- Iran 2-0 Tanzania, haya ndio matokeo rasmi kwenye mchezo wa kirafiki kwenye Uwanja wa Rashid.
- Wenyeji Iran walipata ushindi kupitia magoli ya Amirhossen Hosseinzadeh na Mohammad Mohebi.
- Haya ndio matukio, magoli na matokeo rasmi ya Iran vs Tanzania
Iran 2-0 Tanzania ndio matokeo rasmi kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliochezwa Oktoba 14,2025 pale Dubai. Iran walipata goli la kwanza kupitia tuta la penalti dakika ya 17 na kuongeza la pili dakika ya 26. Mchezo uliopita Tanzania, ilipoteza kwa kufungwa goli 1-0 dhidi ya Zambia, mchezo uliochezwa Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
Unasubiri nini? Vuna mamilioni sasa hivi
Kuna jambo umekwama kwa sasa kuhusu mkwanja? Usiogope, rubani ni jasiri na kazi yake ni kupaisha kindege cha SportPesa. Cheza sasa hivi Aviator uvune mamilioni bofya hapa chini.

SOMA HII: CHAN 2024: Central African 0-0 Tanzania | Matokeo, vikosi, takwimu |Feisal Salum na tuzo
Iran 2-0 Tanzania, wajue wachezaji waliofunga magoli

Amirhossen Hosseinzadeh alifungua pazia la kufunga dakika ya 17, huku Mohammad Mohebi akitikisa wavu dakika ya 26. Kufikia kipindi cha pili Iran waliongeza goli tatu lilikataliwa na mwamuzi wa mechi. Magoli hayo yalidumu mpaka mwisho wa mchezo huku Tanzania ikipoteza kwa 2-0 dhidi ya Iran.
Haya ndio maoni ya Kocha Mkuu wa Tanzania Hemed Morocco

Morocco amesema:”Tulikuwa na mchezo mgumu, tulipata nafasi tukashindwa kutumia. Makosa ya mtu mmojammoja yalitokea na hapo wapinzani wakapata nafasi wakatumia.
“Tulikuwa tumeanza vizuri dakika 20, 25 kulikuwa na presha kubwa kutoka kwa wapinzani wetu Iran. Kwa aina ya wachezaji ambao tupo nao makosa ambayo yanatokea ni sehemu ya mchezo. Katika dakika za mwanzo tulikuwa tunafanya kazi kubwa. Mwisho wapinzani wetu walikuja kulazimisha kutafuta magoli.
“Ninajivunia kwa ajili ya wachezaji kwa namna ambavyo wanacheza. Kuna mwendelezo ambao upo kwa ajili ya wakati ujao. Ilikuwa ni mechi ngumu hivyo tukipata mechi nyingine kama hizi tutakuwa bora zaidi.
“Kipindi cha pili tulikuja na mbinu ya kutafuta usawa. Haikuwa hivyo bado tulikwama kufunga. Unaona kuna mwendelezo ambao upo kwa kuwa vijana wanazidi kuwa imara.
Magoli yote yalifungwa kipindi cha kwanza na nyota wa Iran, dakika ya 17 kwa mkwaju wa penalti na dakika ya 26.
SOMA HII: CHAN 2024: Tanzania 2-1 Madagascar Mzize afunga magoli mawili/ Robo fainali imejibu, rekodi, magoli

Kikosi cha Iran vs Tanzania
Kocha Mkuu, Amir Ghalenoei
Mlinda mlango
P. Niazmand
Mabeki
D Esmaeulifar
S. Khalilzadeh
M.A. Hazbavi
M. Mohammadi
Viungo
S.Ghoddos
S. Ezatolahi
K.Taheri
Washambuliaji
A.Hisseinzade
M.Hashemnejad
M. Mohebi.
Wachezaji wa akiba
Mohammadjavad Hosseinnehed
Alireza Jahanbakhs
Ali Nemati
Mohammad Ghorbani
Allahyar Sayyadmanesh
Ali Alipour
Mohammadreza Akhbari
Alireza Beiranvand
Omid Noorafkan
Mehdi Zare
Mohammad Khodabandelou
Ramin Rezaeian.
Kikosi cha Tanzania, Taifa Stars vs Iran

Kocha Mkuu Hemed Suleiman
Mlinda mlango
Yakoub Suleiman
Mabeki
Ibrahim Bacca
Pascal Msindo
Bakari Nondo
Israel Mwenda
Viungo
T. Allarakhia
Miroshi
Y. Omary
Feisal Salum
Washambuliaji
P.Peter
C. M’Mombwa
Wachezaji wa akiba
Lusajo Mwaikenda
Morice Abraham
Abdul Suleiman
Zuber Foba
Offen Chikola
Miano Danilo
Lameck Lawi
Hussen Masaranga
Khalid Habibu
SOMA HII: CHAN 2024: Tanzania 0-1 Morocco ni kilio kwa wenyeji | Matukio muhimu, vikosi, takwimu

Hitimisho
Iran 2-0 Tanzania ndio matokeo kwenye mechi ya kirafiki iliyochezwa pale Dubai. Kwa Taifa Stars kilikuwa ni zaidi ya kipimo kwa kuwa wachezaji wamepata nafasi kujitangaza. Kukosa ushindi kutawapa nafasi kujipanga kwa mechi zijazo kuwa imara zaidi. Baada ya mchezo huu, Iran wanajipanga kwenda kwa mashindano mengine ya timu nne yatakayofanyika Dubai mnamo Novemba 2025.

