- John Bocco mfungaji wa muda wote akifunga magoli zaidi ya 110 atapewa tuzo siku ya kilele cha Simba Day.
- Gor Mahia ya Kenya kucheza na Simba SC mchezo wa kirafiki Uwanja wa Mkapa, Dar Septemba 10 2025.
- Jonas Mkude alidumu Simba SC kwa muda mrefu ni timu mbili kubwa amecheza Bongo.
Mfungaji bora wa muda wote John Bocco na kiungo wa kazi Jonas Mkude wanatarajiwa kupewa tuzo za heshima kilele cha Simba Day. Ni Septemba 10 2025 tamasha hilo kubwa linatarajiwa kufanyika. Sababu kubwa za wachezaji hao kupewa tuzo hizo ni kuheshimu mchango ambao wameutoa ndani ya Simba SC.
Muda wa kuvuna mamilioni ukipaisha Kindege cha SportPesa
Rubani wikiendi haipoi kwa kuwa kuna mamilioni yanakusubiri sasa hivi. Ni rahisi mno, unachotakiwa kufanya ni kupaisha Kidege cha SportPesa. Cheza Aviator upate mgao wako.

Mfungaji bora wa muda wote John Bocco na kiungo Jonas Mkude
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano, Simba SC ameweka wazi kuwa kuna utaratibu wakutambua mchango wa wachezaji. Kutokana na kila mchezaji kuwa na umuhimu wake watamfikia mmojammoja. Ni nahodha John Bocco na kiungo mkabaji Jonas Mkude hawa watapewa tuzo za heshima.

Soma hii: Simba Day 2025 msimu wa 17 viwango vingine
“Mwaka huu kwenye Simba Day tutawaalika na kuwatunza wachezaji wa zamani ambao wamefanya makubwa na tutawapa tuzo ya heshima. Wachezaji hawa ni John Bocco lakini vile vile tutakwenda kumuaga nahodha wetu mwingine ambaye ameitumikia Simba SC kwa miaka 15, Jonas Gellard Mkude.
“Tutaendelea kuwaaga malengendary wetu taratibu taratibu tutakapopata nafasi. Hii inatokana na ukubwa wa Simba SC na mchango mkubwa waliofanya. John Bocco yeye ameamua kustaafu na tumeongea naye amekubali.
“Ukimzungumzia Bocco, akiwa na Simba SC alitwaa mataji manne ya ligi. Hii ni heshima kubwa. Alikuwa ni nahodha mwenye nidhamu na juhudi katika kuipambania nembo ya Simba SC.
“Mkude aliondoka Simba SC alienda kupata malisho mengine. Hatukupata muda wa kumuaga tayari hatakuwa ndani ya timu aliyokuwa anacheza. Tunathamini mchango wa kila mmoja ndani ya Simba SC.
John Bocco mfungaji bora wa muda wote

Soma hii: Simba Day Septemba 10 2025
John Bocco mfungaji bora wa muda wote alisajiliwa na Simba SC 2017 akitokea Azam FC. Akiwa ndani ya Simba SC alikuwa ni nahodha na mfungaji bora wa muda wote ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo ni namba nne kwa ubora. Bocco anashikilia rekodi ya kuwa mzawa aliyefunga mabao zaidi ya 110 rekodi aliyonayo yeye mwenyewe.
Akiwa na uzi wa Simba SC alikuwa miongoni mwa wachezaji waliotinga hatua ya robo fainali kwenye mashindano ya CAF. Alitwaa tuzo ya ufungaji bora 2020/21 alipofunga jumla ya mabao 16 ndani ya ligi akiwa na uzi wa Simba SC. Hiyo ilikuwa ni baada ya mechi 34. Baada ya mkataba wake kuisha Simba SC, 2024/25 alitambulishwa JKT Tanzania.
Kuhusu Jonas Mkude
Jonas Mkude alikuwa na Simba SC akiwa kijana mdogo. Ni timu mbili kubwa amecheza za ushindani Simba SC alipodumu miaka 15 na Yanga SC alipodumu kwa misimu miwili. Jina lake maarufu ni nungunungu. Mguu wake wenye nguvu akiwa uwanjani ni ule wa kushoto.
Mkude Agosti 9 2022 kwenye Simba Day ya 12 alikuwa yupo kwenye kikosi cha Simba SC. Hii inamaanisha kuwa tangu Simba Day ya kwanza Mkude alikuwa na uzi wa Simba SC. Septemba 10 2025 itakuwa ni Simba Day ya 17, Mkude anayevaa jezi namba 20 atapewa tuzo ya heshima.
Hii hapa ratiba ya Simba Day 2025
Ahmed Ally alibainisha kuhusu ratiba ya Simba SC kuelekea Simba Day ambapo wataanza na uzinduzi wa wiki ya Simba Day. Agosti 2025 msafara wa Simba ulitia timu Mafinga. Uzinduzi rasmi wa Wiki ya Simba ni Agosti 31, 2025 kwenye viwanja vya Mafinga vilivyopo Mafinga Mjini.
“Septemba 2, 2025 ni siku ya kitaifa ya Wanasimba kuchangia damu kwenye hospitali mbalimbali. Tuna wajibu wa kusaidia kuokoa maisha ya Watanzania wenzetu. Hapa Dar es Salaam tutakuwa na vituo mbalimbali vya kutolea damu.
“Septemba 3, 2025 kutakuwa na droo ya bonanza. Mwaka jana mmnakumbuka tulikuwa na bonanza lilishirikisha matawi. Na mwaka huu tutarudisha tena na linahusisha matawi yote ya Simba Sports Club. Matawi yote ambayo yanataka kushiriki tutawapa namba ya kutuma jina lenu kushiriki. Tunafanya hivi ili kutengeneza umoja na upendo kwenye matawi ya Simba.
“Septemba 4, 2025 ni siku ya matawi, tunafahamu yapo matawi mengi yanahitaji kuzinduliwa. Tayari tuna matawi mawili hapa. Kama kuna mwingine amekamilisha utaratibu wote awasiliane na mkurugenzi wa Wanachama wa Simba.”
“Septemba 5, 2025 itakuwa ni biryan day. Tutakwenda kupata lunch kwenye kituo cha watoto yatima ambacho tutakichagua na kukitangaza, tutawapa taarifa. Tunafanya hivi kurudisha kwa jamii lakini pia kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu. Ukikaa na watoto wale yatima mkagonga biryan watoto wanafurahi wanaomba dua na Simba tunaneemika. Tarehe 5 njoo na njaa yako utashiba kwenye biryan la Simba Sports Club.
“Septemba 6, 2025 kutakuwa na bonanza tutafanyia kwenye viwanja vya Mwembe Yanga. Septemba 7, 2025 itakuwa Simba Day Fun Run hii itakuwa siku maalumu. Baada ya kufanya bonanza itakuwa ni malaumu Wanasimba kukimbia au ukiamua hata kutembea. Mbio zetu zitaanzia round about ya Agha Khan, tutapita daraja la Tanzanite, tutapita Coco Beach hadi Sea Cliff alafu tutarudi Coco Beach. Kiingilio pekee ni jezi yako mpya ya msimu huu.

Soma hii: Kikosi cha Simba SC kurejea Tanzania leo Agosti 28, 2025 usiku
“Septemba 8, 2025 tutarudisha kwa jamii tukiwa na timu nzima kuanzia wachezaji, makocha na viongozi wa Simba SC tutakwenda kutoa msaada kwenye kituo pendekezwa cha watoto yatima. Septemba 9, 2025 itakuwa kufanya mazoezi, kuongea na waandishi wa habari kuelekea Simba Day. Niwambie tu hii ni Simba Day ya 17 ni viwango vingine.
Hitimisho
Agosti 29 2025 wachezaji na msafara uliokuwa Misri kwa kambi umerejea Dar. Tayari kwa maandalizi kuelekea Septemba 10 2025 kilele cha Simba Day.Mchezo wao wa kimataifa wa kirafiki itakuwa dhidi ya Gor Mahia ya Kenya.


