Barcelona vs Atletico MadridBarcelona vs Atletico Madrid
  • Barcelona vs Atletico Madrid sio tu, ni mchezo wa Ligi Kuu ya Uhispania, bali ni vita halisi ya kusaka ubingwa.
  • Mbungi hii itapigwa Jumanne hii katika dimba la Camp Nou.
  • Je, Barcelona watarudia makosa ya kuruhusu kupoteza kwa mara ya pili mbele ya Atletico msimu huu?

Vita ya ubingwa wa Ligi Kuu Hispania itaendelea Jumanne hii katika mechi ya vigogo. Barcelona vs Atletico Madrid watakuwa wakitifuana Wakisaka kuimarisha matumaini yao ya kutwaa taji. Mchezo huo wa ligi unatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Camp Nou. Wenyeji Barcelona wanaongoza msimamo wa ligi, huku kikosi cha Diego Simeone kikiwa nyuma kwa pointi tatu katika nafasi ya nne.

SOMA HII PIA: La Liga Table 2025/26

Cheza sasa ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa

Bado hujashinda na SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

image

H2H, Barcelona vs Atletico Madrid

Mechi zilizopita
Mechi zilizopita

Timu hizi mbili zimekutana katika michezo 64 katika historia ya mechi za ushindani. Barcelona wamefanikiwa kushinda mechi 34, Atletico Madrid wameshinda mechi 14, huku mechi 16 zikiisha kwa matokeo ya sare. Mchezo huu unakwenda kutoa taswira mpya katika rekodi za timu zote mbili na vita ya ubingwa.

SOMA HII ZAIDI: Barcelona FC- Latest news, fixtures, results, table standings, squad players, transfer news and statistics

Matokeo ya mechi 5 zilizopita za Barcelona

The final push of the year- ❄️⚽️
Ratiba ya Barcelona

Barcelona 3-1 Alaves

Chelsea 3-0 Barcelona

Barcelona 4-0 Athletic Bilbao

Celta Vigo 2-4 Barcelona

Club Bruges 3-3 Barcelona

Matokeo ya mechi 5 zilizopita za Atletico Madrid

Atletico Madrid 2-0 Real Oviedo

Atletico Madrid 2-1 Inter

Getafe 0-1 Atletico Madrid

Atletico Madrid 3-1 Levante

Atletico Madrid 3-1 Union St.-Gilloise

SOMA HII PIA: Top 5 Dominating Soccer Teams in 2023-2024: Who Will Reign Supreme?

Kikosi tarajiwa cha Barcelona vs Atletico Madrid

Kikosi cha Barcelona
Kikosi cha Barcelona

Kipa: Garcia

Walinzi: Kounde, Garcia, Cubarsi, Balde

Viungo: De Jong, Pedri; Yamal, Olmo, Raphinha

Mshambuliaji: Lewandowski

Kikosi tarajiwa cha Atletico Madrid vs Barcelona

Kipa: Oblak

Walinzi: Molina, Gimenez, Hancko, Ruggeri

Viungo: Cardoso; Simeone, Barrios, Koke, Baena

Mshambuliaji: Alvarez

Taarifa za majeruhi wa timu kuelekea mchezo

Barcelona bado inawakosa kipa Marc-Andre ter Stegen na kiungo Gavi, huku Fermin Lopez akikosa mechi ya pili kutokana na jeraha la kifundo cha mguu. Ronald Araujo alikosa mechi dhidi ya Alaves kutokana na maradhi, na huenda asiwe tayari kwa mchezo wa katikati ya wiki dhidi ya Atletico. Eric Garcia anatarajiwa kuwa fit licha ya kutolewa mapema Jumamosi.

Frenkie de Jong anatarajiwa kurejea baada ya kukosa mechi dhidi ya Alaves, kwa sababu za kifamilia. Nyota huyo wa Uholanzi anatarajiwa kurejea kwenye kikosi, sambamba na Jules Kounde na Pedri.

Kwa upande wa Atletico, Marcos Llorente hatasafiri kutokana na jeraha la paja. Beki Robin Le Normand pia anatarajiwa kukosa mechi muhimu ya ligi kutokana na jeraha la goti, alilopata katika Ligi ya Mabingwa mapema Novemba. Baada ya kufanya mabadiliko mwishoni mwa wiki, Simeone anaweza kuwarejesha Jose Maria Gimenez, Matteo Ruggeri, Pablo Barrios, Johnny Cardoso na Giuliano Simeone.

Koke pia anatarajiwa kurejea katika safu ya kiungo, huku Julian Alvarez akipewa nafasi mbele ya Sorloth licha ya Mnorwey huyo kufunga mabao mawili Jumamosi iliyopita.

Taarifa za timu na rekodi

Alvalez
Alvalez

Barcelona huenda wanapata ugumu kurudia kiwango chao cha juu walichoonyesha msimu uliopita, lakini bado wamefanya makubwa hadi kurejea kileleni baada ya mechi 14 za La Liga. Vijana hao wa Hansi Flick wameshinda mechi 11 za ligi msimu huu, wamesare mchezo mmoja na kupoteza mara mbili. Hii ni pamoja na ushindi katika mechi zao nne za mwisho za ligi, tangu walipopoteza dhidi ya Real Madrid katika El Clasico mwishoni mwa Oktoba.

Katika michezo hiyo waliwafunga Elche, Celta Vigo na Athletic Bilbao, kisha wakarejea kwenye ushindi wa 3-1 Jumamosi dhidi ya Deportivo Alaves. Ushindi huu ulikuja baada ya kupoteza kwa Chelsea kwenye Ligi ya Mabingwa.

Wakiwa wamefunga mabao 39 msimu huu mabao mengi zaidi katika ligi, Barcelona watajihisi wana ubora wa kushinda safu ya ulinzi ya Atletico ambayo ina rekodi bora ya ulinzi msimu huu. Atletico walionekana kuwa nje ya mbio za ubingwa walipoanza msimu kwa kusuasua na kushinda mechi tatu, sare nne na kupoteza moja kati ya mechi zao nane za kwanza.

Hata hivyo, tangu wakati huo wameshinda mechi zao sita za mwisho za ligi, wakionesha dhamira ya kuwa washindani halisi katika mapambano ya taji.

Simeone sasa analenga ushindi wake wa 324 wa La Liga kama kocha wa Atletico katika mtihani mgumu wa Jumanne, dhidi ya Barcelona. Mechi hii ilisogezwa mbele kutoka Januari kutokana na Super Cup ya Uhispania. Katika mchezo huu Atletico wanatafuta ushindi wa pili mfululizo wa ugenini, dhidi ya Barcelona.

Hitimisho

Barcelona vs Atletico Madrid sio tu, ni mchezo wa Ligi Kuu ya Uhispania, bali ni vita halisi ya kusaka ubingwa. Ushindi kwa Atletico utamaanisha kufungana pointi na Barcelona, hivyo kuchagiza zaidi vita ya ubingwa. Je, Barcelona watarudia makosa ya kuruhusu kupoteza kwa mara ya pili mbele ya Atletico msimu huu?

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.