Afisa uhusiano na mawasiliano SportPesa- Jason NdambalaAfisa uhusiano na mawasiliano SportPesa- Jason Ndambala
  • Zikiwa zimebaki siku 3 tu, kuelekea kilele cha wiki ya wananchi Wadhamini wa Yanga SC wameungana.
  • Hii ni pamoja na mdhamini mkuu Kampuni ya SportPesa, ambao hivi karibuni walisaini nao mkataba wa Bilioni 21.7
  • Yanga SC vs Bandari FC Septemba 12, ndiyo burudani kubwa ya mchezo wa soka kwenye kilele wiki ya wananchi.
  • Burudani ya Zuchu inatarajiwa kuweka historia kwa Mkapa.

Huku ukisubiriwa mchezo mkali kati ya Yanga SC vs Bandari FC Septemba 12 kwenye kilele cha wiki ya wananchi, Makampuni wadhamini wa Yanga SC wameungana. Pamoja na mambo mengi ambayo wameyazungumza, kubwa ni kuandaa tamasha la kihistoria. Hii ni katika mchakato wa hamasa kuelekea tukio hilo.

SOMA HII ZAIDI: Wiki ya Mwananchi Septemba 12 2025 tunapiga kichwani tu | Matukio muhimu, burudani, wachezaji wapya

Paisha ‘Kindege’ cha Sportpesa ushinde mamilioni sasa kwa kubonyeza picha hii chini

image

Kuhusu Yanga SC vs Bandari FC Septemba 12 Tamasha la Wananchi

Ikumbukwe kuwa Wiki ya wananchi ni miongoni mwa matamasha makubwa ya soka kwa ukanda wa Afrika Mashariki. Kwa kawaida Tamasha hili, hutumiwa kwa ajili ya kutambulisha wachezaji na kikosi kipya mbele ya mashabiki. Sambamba na hilo burudani za muziki na mechi kali ya soka pia hunogesha.

Katika kusherehesha zaidi tukio hilo, katika miaka ya karibuni mara nyingi tamasha hilo huhusisha burudani mbalimbali za wasanii wakubwa wa ndani na nje ya Tanzania. Ambapo tayari kwa mwaka huu tayari Yanga wamemtangaza Malkia wa Bongo Fleva Zuchu kuwa mtumbuizaji wao mkuu.

Wadhamini wa Yanga waungana kufanya Tamasha la kihistoria

Mdhamini Mkuu SportPesa

Afisa uhusiano na mawasiliano SportPesa- Jason Ndambala
Afisa uhusiano na mawasiliano SportPesa- Jason Ndambala

Kampuni bora ya michezo ya kubashiri SportPesa, ndiyo wadhamini wakuu wa Yanga. Kupitia kwa Afisa uhusiano na mawasiliano, Jason Ndambala amesema: “Tunawashukuru sana Yanga kwa fursa hii adhimu ambayo tumepewa, kwa lengo la kuwa pamoja kwenye hii wiki.

“Ni matarajio yetu uhusiano wetu utaleta chachu na tukio hili kufana. Tutatoa ushirikiano mkubwa katika kila tukio ambalo litafanyika. Niwaombe mashabiki wengi kujitokeza uwanjani. Vile vile tunawasihi mashabiki kujisajili na Sportpesa na kubashiri nasi.”

SOMA HII ZAIDI: Mkutano mkuu wa Yanga SC 2025: Mambo 10 yaliyotikisa ‘Super Dome’ leo

Gsm bevarage

“Kesho tunapomaliza kuchangia damu, ukimaliza tunakupatia vinywaji mbalimbali kutoka GsM. Tutakuwepo kwenye matukio mbalimbali ambayo yatafanywa na Yanga kuhakikisha wananchi wanakata kiu. Mwaka huu tutatoa maji na soda uwanja mzima bure, siku ya kilele cha wiki ya mwananchi. Tutakuwa na vinywaji vya aina yote kutoka GsM Beverage,” amesema ofisa wa GSM Bevarage, Rukia Yazid.

 GSM Foundation

amesema ofisa wa GSM Bevarage- Rukia Yazid-
GSM Bevarage- Ofisa wa Rukia Yazid

“Sisi kama GSM Foundation tumefanya kazi nyingi sana na Yanga SC. Matukio yote ya kijamii ambayo yatafanywa katika wakati huu wa wiki ya mwananchi tutashiriki. Tunawaomba sana wananchi watuunge mkono. Tunawoamba mashabiki wajitokeze Kawe siku ya jumatano hasa hasa maeneo ya sokoni kufanya usafi pamoja na kuotesha miti maeneo ya kawe,” amesema Faith Gugu – GSM Foundation

Makampuni mengine yanayoidhamini Yanga ambayo yalituma wawakilishi waliozungumza ni pamoja na Haire.

Semaji Ali Kamwe naye atoa ratiba nzito kuelekea Yanga SC vs Bandari FC Septemba 12

Kupitia mkutano huo, Ofisa Habari wa Yanga SC, Ali Kamwe naye amesema: “Leo tunatoa ratiba ya wiki ya mwananchi. Jambo lolote ambalo litafanywa na mashabiki, au wanachama wetu kutoka maeneo mbalimbali. Kinachofanyika Mbagala au Tegeta, linapaswa kufanywa na wanachama wetu waliopo Tokyo, Lubumbashi, Pretoria, New York na Mombasa. Kesho Jumanne tutakuwa na zoezi la kuchangia damu.

“Hii ni sehemu ya matukio yetu ya wiki ya wananchi. Kituo chetu kikuu ni Makao makuu ya Klabu yetu Jangwani. Lakini tunawaomba wanachama wetu kuchangia damu katika hospital iliyopo karibu nawe. Kuna thamani kubwa sana ya chupa yako ya damu katika kuokoa maisha.

“Watu watakaochangia damu watapewa zawadi mbalimbali kutoka kwa wadhamini wetu. Baada ya kuchangisha damu tutapata supu kama kawaida yetu. Tunapata supu huku tukijadiliana namna tutakwenda kilele cha wiki ya mwananchi tukiwa na vibe.

“Jumatano tutakuwa na DUA maalumu. Lakini tunatamani kila mkoa mwanachama wa Yanga kwa imani tofauti tofauti wanapaswa kufanya dua kwenye maeneo yao. Dua hiyo itapaswa kufanywa mchana, ili tumuombe Mungu baraka zake ili atujalie mafanikio tele. Kitaifa dua hii itafanyika makao makuu ya klabu. Wote mnakaribishwa.

“Alhamis tutakuwa na charity katika hospital ya Muhimbili. Wanayanga wanapaswa kufika hospitali hiyo tukiwa na mahitaji mbalimbali. Kwa wale ambao hawataweza kufika muhimbili basi wanapaswa kwenda kwenye vituo mbalimbali na kuwafikia wahitaji.

Mastaa wapya wanaosubiriwa kwa hamu kutambulishwa ndani ya Yanga Day ni:

Mohamed Doumbia

Alisaini kuitumikia Yanga SC ilimshusha staa huyu usiku wa Agosti 3, 2025. Doumbia ni ingizo jipya ndani ya kikosi cha Yanga SC 2025/26, ambapo nyota huyo mwenye umri wa miaka 26 amejiunga na Yanga SC akitokea FC Slovan Liberec ya Jamuhuri ya Czech.

Boyeli

MVP wa zamani wa Ligi Kuu ya Zambia, ambaye naye amejiunga na Wananchi kutokea Afrika Kusini. Alitambulishwa Julai 31, 2025. Staa huyo mwenyw umri wa miaa 24 alikuwa anacheza Sekhukhune United ya Afrika Kusini. Sasa nyota huyo atahudumu kwa mkopo wa mwaka mmoja na Wananchi.

Ecua Elastin

1/08/ 2025 uongozi wa Yanga ulimtambulisha Ecua kwa dili la miaka miwili. Ikumbukwe Msimu wa 2024/25 alikuwa anacheza Zoman FC, ambapo alifunga magoli 15 na pasi 12 za magoli.

Balla Conte

Huyu ndiye staa ambaye usajili wake ulikuwa na mvutano mkubwa, hii ni baada ya kuelezwa kuwa alikuwa anatajwa kuwa kwenye rada za Simba SC na Yanga SC. Julai 18, 2025 Yanga SC ilimtambulusha Moussa Balla Conte. Ingizo hili jipya ni kutoka CS Sfaxien ya Tunisia yeye ni raia wa Guinea.

Mastaa wengine ambao watatambulishwa Yanga Day ni Pamoja na Offen Chikola, Casemiro, Ninju na kocha wao Roman Folz.

Hitimisho: Zuchu kuiteka shoo

Yanga SC vs Bandari FC Septemba 12
Zuchu

Ukiachana na mechi ya Yanga SC vs Bandari FC Septemba 12, miongoni mwa matukio yanayosubiriwa kwa hamu ni shoo ya Zuchu. Hii ni baada ya kutambulishwa rasmi siku ya jana Jumapili. Ikumbukwe Zuchu ana hitsong nyingi ikiwemo ‘Amanda’ na Sukari ulio na zaidi ya watazamaji milioni 100 kwenye jukwaa la You Tube pekee. Hivyo hili linatarajiwa kuwa tukio la kihistoria.

SOMA HII PIA: Yanga SC yamsajili Frank Assinki kutoka Ghana kwa mkopo | Usajili Ligi Kuu ya NBC 2025/26

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.