- Hersi Ally Said, Rais wa Yanga SC na Mwenyekiti wa African Club Association (ACA), ateuliwa na FIFA.
- Hii ni baada ya kuteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Mashindano ya Klabu za Wanaume Duniani.
- Msimamizi wa soka huyu na Mwanabiashara amechaguliwa kufuatia kuonyesha ukakamavu kwenye uongozi wa masuala ya soka barani Afrika.
Hersi Ally Said, Rais wa Yanga SC ameteuliwa na FIFA kuwa Mjumbe wa Kamati ya Klabu za Wanaume Duniani. Mtendaji wa soka na mwanabiashara huyu, ameandika historia mpya kufuatia uteuzi huu. Ametuliwa kuwakilisha kwa kipindi cha miaka minne kuanzia 2025 hadi 2029. Fahamu kiundani kuhusu uteuzi wa Hersi Said FIFA kupitia nakala hii.
Cheza na ushinde sasa na ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni muda huu
Unaweza kuwa mshindi mpya wa mamilioni ya SportPesa muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kucheza kupitia Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa bonyeza picha hii chini.

Kuhusu Hersi Said Rais wa Yanga SC kuteuliwa FIFA

Uteuzi wa Mhandisi Hersi unatajwa kuwa ni hatua ya kihistoria. Hii ni kwa kuwa unamfanya Hersi kuwa mtu wa kwanza kutoka Afrika Mashariki na Kati, kuhudumu kwenye mojawapo ya kamati zenye ushawishi mkubwa zaidi ndani ya FIFA. Kamati hii ina jukumu la kusimamia, kutoa ushauri, na kuunda mwelekeo wa baadaye kwa mashindano ya klabu za wanaume duniani. Hii inahusisha Kombe la Dunia la Klabu na michuano mingine ya kimataifa.
Mhandisi Hersi amekuwa kinara katika mageuzi makubwa ndani ya klabu ya Yanga SC. Hii ni baada ya kuibadilisha kuwa moja ya vilabu bora na zinazoendeshwa kisasa barani Afrika. Ikumbukwe kuwa uongozi wake umevuka mipaka ya Tanzania na kupata kutambuliwa barani kote. Kwa sasa akijulikana pia katika nafasi ya Mwenyekiti wa Chama cha vilabu barani Afrika.
SOMA HII PIA: Injinia Hersi anaondoka au bado yupo Yanga? Mwenyewe afunguka mazito ishu ya siasa

Wadau wampongeza Hersi

Tangu tangazo la uteuzi huo, wadau wa soka kutoka kila kona ya Afrika wameendelea kumpongeza Hersi. Wengi wao wameeleza kuwa, hii ni ishara ya kutambuliwa kwa juhudi zake, ubunifu, na maono yake. Hii yote ni katika kukuza mchezo huo zaidi ya mipaka ya kitaifa.
Miongoni mwa wale waliompongeza ni Makamu rais wake ndani ya Yanga SC, Arafat Haji ambaye amesema: “Hongera sana kwa kuteuliwa na FIFA, kuwa Mjumbe wa Kamati ya Mashindano ya vilabu kwa Wanaume Duniani. Hii si tu, ni heshima kwako binafsi, bali ni fahari kwa Tanzania, Yanga SC na Afrika kwa ujumla.
“Uongozi wako umeendelea kuwa chachu ya mabadiliko, dira ya maendeleo, na uthibitisho kwamba mipaka ya mafanikio haipo pale penye juhudi, maono na uadilifu. Tunajivunia. Endelea kupeperusha bendera ya nchi yetu kimataifa.”
SOMA HII ZAID: Ujenzi Uwanja wa Yanga SC balaa! Injinia Hersi afanya kikao Kizito

Alichosema Hersi baada ya uteuzi

Kufuatia uteuzi huo, Hersi amesema: “Ninajivunia kuwajulisha kuwa, nimepata heshima kubwa ya kuteuliwa na FIFA kuwa mjumbe wa Kamati ya Mashindano ya Klabu za Wanaume. Hii ni kwa kipindi cha 2025–2029. Uteuzi huu sio mafanikio binafsi tu, bali ni tukio la kujivunia kwa Afrika Mashariki. Lakini pia huu ni ujumbe mzito kuwa, uongozi kutoka ukanda huu unatambuliwa katika ngazi ya juu ya kimataifa.”
Hersi amesema kupitia nafasi yake ndani ya Yanga SC pamoja na Jumuiya ya Vilabu vya Afrika (ACA), ameona uwezo mkubwa wa vilabu vya Afrika. Kutokana na hilo amesisitiza umuhimu wa kuwakilishwa kwenye meza za maamuzi ya kimataifa.
“Ninaamini jukumu hili litatoa nafasi kwa Afrika kuwa na sauti thabiti, katika maamuzi makubwa ya soka la vilabu duniani. Ni wakati wa Afrika kushiriki kikamilifu katika mabadiliko ya kisasa ya mchezo huu. Hii ni katika kuhakikisha tunaleta maendeleo ya mchezo.”
Hersi awashukuru viongozi wakuu wa FIFA
Kutokana na Imani ya uteuzi huo, Hersi amewashukuru Rais wa FIFA Gianni Infantino, Rais wa CAF Dkt. Patrice Motsepe, na Katibu Mkuu wa FIFA Mattias Grafström. Hii ni kutokana na kumuamini na kwa kuendeleza jitihada za kuinua soka la Afrika.
“Ninathamini sana imani waliyonionyesha. Nafasi hii si yangu peke yangu, bali ni ya kila kijana wa Kiafrika anayeamini kuwa ubora hauna mipaka. Nitawajibika kufanya vizuri zaidi,” amesema Hersi.
Hersi ahudhuria mkutano Mkuu wa 32 wa EFC, Roma
Mnamo Oktoba 7–9, 2025, Hersi pia alihudhuria Mkutano Mkuu wa 32 wa Shirikisho la vilabu vya Ulaya (EFC), uliofanyika jijini Roma, Italia. Mkutano huu ulihudhuriwa na viongozi wakuu wa soka duniani. Hii ni Pamoja na Rais wa FIFA Gianni Infantino na Mwenyekiti wa EFC, Nasser Al-Khelaïfi. Katika tukio hilo la kihistoria, ECA ilibadilika rasmi na kuwa EFC. Hatua iliyolenga kuimarisha mshikamano wa vilabu vya Ulaya, na duniani kwa ujumla.
SOMA HII PIA: SportPesa yaipa Yanga SC Milioni 262.5: Makombe matano yatajwa

Zaidi ya klabu 800 zahudhuria

Baada ya kuhudhuria mkutano huo Hersi amesema: “Ilikuwa heshima kubwa kuwa sehemu ya tukio hili kubwa la kihistoria. Zaidi ya vilabu 800 vilihudhuria. Jambo linaloonyesha nguvu ya umoja na ushirikiano katika kusukuma mbele soka la klabu duniani.
Katika mkutano huo, Nasser Al-Khelaïfi alisisitiza kuwa ingawa EFC itaweka Ulaya mbele. Lakini itaendelea kushirikiana kimataifa, ili kusaidia vilabu vya mabara mengine. Hii ni katika kujenga mifumo imara ya kitaasisi.
Hitimisho
Kufuatia Hersi Ally Said, Rais wa Yanga SC kuteuliwa FIFA, inaonyesha ukuaji na ushawishi wa soka la Afrika Mashariki. Hii ni nafasi kubwa kwake kuthibitisha imani ya waliomteua na kukuza soka la Afrika. Atawakilisha kwa muda wa miaka minne itakayoanza mwaka huu wa 2025 hadi 2029. Miongoni mwa majukumu makubwa ambayo anatarajiwa kuwa nayo ni; kushiriki katika kusimamia, kutoa ushauri, na kuunda mwelekeo wa baadaye kwa mashindano ya klabu za wanaume duniani.

