- Simba SC wanatarajiwa kukabiliana na Namungo FC kwenye mechi ya pili ya Ligi Kuu ya NBC 2025/26.
- Mchezo huu mkali wa Simba SC vs Namungo FC utapigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Jumatano hii ya Oct 1, 2025.
- Baada ya kufungua ligi kwa ushindi wa mabao 3-0 Je, Simba SC wataendeleza wimbi la ushindi Jumatano kwa Mkapa?
Baada ya kufanikiwa kuibuka na ushindi muhimu wa mabao 3-0, katika mchezo wao wa ufunguzi wa Ligi Kuu ya NBC 2025/26. Kikosi cha Simba SC Jumatano hii kitashuka tena uwanjani, kuwinda ushindi wao wa pili. Timu hizi Simba SC vs Namungo FC zimeweza kukabiliana mara 12, huku Simba SC wakiibukia washindi mara 7, michezo 5 iliyosalia ikiisha kwa sare.
SOMA HII PIA: Namungo FC—Muhtasari, Kikosi, Ratiba, Matokeo, Takwimu, Tuzo na Habari Mpya
Cheza na ushinde sasa na ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni muda huu
Ni zamu yako kushinda na SportPesa, unaweza kushinda mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kupitia Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa bonyeza picha hii chini.

H2H kati ya Simba SC vs Namungo FC

Kiujumla katika historia ya ushindani wa timu hizi mbili zimekutana katika michezo 12. Simba SC wamefanikiwa kushinda mechi 7, Namungo FC hawajashinda mchezo wowote. Michezo mitano iliyosalia iliisha kwa matokeo ya sare. Hivyo mechi ya Jumatano hii usiku itakuwa mechi yao ya 13 kwao kukutana.
SOMA HII ZAIDI: Simba SC yatambulisha mbeba mikoba ya Zimbwe Jr 2025/26 Antony Mligo | Sekeseke lake la usajili

Michezo mitano iliyopita ya Simba SC
28 Sep Simba SC 1-1 Gaborone United
25 Sep Simba SC 3-0 Singida Big Stars
20 Sep Gaborone United 0-1 Simba SC
25 Jun Young Africans 2-0 Simba SC
22 Jun Simba SC 1-0 Kagera Sugar
Michezo mitano iliyopita ya Namungo FC
21 Sep Namungo FC 1-0 Tanzania Prisons
18 Sep Namungo FC 1-1 Pamba Jiji
22 Jun Namungo FC 5-0 KenGold
18 Jun Namungo FC 0-0 Kagera Sugar
13 May Young Africans 3-0 Namungo FC
Kikosi cha Simba SC kinachotarajiwa kucheza dhidi ya Namungio FC

Kipa :
Yakoub Suleiman
Walinzi:
Kapombe, Naby, Karabou, Rushine,
Viungo:
Kagoma, Kibu, Ahoua,
Washambuliaji:
Sowah, Morice, Mpanzu
Kikosi cha Namungo FC kinachotarajiwa kucheza dhidi ya Simba SC

Kipa:
Jonathan Nahimana
Walinzi
Machupa Jr, Amoah, Kazi, Jigwa
Viungo
Nyenye, Lukindo, Jofrey
Washambuliaji
Shahame, Makambo, Kipenye
Habari mpya kuhusu Simba SC vs Namungo FC

Kocha Suleiman Matola anatarajiwa kurejea tena kwenye benchi la Simba SC kuiongoza timu hiyo. Hii ni baada ya kuukosa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Gaborone United. Ikumbukwe Matola aliukosa mchezo huo kutokana na kutumikia adhabu ya kadi nyekundu. Kocha huyo ndiye aliyeipa Simba SC ushindi wake wa kwanza msimu huu, mbele ya Fountain Gate FC.
Kutokana na changamoto hizo hususani ya kumpoteza kocha wao mkuu, Fadlu Davis. Simba walilazimika kumteua kocha wa Stars, Hemed Morocco kuwa kocha wa muda. Hivyo sasa Matola anarejea kuendeleza majukumu yake, huku Simba ikielezwa inatarajia kumtangaza kocha mkuu mpya hivi karibuni.
SOMA HII ZAIDI: Simba SC 3-0 Fountain Gate FC | Rushine afungua akaunti ya magoli Uwanja wa Mkapa

Semaji Ahmed atamba kuendeleza ‘ubaya ubwela’ part 2
Akiendelea kuzungumzia mwanzo bora wa kikosi chao, Ahmed amesema: “Wanasimba tutulie, mambo mazuri yanakuja ndugu zangu Wana Simba. Hii ni timu kubwa yenye msingi imara ya kitaasisi na niwakumbushe kuwa tumejipanga vizuri msimu huu.
“Ni jambo la kawaida Watumishi kuajiriwa na kuoandoka kwenye timu. Muhimu ni kutafuta mbadala sahihi na bora zaidi ya aliyeondoka, ninachoweza kuwahikikishia kwamba hakuna kitakachoharibika, wala kurudi nyuma ndani ya klabu yetu. Tunasonga mbele tukiwa bora na imara zaidi kuutimiza ubaya ubwela part 2.”
Hitimisho
Kwa namna ambavyo msimu wa Ligi Kuu ya NBC 2025/26 umeanza kwa ushindani mkubwa miongoni mwa timu shiriki, hii inaonyesha ni kwa kiasi gani kila timu imejizatiti. Licha ya Simba SC kuanza kwa kishindo msimu mpya wa 2025/26 bado mechi ya Simba SC vs Namungo FC inatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa. Simba SC watakuwa wanasaka kuendeleza rekodi yao ya asilimia 100 ya ushindi dhidi ya Namungo FC ambao wanasaka kuvunja mwiko.

