Simba SC vs Petro de Luanda CAF Champions League funga kaziYakoub- Rushine
  • CAF Champions League Jumapili Novemba 23,2025 saa 10:00 jioni mchezo wa kwanza hatua ya makundi kwa kundi D utachezwa Uwanja wa Mkapa.
  • Simba SC vs Petro de Luanda nani atachukua pointi tatu CAF Champions League? Jibu linasubiriwa kujibiwa na wachezaji.
  • Petro de Luanda wagumu kufungika wanakutana na mnyama mwenye kiu yakupata ushindi kwa mara ya kwanza kimataifa nyumbani.

Simba SC vs Petro de Luanda nani atachukua pointi tatu CAF Champions League? Huu ni mchezo wa kwanza hatua ya makundi. Mnyama atakuwa Uwanja wa Mkapa mbele ya mashabiki wake huku vijana wa Angola wakiwa ugenini. Huo utakuwa mchezo wa kwanza kati ya sita katika kundi D unaotarajiwa kuchezwa Jumapili, Novemba 23,2025 saa 10:00 jioni.

SOMA HII: Simba SC vs Petro de Luanda CAF Champions League 2025/26/ Live score, H2H

Shinda na ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa hivi

Ni zamu yako kushinda na SportPesa, unaweza kushinda mamilioni sasa hivi. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kupitia Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa bonyeza picha hii chini.

image

Simba SC vs Petro de Luanda nani atachukua pointi tatu CAF Champions League?

Simba SC vs Petro de Luanda nani atachukua pointi tatu CAF Champions League?
Mashabiki Simba SC watakuwa Uwanja wa Mkapa, Novemba 23,2025. Source: Simba SC.

Kuna swali kuhusu Simba SC vs Petro de Luanda nani atachukua pointi tatu CAF Champions League?Mashabiki watapata jibu hilo wakishuhudia live Uwanja wa Mkapa na wengine watakuwa nyumbani wakiutazama kupitia Azam TV. Huu ni mchezo wa hatua ya makundi unaosubiriwa kwa shauku kubwa. Wababe hawa wote wawili wanasaka tiketi kutinga hatua ya robo fainali.

Matokeo ya mechi 5 za Simba SC

Morice Abraham kiungo mshambuliaji Simba SC
Moricee Abraham kiungo mshambuliaji wa Simba SC. Source: Simba SC.

Novemba 8,2025, JKT Tanzania 1-2 Simba SC, NBC Premier League.

Oktoba 26,2025, Simba SC 0-0 Nsingizini Hotspurs, CAF Champions League.

Oktoba 19,2025, Nsingizini Hotspurs 0-3 Simba SC, CAF Champions League

Oktoba Mosi 2025, Simba SC 3-0 Namungo FC, mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Septemba 28 2025, Simba SC 1-1 Gaborone United, Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kwenye mechi 5 za hivi karibuni, ushindi kwa Simba SC ni mechi 3. Ilipata sare katika mechi 2. Haijapoteza mchezo hivi karibuni kwenye mechi za ushindani.

Katika eneo la safu ya ushambuliaji imefunga jumla ya magoli 9. Safu ya ulinzi imeruhusu kufungwa magoli 2. Hivyo ina wastani wakufunga goli moja kila baada ya dakika 50.

SOMA HII: Mechi za Simba SC 2025/26 CAF Champions League, NBC Premier League ni moto| Matokeo na wafungaji

image

Nyumbani kimataifa Simba SC hawajapata ushindi

Jean Ahoua (-)
Jean Ahoua kiungo wa Simba SC aliyefunga goli kimataifa Uwanja wa Mkapa 2025/26. Source: Simba SC.

Licha ya kwamba watakuwa nyumbani kuna rekodi mbaya kwa mnyama. Msimu wa 2025/26 mechi zote za kimataifa hawajapata ushindi. Matokeo yote CAF Champions League ilikuwa ni sare.

Matokeo ya mechi 5 kwa Petro de Luanda

25/10/2025, Petro de Luanda 2-0 Stade d’Abdjan Caf Champions League.
29/10/2025 Sao Salvador 2-1 Petro de Luanda, mchezo wa ligi ya Angola.
01/11/2025, Petro de Luanda 4-1 Libolo, mchezo wa ligi ya Angola.
05/11/2025, Petro de Luanda 1-0 Interclube, mchezo wa ligi ya Angola.
09/11/2025, Petro de Luanda 0- 1 de Agosto, mchezo wa ligi ya Angola.
Kwenye mechi 5 zilizopita timu hiyo imepata ushindi mechi 3. Ilipoteza mechi 2. Safu ya ushambuliaji ilifunga jumla ya magoli 8 wastani wakufunga kila baada ya dakika 56 huku ukuta ukiruhusu kufungwa magoli 3.

SOMA HII: Ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara ya NBC 2025/26 hii hapa | Mechi za Dabi, kanuni kwa timu ambayo haitafika uwanjani

image

H2H

22/11/2025 ni Simba SC vs Petro de Luanda

06/02/2025 ni Petro de Luanda vs Simba SC

Hitimisho

Simba SC vs Petro de Luanda nani atachukua pointi tatu CAF Champions League? Jibu litapatikana Jumapili kabla siku haijaisha. Mnyama anatabiriwa kupata ushindi mbele ya wapinzani Petro de Luanda. Licha ya faida ya kuwa nyumbani bado matokeo rasmi yatafahamika baada ya mchezo kukamilika.

Share this: