JS Kabylie vs Yanga SCBacca safari (-)
  • Yanga SC msafara wa wachezaji 24 umesafiri kuelekea Algeria kwa maandalizi ya mwisho mchezo wa hatua ya makundi.
  • JS Kabylie vs Yanga SC CAF Champions League utachezwa Novemba 28/2025 Uwanja wa Hocine Ait Ahmed.
  • Yanga SC 1-0 AS Far Rabat ni matokeo ya mchezo wa kwanza huku JS Kabylie wakipoteza kwa kufunwa goli 4-1 dhidi ya Al Ahly.

JS Kabylie vs Yanga SC ni ratiba ijayo CAF Champions League hatua ya makundi Novemba 28,2025. Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa saa 1:00 usiku. Wananchi watakuwa ugenini raundi ya pili, Uwanja wa Hocine Ait Ahmed. Wenyeji JS Kabylie wametoka kupata kipigo cha goli 4-1 dhidi ya Al Ahly wanakutana na wageni waliotoka kushinda goli 1-0 dhidi ya AS Far Rabat.

SOMA HII: Ratiba ya mechi za CAF Champions League 2025/26/ Matokeo na magoli

Unasubiri nini? Muda wa kuvuna mamilioni sasa hivi

Kuna jambo umekwama kwa sasa kuhusu mkwanja? Usiogope, rubani ni jasiri na kazi yake ni kupaisha kindege cha SportPesa. Cheza sasa hivi Aviator uvune mamilioni bofya hapa chini, muda ni wako na nafasi ya ushindi inakusubiri wewe.

image

Kundi B JS Kabylie vs Yanga SC CAF Champions League Novemba 28

JS Kabylie vs Yanga SC
Pacome kiungo wa Yanga SC. Source: Yanga SC.

Mechi ya raundi ya pili kundi B inayofuata ni JS Kabylie vs Yanga SC. Msafara wa Yanga SC wenye jumla ya wachezaji 24 umesafiri kuelekea Algeria. Kutoka Tanzania safari ilianza Novemba 24,2025 kwa kupitia Dubai.

Rekodi zinaonyesha kwenye mechi 8 ambazo JS Kabylie alicheza nyumbani alipata ushindi mechi 7.
Yanga SC katika mechi 3 zilizopita ugenini ushindi mechi moja, sare moja na alipoteza mchezo mmoja.

Msimamo wa kundi B

1. Al Ahly mechi 1 pointi 3
2.Yanga SC mechi 1 pointi 3
3. AS Far Rabat mechi 1 pointi 0
4. JS Kabylie mechi 1 pointi 0

Matokeo ya mechi 7 zilizopita kwa JS Kabylie

JS
Nyota wa JS Kabylie kwenye mchezo wa ushindani. Source: JS Kabylie.

22/11/2025 Al Ahly 4-1 JS Kabylie, CAF Champions League
09/11/2025 CS Constantine 1-0 JS Kabylie, Ligue 1
03/11/2025 JS Kabylie 4-1 Mc El Bayadh, Ligue 1
29/10/2025 JS Saoura 2-2 JS Kabylie, Ligue 1
25/10/2025 JS Kabylie 2-1 US Monastir, CAF Champions League.
21/10/2025 JS Kabylie 1-0 USM Khenchela.
17/10/2025 US Monastri 0-3 JS Kabylie CAF Champions League

Mechi 7 ushindi katika mechi 4
Poteza mechi 2
Sare mechi 1
Mabao ya kufunga 13
Mabao yakufungwa 9

Mechi za Yanga SC 7 zilizopita

Septemba 24,2025 – Yanga SC 3-0 Pamba Jiji.(Ligi ya NBC)

Septemba 30,2025-Mbeya City 0-0 Yanga SC (Ligi ya NBC).

Silver Strikers FC 1-0 Yanga SC CAF Champions League, Oktoba 18, 2025 Uwanja wa Bingu, Malawi.

Yanga SC 2-0 Silver Strikers FC, Uwanja wa Benjamin Mkapa, Oktoba 25, 2025

Yanga SC 2-0 Mtibwa Sugar, Oktoba 28 2025, Uwanja wa KMC, Complex.

Yanga SC 4-1 KMC FC, Novemba 9,2025, Uwanja wa KMC Complex.

Novemba 22,2025, Yanga SC 1-0 AS Far Rabat, New Amaan Complex, Ligi ya Mabingwa Afrika.

Katika mechi 7 magoli 12 safu ya ushambuliaji ilifunga. Ukuta uliruhusu kufungwa magoli mawili. Ushindi kwenye mechi 5, ilipoteza mchezo mmoja na sare moja.

SOMA HII: CAF Champions League matokeo mechi zote hatua ya makundi 2025/26

image

Kikosi cha JS Kabylie kinachotarajiwa kuanza


Mlinda mlango
Hadid

Mabeki
Benchana
Belaid
F. Nechat

Viungo
Merghem
Babacar Sarri
J. BARA
Boudjemaa

Washambuliaji
Mouali
Messaoudi
L. Akhrib
Kocha Mkuu wa JS Kabylie anaitwa Joe Zinbauer

Kikosi cha Yanga SC kinachotarajiwa kuanza vs JS Kabylie

Zimbwe Jr -
Zimbwe Jr beki wa Yanga SC. Source: Yanga SC.


Langoni
Djigui Diarra

Mabeki
Zimbwe Jr
Dickson Job
Ibrahim Hamad
Israel Mwenda

Viungo
Pacome Zouzoua
Duke Abuya
Mudathir Yahya
Maxi Nzengeli

Washambuliaji
Prince Dube
Edmund John
Kocha Mkuu wa Yanga SC, Pedro Goncalves

SOMA HII: Ratiba ya Yanga SC 2025/26 NBC Premier League, CAF Champions League/ Live scores

image

Orodha ya wachezaji wa Yanga SC walioelekea Algeria

Makipa

Djigui Diarra, Aboutwalib Mshery na Khomeiny

Mabeki

Bakari Mwamnyeto, Dickson Job, Ibrahim Bacca, Assinki, Zimbwe Jr, Israel Mwenda na Boka.

Viungo

Mudathir Yahya, Duke Abuya, Maxi Nzengeli, Shekhan, Conte, Aziz Andambilwe, Kouma, Edmund John, Chikola, Ecua, Doumbia, Pacome.

Washambuliaji
Boyel na Dube.

Hitimisho

JS Kabylie vs Yanga SC mchezo wa kutafuta tiketi kutinga robo fainali. Mwenyeji ana hasira zakupoteza mchezo uliopita huku mgeni akitoka kushinda. Wababe hawa watakutana raundi ya pili hatua ya makundi.

Share this: