Kocha mpya Simba SCDimitar Pentev
  • Pantev alikuwa akifundisha Klabu ya Gaborone inayoshiriki Ligi Kuu ya Botswana.
  • Mifumo ya Dimitar Pantev Kocha Mkuu Simba SC inakwenda kuonekana kwa mara ya kwanza katika mechi za kimataifa.
  • Kwenye mechi zijazo Yanga SC vs Simba SC ipo katika ratiba inatarajiwa kupigwa Uwanja wa Mkapa, Desemba 13 2025.

Mifumo ya Dimitar Pantev Kocha Mkuu Simba SC kwa mara ya kwanza itaonekana kimataifa. Mrithi huyo wa mikoba ya Fadlu Davids yupo Tanzania. Oktoba 4 2025 aliwasili na kuanza majukumu yake kukifundisha kikosi hicho. Kocha huyo anatajwa kupendeleza zaidi mfumo wa kushambulia akitumia 4-3-3

SOMA HII: Dimitar Pantev kocha mpya Simba SC anapenda kushambulia | Mkataba wake, orodha ya wachezaji wapya

Shinda sasa na ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni muda huu

Zamu yako kushinda na SportPesa, unaweza kushinda mamilioni sasa hivi. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kupitia Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa bonyeza picha hii chini.

image

Mifumo ya Dimitar Pantev Kocha Mkuu wa Simba SC mechi zijazo

 Mifumo ya Dimitar Pantev Kocha Mkuu wa Simba SC
Dimitar Pantev, Kocha Mkuu wa Simba SC 2025/26. Source: Simba SC.

Mnyama alipishana na ubingwa msimu wa 2024/25 ndani ya NBC na Kombe la Shirikisho Afrika. Mifumo ya Dimitar Pantev Kocha Mkuu wa Simba SC inasubiriwa kutoa majibu kwenye mechi za ushindani. Kazi yake ya kwanza itakuwa katika hatua ya pili ya mtoano Ligi ya Mabingwa Afrika. Ni Oktoba 17 dhidi ya Nsingizini Hotspurs ya Eswatini.

Simba SC imempa kandarasi ya miaka miwili Pantev kukinoa kikosi hicho. Kabla ya kujiunga na Simba SC alikuwa Gaborone United. Timu hiyo iliondolewa na Simba SC katika hatua ya awali.

Mchezo wake wa pili kwa Pantev utakuwa Uwanja wa Mkapa. Oktoba 24-25 Simba SC vs Nsingizini Hotspurs utakuwa mchezo wa kwanza Uwanja wa Mkapa. Tayari kocha huyo ameanza kazi akishirikiana na Selemena Matola ambaye ni kocha msaidizi.

Mechi zijazo za Pantev ndani ya Simba SC

Kocha mpya Simba SC CV
Dimitar Pantev kwenye ardhi ya Tanzania kuanza majukumu kuifundisha Simba SC. Source: Simba SC.

Novemba 2 2025, Simba SC vs Azam FC, Uwanja wa Mkapa. Huu utakuwa mchezo wa kwanza kweye Ligi ya NBC. Utakuwa ni mchezo wa tatu kwenye ligi kwa kuwa Simba SC imecheza mechi mbili na kupata ushindi.

Funga kazi ndani ya 2025 itakuwa ni Kariakoo Dabi. Mchezo huo uatarajiwa kuchezwa Desemba 13 2025. Yanga SC vs Simba SC, Uwanja wa Mkapa.

Hii itakuwa ni Kariakoo Dabi ya kwanza kwa Pantev. Fadlu ambaye yupo ndani ya Raja Casablanca alipoteza mechi zote dhidi ya Yanga SC. Kocha huyu atakuwa na kazi kubwa kuvunja rekodi hiyo inayoitesa Simba SC.

SOMA HII: Simba SC yatambulisha mbeba mikoba ya Zimbwe Jr 2025/26 Antony Mligo | Sekeseke lake la usajili

image

Neno la Pantev baada ya kutua Bongo

Pantev ambaye Simba SC wamempa cheo cha kuwa Meneja Mkuu amebainisha kuwa anapenda kuona matokeo mazuri. Pantev aliongeza anatambua ushindani upo hilo halimpi shida. Kutokan ana kufundisha soka la Afrika ni mwanzo kuendelea pale alipoishia.

“Nimefurahi kuwa hapa na kuanza kazi ndani ya Simba SC. Uzoefu kwenye kufundisha soka la Afrika ninao. Ninapenda kuona timu inakuwa kwenye umiliki wa mpira na kushambulia kutafuta matokeo.”

Ahmed Ally kuhusu Pantev

Ahmed Ally kwenye uzinduzi wa jezi mpya za Simba SC 2025/26
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC. Source: Simba SC.

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC, Ahmed Ally amesema Pantev ni mwalimu wa mbinu. Amebainisha kuwa mara baada ya kutua Dar tayari Simba SC imeanza kubadilika. Aidha aliwaomba mashabiki kuwa na subira kupata kilicho bora.

“Mwalimu Pantev ni mtu wa mpira ambaye ataleta mabadiliko makubwa. Yeye anapenda mpira wa kasi na kushambulia zaidi. Amesema kuwa hakuna kupiga pasi za nyuma ni mwendo wa mbele kwa mbele.

“Mbinu zake nyingi ni bora hivyo tutaona mabadiliko makubwa kwenye uchezaji. Tunakwenda kuona Simba SC yenye kasi kwelikweli.Tunakwenda kushuhudia burudani na pasi nyingi zikipigwa uwanjani.

“Kikubwa mashabiki wawe na subira mambo mazuri yanakuja. Mchezo wake wa kwanza itakuwa Oktoba 17 kwenye anga la kimataifa. Tunaamini kazi kubwa itafanyika kutokana na uwezo alionao na ubora wa wachezaji wetu,”.

SOMA HII: Mechi ya kirafiki: Simba SC 2-0 Kahraba Ismailia| Jonathan Sowah na Bajaber wafunga magoli

image

Hitimisho

Mifumo ya Dimitar Pantev Kocha Mkuu Simba SC itatoa majibu ya kile ambacho kilitokea katika hatua ya awali. Kwenye mchezo wa Simba SC vs Gaborone United aliyokuwa akiifundisha timu hiyo ilitoa upinzani mkubwa kwa mnyama. Mchezo mwingine unaosubiriwa ni Kariakoo Dabi dhidi ya Yanga SC Uwanja wa Mkapa.

image




Share this: