CAF Champions League matokeo mechi zote hatua ya makundiAl Ahly CAF
  • Simba SC 0-1 Petro de Luanda, Dimitar Pantev ameanza kwa kipigo hatua ya makundi
  • CAF Champions League matokeo mechi zote hatua ya makundi 2025/26 yapo hadharani.
  • Al Ahly SC 4-1 JS Kabylie mchezo uliokusanya magoli mengi zaidi katika mechi za mwanzo.

CAF Champions League matokeo mechi zote hatua ya makundi 2025/26 yameshajulikana mara baada ya timu kushuka uwanjani. Al Ahly SC 4-1 JS Kabylie ni mchezo uliokusanya mabao mengi ambayo ni matano. Esperance ST 0-0 Stade ukiwa ni mchezo pekee ambao umekamilika bila goli ndani ya dakika 90.

SOMA HII: Yanga SC 1-0 AS FAR Rabat CAF Champions League/ Prince Dube afunga goli la ushindi New Amaan Complex

Cheza sasa ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa

Bado hujashinda na SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

image

CAF Champions League matokeo mechi zote hatua ya makundi 2025/26 ni moto

CAF Champions League matokeo mechi zote hatua ya makundi 2025/26
Pacome kiungo wa Yanga SC vs AS FAR Rabat. Source: Yanga SC.

Kila mmoja anapambania pointi tatu kwenye CAF Champions League matokeo mechi zote hatua ya makundi 2025/26 baada ya timu zote kucheza mchezo mmoja. Bado safari inaendelea ikiwa ni vita ya kusaka tiketi ya kutinga hatua ya makundi. Mchezo wa ufunguzi mwenyeji alishinda na ule wa funga kazi hatua ya makundi mwenyeji alipoteza.

Al Hilal Omdurman 2-1 MC Alger

MC Alger ya Mokwena yaanza kwa kipigo 2-1 Al Hilal Omdurman CAF Champions League
Al Hilal Omdurman vs MC Alger. Source: Al Hilal Omdurman

Huu ulikuwa ni mchezo wa ufunguzi katika hatua ya makundi. Uwanja wa Amahoro, Kigali ulikuwa kazini. Mwenyeji alipata matokeo na kupata pointi tatu. Magoli yamefungwa na Mohamed Raman dakika ya 75 na Abdelrazing Omer dakika ya 45. MC Alger walipata goli kupitia kwa Mustafa Karshoum alijifunga dakika ya 53. Hiyo ilikuwa Novemba 21,2025.

SOMA HII: MC Alger ya Mokwena yaanza kwa kipigo 2-1 Al Hilal Omdurman CAF Champions League

image

Yanga SC 1-0 AS FAR Rabat

Kutoka Tanzania mchezo wa kwanza ulichezwa Novemba 22,2025. Uwanja wa New Amaan Complex pointi tatu zilibaki Zanzibar. Goli la Yanga SC limefungwa na Prince Dube dakika ya 58. Pasi ya Mudathir Yahya ilibakiza pointi tatu zote nyumbani.

Mamelodi Sundowns 3-1 St Eloi Lupopo

Mwendelezo wa mechi za CAF Champions League ilikuwa Novemba 22,2025. Magoli ya Mamelodi Sundowns yamefungwa na Nuno Santos dakika ya 4 na 77, Marcelo Allende dakika ya 61. St Eloi Lupopo goli lao limefungwa na Ramos Kashala Wanet dakika ya 44.

SOMA HII: Simba SC 1-0 Gaborone United CAF Champion League | Goli la Ellie Mpanzu, kadi nyekundu

image

Al Ahly SC 4-1 JS Kabylie

Mchezo uliokusanya magoli mengi katika hatua ya makundi. Magoli kwenye mchezo huo yale ya Al Ahly yamefungwa na Mahmoud Trezeguet dakika ya 36 na 84, Mohamed Sherif dakika ya 39 na Mohamed Hadid dakika ya 90+3. Lile la JS Kabylie ni Mohamed El Shenawy dakika ya 90 alijifunga.

Esperance ST 0-0 Stade

Haijalishi upo nyumbani ama ugenini matokeo yanatafutwa. Ni mchezo ambao umeshuhudia wababe wawili wakigawana pointi mojamoja.Ilichezwa Novemba 22,2025.

RSB Berkane 3-0 Power Dynamo

Pointi tatu zilibaki Morocco. Magoli ya RSB Berkane yamefungwa na Paul Bassene dakika ya 65, Mounir Chouiar dakika ya 16 na lile la ufunguzi ni Aaron Katebe dakika ya 13. lichezwa Novemba 22,2025.

Pyramids 3-0 Rivers United

Mabingwa watetezi wana jambo lao pia msimu wa 2025/26. Magoli yalifungwa na Ahmed Atef Otta dakika ya 72, 57 na dakika ya 52. Pointi tatu zimebaki nyumbani.

Simba SC 0-1 Petro de Luanda

Dimitar Pantev
Dimitar Pantev, Meneja Mkuu wa Simba SC. Source: Simba SC.

Funga kazi ilikuwa Uwanja wa Benjamini Mkapa Simba SC 0-1 Petro de Luanda. Hapa wenyeji wamepoteza pointi tatu mbele ya mashabiki wao waliojitokeza. Ni Novemba 23,2025 goli likifungwa na Benny dakika ya 78 pasi ya Tiago Reis.

Hitimisho

CAF Champions League matokeo mechi zote hatua ya makundi yapo wazi kwa sasa. Kundi D limechangamka huku mnyama Simba SC chini ya Meneja Mkuu Dimitar Pantev akianza kwa joto la jiwe. Bado mechi tano kwa kila timu kukamilisha safari ya kusaka tiketi kutinga hatua ya robo fainali.

Share this: