Ellie Mpanzu EMEllie Mpanzu EM
  • Gaborone United hawana chakupoteza kwenye mchezo ujao Uwanja wa Mkapa ambao utachezwa bila ya uwepo wa mashabiki kutokana na adhabu ya CAF.
  • Simba SC 1-0 Gaborone Unted CAF Champion League jasho limevuja kwa wachezaji katika anga la kimataifa.
  • Ellie Mpanzu goli lake la mapema limudumu mpaka mwisho wa mchezo kimataifa akitumia pasi ya Shomari Kapombe

Simba SC 1-0 Gaborone United CAF Champion League baada ya dakika 90 kukamilika ugenini. Goli pekee kwenye mchezo wa leo limefungwa na nyota Ellie Mpanzu dakika 15. Licha ya Gaborone United kuwa imara katika kushambulia walikutana na umakini wa mlinda mlango Moussa Camara.

Simba SC 1-0 Gaborone United CAF Champion League
Simba Gaborone

Vuna mamilioni kwa kupaisha Kindege cha SportPesa

Ni muda wako sasa hivi kuvuna mamilioni ukipaisha Kindege cha SportPesa. Ushindi ni mwingi na mkubwa unakusubiri wewe tu. Rahisi sana cheza Aviator upate mgao wako.

image

Simba SC 1-0 Gaborone United CAF Champion League ugenini

Ikiwa ugenini, Simba SC 1-0 Gaborone Unted CAF Champion League ikiwa ni hatua ya awali. Ushindi huo ulikuwa ni wa jasho kwa timu zote mbili. Licha ya Simba SC kupata ushindi kwenye mchezo huo ilitumia muda mwingi kujilinda kutokana na uimara wa wapinzani wao Gaborone United.

Soma hii: Gaborone United vs Simba SC Septemba 20 | Ligi ya Mabingwa Afrika, vikosi, H2H – SportPesa Tanzania

Mchezo huo umechezwa Uwanja wa Francistown na Gaborone. Katika mchezo wa pili utachezwa Uwanja wa Mkapa bila ya uwepo wa mashabiki. Hilo linatokana na adhabu ambayo Simba SC imepata kutoka kwa CAF.

Katika mchezo wa leo kocha msaidizi wa Simba SC Seleman Matola alionyeshwa kadi nyekundu. Ilikuwa ni kipindi cha pili dakika ya 68. Ni kadi moja pekee nyekundu imetolewa kwenye mchezo wa leo.

Goli la Ellie Mpanzu kimataifa

MP (-)
Ellie Mpanzu nyota wa Simba SC ambaye alianza kikosi cha kwanza dhidi ya Gaborone. Source: Simba SC.

Kiungo mshambuliaji wa Simba SC, Ellie Mpanzu alipachika goli la kwanza. Ni dakika ya 15 akiwa ndani ya 18 kwa pigo la kichwa. Pasi ilitoka kwa beki ambaye ni nahodha Shomari Kapombe. Simba SC imepata ushindi ikiwa imetoka kucheza mchezo mgumu dhidi ya Yanga SC.

Soma hii:Gaborone United Vs Simba SC: ‘Live’ CAF Champions League 2025, Botswana

Katika eneo la 18 kulikuwa na wachezaji wawili wa Simba SC, Mpanzu na Seleman Mwalimu. Chaguo la Kapombe ambaye alipokea pasi kutoka kwa Naby Camara ilikuwa ni moja kwa moja ndani ya 18 ikakutana na Mpanzu.

Jean Ahoua nafasi ya kwanza mapema

Ahoua Gaborone
Ahoua Jean kiungo mshambuliaji wa Simba SC. Source: Simba SC.

Kiungo mshambuliaji wa Simba SC alikuwa kwenye nafasi nzuri kufunga kipindi cha kwanza. Katika sekundi ya 56 Ahoua alifanya jaribio akiwa ndani ya 18 kuelekea lango la wapinzani wao. Ni pigo la mguu la kulia lilikwenda nje ya lango.

Mlinda mlango wa Gaborone, Thabo Musogore amekuwa akicheza na kutoa maelekezo. Simba SC kwenye anga la kimataifa msimu uliopita iliishia hatua ya fainali. Ilipoteza kwa kufungwa dhidi ya RS Berkane.

Anthon Mligo kwenye mikoba ya Zimbwe Jr

Beki wa kushoto wa Simba SC, Anthon Mligo kwenye mikoba ya Mohamed Hussen Zimbwe Jr. Zimbwe Jr kwa sasa yupo ndani ya kikosi cha Yanga SC. Kwenye mchezo wa leo kimataifa Mligo ameanza kikosi cha kwanza.

Katika dakika 45 za mwanzo amekuwa katika ubora wake kwenye kutimiza majukumu. Amekuwa akiokoa hatari zile za juu na chini akiwa uwanjani. Pia amekuwa akipewa majukumu kwenye mipira ya kurusha.

Miongoni mwa hatari ambazo aliokoa Mligo ambaye msimu wa 2024/25 alikuwa ndani ya kikosi cha Namungo FC ni dakika ya 44 na 45. Mguu wake wenye nguvu katika kutimiza majukumu ni ule wa kulia.

Kikosi cha Simba SC ambacho kilianza dhidi ya Gaborone United

Mousa Camara jezi namba 20 alianza langoni. Chamou beki anayeyevaa jezi namba 2, Athony Mligo beki wa kushoto, Allasane Kante jezi namba 8.

Jean Ahoua kiungo mshambuliaji jezi namba 10, Shomari Kapombe jezi namba 12, De Reuck beki wa kati jezi namba 23. Ellie Mpanzu, Naby Camara jezi namba 30, Maema jezi namba 35 na Seleman Mwalimu jezi namba 40 huyu ni mshambuliaji.

Wachezaji wa akiba

Yakoub Suleman, Ladack Chasambi, Wilson Nangu, Mzamiru Yassin, Kibu Dennis, Morice Abraham. Steven Mukwala, Jonathan Sowah, Joshua Mutale hawa walikuwa kwenye kikosi cha akiba.

Hitimisho

Simba SC 1-0 Gaborone United CAF Champion League bado haijaisha mpaka iishe. Kwa namna ambavyo wapinzani wanacheza wamekuwa hawana hofu yoyote. Beki wa kati wa Simba SC, Rushine amekuwa katika kuokoa hatari nyingi wakishirikiana na Anthon Mligo.

image
Share this: