- Sio siri tena! Maisha ya kocha, Roman Folz yamethibitishwa kufika mwisho.
- Taarifa ni kuwa uongozi wat imu hiyo umemfuta kazi rasmi, sasa inasubiriwa taarifa kwa Umma.
- Kufuatia maamuzi hayo, kocha mpya Yanga SC kutua kutoka Madagascar.
Dili limetiki ndivyo unavyoweza kusema, hii ni baada ya taarifa za ndani ya Yanga SC kuthibitisha ujio wa kocha mpya. Wananchi wako kwenye hatua za mwisho za kuachana na kocha Folz, huku ikielezwa kuwa kocha mpya Yanga SC ni Romuald Rakotondrabe. Kocha huyo anatajwa kuchukua mikoba ya kuiongoza Yanga SC, baada ya kupata mafanikio makubwa akiwa na timu ya Taifa ya Madagascar.
SOMA HII PIA: Roman Folz kufukuzwa Yanga SC, kocha mpya huyu hapa
Cheza na ushinde sasa na ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni muda huu
Hujashinda na kindege cha SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kubashiri SportPesa bonyeza picha hii chini.

Kwa ufupi, mjue Kocha mpya Yanga SC, Romuald Rakotondrabe

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya Yanga SC, uongozi wa timu hiyo umetajwa kuwa kwenye mazungumzo ya mwisho na kocha wa timu ya taifa ya Madagascar, Romuald Rakotondrabe. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 60 amekuwa na mafanikio makubwa akiwa na Madagascar. Hii ni baada ya kuipeleka Madagascar fainali kwenye michuano ya CHAN 2024. Japokuwa dili hilo bado halijakamilika kwa asilimia 100, Ila pande hizo mbili zimefikia pazuri.
SOMA HII ZAIDI: Romain Folz amefutwa kazi Yanga SC? Ratiba ya mechi zijazo Jangwani

Kocha Romuald kutua Tanzania
Mpaka sasa kwa 90% Yanga na Romuald Rakotondrabe wamekubaliana kila kitu, kilichobaki ni kocha huyo kusaini mkataba na kutangazwa. Hii ni kwa mujibu wa gwiji wa Habari za usajiri, Hans Raphael. Muda wowote kutoka sasa kocha huyo atatua Bongo kusaini mkataba wa miaka miwili.
Nini kitatokea kwa Folz?

Kwa mujibu wa Hans, licha ya kurejea nchini kocha Romain Folz anatarajiwa kupewa barua ya kufutwa kazi, muda wowote kuanzia sasa. Hii ni baada ya tathimini yao kuonyesha kocha huyo ameshindwa kuthibitisha ubora wake.
Taarifa kuhusu kocha Folz kufukuzwa Yanga SC ziliripotiwa muda mrefu, lakini zilipata nguvu zaidi baada ya mchezo wao dhidi ya Mbeya City. Ripoti za hivi karibuni zimethibitisha kuwa uongozi wa Yanga SC umemfuta kazi kocha Folz. Taarifa hiyo inaeleza sababu kubwa ya maamuzi hayo ni kutokana na shinikizo la mwenendo usioridhisha wa kikosi.
Romain Folz alipewa nafasi ya kuwa kocha wa Yanga kuanzia msimu wa 2025/26, akichukua nafasi ya Miloud Hamdi. Kocha huyo alipewa malengo ya kudumisha utawala wa ndani, pamoja na kuifikisha mbali Yanga SC katika michuano ya Afrika. Lakini licha ya matumaini makubwa, kuna dalili zinazoonyesha kutoridhika kwa baadhi ya mashabiki na uongozi.
SOMA HII PIA: Romain Folz bado yupoyupo Yanga SC | Ratiba ya mechi zijazo, Kariakoo Dabi

Kuna sababu nyingine za kumng’oa folz Yanga SC?
Ukiachana na kiwango cha timu kuelezwa kushuka na matokeo ya mchezo dhidi ya Mbeya City, inaelezwa kuna sababu nyingine za kumtimua Folz. Hii ni pamoja na matatizo ya mambo ya ndani. Hii ikimaanisha kufanya marekebisho katika benchi la ufundi, wasaidizi na wataalamu wengine.
Makocha wengine wanaotajwa kumrithi Folz Yanga SC

Ukiachana na Romuald, wapo makocha wengine ambao wametajwa kuwindwa na Yanga SC. Miongoni mwa makocha hao ni, Sead Ramovic. Ikumbukwe kuwa Ramocic aliwahi kuhudumu kwa muda mfupi ndani ya Yanga SC, kwa sasa yupo nchini Algeria.
Sead Ramović alijiunga na Yanga SC tarehe 15 Novemba 2024, akichukua nafasi ya Miguel Gamondi. Mwanzoni alionyesha uzoefu mzuri katika ligi ya ndani, Yanga ilishinda michezo mingi kwa soka lake maarufu ‘Gusa Achia, twende kwao’. Lakini licha ya mwanzo mzuri, matokeo ya kimataifa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika hayakuenda kama walivyopanga. Hii ilipelekea Ramović kuondoka na kujiunga na klabu ya CR Belouizdad ya Algeria.
Matokeo ya Yanga SC chini ya kocha Romain Folz

Yanga 1-0 Bandari ya Kenya. (Mechi ya kirafiki)
Yanga SC 1-0 Simba SC, (Ngao ya Jamii).
Wiliete 0-3 Yanga SC, (Ligi ya Mabingwa Afrika).
Yanga SC 3-0 Pamba Jiji, (Ligi ya NBC).
Yanga 2-0 Wiliete SC, (Ligi ya Mabingwa Afrika).
Mbeya City 0-0 Yanga SC, (Ligi ya NBC).
Hitimisho
Wakati ikisubiriwa uthibitisho rasmi wa kocha, Roman Folz kufukuzwa Yanga SC, shinikizo limezidi kuwa kubwa. Hii ni kutokana na matokeo pamoja na kiwango cha timu. Hivyo ujio wa kocha mpya Yanga SC, unatarajia kuamsha tena ari ya ushindani ambayo itasaidia kutimiza malengo yao.


