- Simba SC vs Petro de Luanda CAF Champions League 2025/26 utapigwa Uwanja wa Mkapa Novemba 22,2025.
- Matokeo ya mechi zilizopita za Simba SC na Petro de Luanda yasome hapa.
- Mabingwa watetezi wa CAF Champions League ni Pyramids 2025/26.
Simba SC vs Petro de Luanda CAF Champions League ni mchezo unaofuata kwenye ratiba kimataifa. Ni Novemba 22,2025 wababe hao kutoka kundi D watakutana kusaka pointi tatu muhimu, Uwanja wa Mkapa. Mnyama anapewa nafasi kubwa kushinda mchezo huo lakini vijana wa Angola sio wakubeza hata kidogo.
SOMA HII: Makundi Klabu Bingwa Afrika CAF 2025/26 haya hapa | Simba SC na Yanga SC zapewa waarabu
Shinda sasa na ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa hivi
Zamu yako kushinda na SportPesa, unaweza kushinda mamilioni sasa hivi. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kupitia Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa bonyeza picha hii chini.

Simba SC vs Petro de Luanda CAF Champions League utakuwa mchezo wa aina gani?

Kwenye hatua ya makundi Simba SC vs Petro de Luanda CAF Champions League unatarajiwa kuwa mchezo mkali. Hii inatokana na aina ya matokeo ya timu hizi kwenye mechi zilizopita. Petro de Luanda amekuwa na rekodi kushinda ugenini huku Simba SC ikiwa haijashinda nyumbani.
Mtifuano mkubwa unatarajiwa kuwa pande zote mbili. Ukubwa wa mashindano nao unatajwa kuwa sababu kuongeza ugumu. Hakuna timu yenye uhakika asilimia 100 kupata matokeo mazuri.
Matokeo ya mechi 7 za Simba SC

Novemba 8,2025, JKT Tanzania 1-2 Simba SC, NBC Premier League.
Oktoba 26,2025, Simba SC 0-0 Nsingizini Hotspurs, CAF Champions League.
Oktoba 19,2025, Nsingizini Hotspurs 0-3 Simba SC, CAF Champions League
Oktoba Mosi 2025, Simba SC 3-0 Namungo FC, mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Septemba 28 2025, Simba SC 1-1 Gaborone United, Ligi ya Mabingwa Afrika.
Septemba 25 2025, Simba SC 3-0 Fountain Gate mchezo wa Ligi Kuu Bara.
Septemba 20 2025, Gaborone United 0-1 Simba SC, Ligi ya Mabingwa Afrika.
Matokeo ya mechi 7 kwa Petro de Luanda

05/10/2025, Wiliete SC 0-2 Petro de Luanda mchezo wa ligi ya Angola.
18/10/2025, Stade d’Abdjan 0-2 Petro de Luanda, CAF Champions League.
25/10/2025, Petro de Luanda 2-0 Stade d’Abdjan Caf Champions League.
29/10/2025 Sao Salvador 2-1 Petro de Luanda, mchezo wa ligi ya Angola.
01/11/2025, Petro de Luanda 4-1 Libolo, mchezo wa ligi ya Angola.
05/11/2025, Petro de Luanda 1-0 Interclube, mchezo wa ligi ya Angola.
09/11/2025, Petro de Luanda 0- 1 de Agosto, mchezo wa ligi ya Angola.
SOMA HII: Mechi za Simba SC 2025/26 CAF Champions League, NBC Premier League ni moto| Matokeo na wafungaji

H2H
22/11/2025 ni Simba SC vs Petro de Luanda
06/02/2025 ni Petro de Luanda vs Simba SC
Msimamo wa kundi D
1. Petro de Luanda
2.Esperance
3. Simba SC
4. Stade Malien
Kuhusu timu hatua ya makundi.
Katika hatua ya makundi kuna timu 16 ambazo zinawania taji hilo. Bingwa mtetezi ni Pyramids FC huku timu iliyotwaa mara nyingi taji hilo ikiwa ni Al Ahly FC. Kila kundi litatoa timu mbili ambazo zitatinga hatua ya robo fainali.
Hitimisho
Simba SC vs Petro de Luanda CAF Champions League ni mchezo wa ufunguzi kwa mnyama nyumbani. Katika kundi D kila timu ina mechi tatu za nyumbani na tatu ugenini. Timu ambazo zitamaliza kwenye msimamao nafasi ya kwanza na ile ya pili zitasonga mbele hatua inayofuata.

