: Nsingizini Hotspurs vs Simba SC CAF Champions League| Mtihani wa kwanza wa Meneja Mkuu Pantev

Matokeo ya mechi mbili za CAF Champions League hatua ya makundi
Simba SC 0-1 Petro de Luanda
Stade Mallien 2-1 Simba SC
Kwenye mechi mbili za hatua ya makundi Simba SC ilipoteza zote. Safu ya ushambuliaji ilifunga goli moja huku ukuta ukiruhusu kufungwa magoli matatu.
Kwa sasa timu hiyo itakuwa chini ya Seleman Matola wakati mchakato wa kutafuta kocha ukiendelea. Timu hiyo msimu wa 2025/26 katika mechi za kimataifa haijawa kwenye mwendo mzuri. Katika mechi za nyumbani zote haijapata ushindi.
Simba SC 1-1 Gaborone United
Simba SC 0-0 Nsingizini Hotspurs
Simba SC 0-1 Petro de Luanda
SOMA HII: Matokeo ya CAF Champions League 2025/26/ Simba SC yafungwa mechi mbili mfululizo

Mbinu zatajwa kumfelisha
Pantev alikuwa ni muumini wa kumaliza mchezo kipindi cha kwanza. Katika mechi zote ambazo alipata ushindi walifunga kipindi cha pili.Iwe ni kwenye mechi za ligi na Ligi ya Mabingwa Afrika.
Nsingizini Hotspurs 0-3 Simba SC, mabao yote ya Simba SC yalifungwa kipindi cha pili.
JKT Tanzania 1-2 Simba SC, mabao yote ya Simba SC yalifungwa kipindi cha pili.
Kwenye mchezo dhidi ya Petro de Luanda alianza na viungo watupu huku washambuliaji asilia wakiwa benchi. Kipindi cha pili aliwapa nafasi kucheza Jonathan Sowah, Steven Mukwala lakini tayari walikuwa wamepoteza.
Katika mchezo wa pili dhidi ya Stade Malien, Pantev alianza na mshambuliaji mmoja ambaye ni Seleman Mwalimu. Kwenye mchezo huo bao la Simba SC lilifungwa na kiungo Neo Maema. Zama za Pantev chaguo la kwanza alikuwa kiungo Joshua Mutale.
Taarifa rasmi kutoka Simba SC

Taarifa kutoka Simba SC imeeleza namna hii:”Uongozi wa Klabu ya Simba SC umefikia makubaliano ya pande mbili ya kusitisha mkataba wa Meneja Mkuu Dimitar Pantev pamoja na wasaidizi wake wawili.
“Kwa sasa kikosi kitabaki chini ya kocha Seleman Matola wakati mchakato wa kutafuta kocha mwingine unaendelea”,.
Ratiba ya mechi zijazo Simba SC

Chini ya Matola kuna mechi mbili ambazo zinatarajiwa kuchezwa hivi karibuni. Simba SC vs Mbeya City, Desemba 4,2025.
Simba SC vs Azam FC, Desemba 7,2025.
Hitimisho
Dimitar Pantev kibarua kimeota nyasi Simba SC ikiwa ni muda mchache baada ya timu hiyo kurejea kutoka Mali. Katika mechi mbili hatua ya makundi CAF Champions League mnyama hajaambulia ushindi. Ni mechi nne zimebaki kujiuliza kutafuta tiketi ya kutinga hatua ya robo fainali.

