- Yanga 2-0 Simba SC ilikuwa ni matokeo ya mwisho wababe hawa wanakutana kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2024/25.
- Kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii nusu fainali Agosti 8 2024, Yanga SC 1-0 Simba SC.
- Septemba 16 kivumbi na jasho kwa wababe hawa Kariakoo Dabi, Uwanja wa Mkapa.
Watani wa Jadi, Yanga SC na Simba SC Septemba 16 2025 watakuwa vitani Uwanja wa Mkapa. Ngwe hiyo ya wababe hawa ni maalumu kwa ufunguzi wa msimu mpya wa 2025/26. Itakuwa ni kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii (Community Shield).
Paisha kindege ushinde mamilioni na SportPesa
Nguvu ipo yakutosha kwako rubani na unaongezewa nyingine. Ukiwa hewani unavuna mamilioni. Muda ni sasa cheza Aviator upate mgao wako.

Ngao ya Jamii mchezo mmoja pekee

Soma hii:Yanga SC 2-0 Simba SC mchezo wa Kariakoo Dabi
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limethibitisha kuwa mwaka huu, Ngao ya Jamii itachezwa kwa mchezo mmoja pekee. Haya yote ni kufuatia mabadiliko ya kanuni yaliyopitishwa na Kamati ya Utendaji. Awali, mashindano haya yalikuwa yakihusisha nusu fainali mbili na kisha fainali.
Mabadiliko hayo yamesababishwa na ugumu wa ratiba, ikiwemo Tanzania kuwa mwenyeji wa Fainali za CHAN zitakazomalizika Agosti 30. Kuna mechi mbili za mchujo za Kombe la Dunia zinazoikabili Taifa Stars mapema Septemba. Mara baada ya Ngao ya Jamii, vilabu vya Tanzania vitakuwa kazini kwa michezo ya raundi ya awali ya mashindano ya CAF.
Yanga SC walivyotwaa Ngao ya Jamii

Soma hii: Yanga SC vs Simba SC vita ya ubingwa bado inaendelea
Yanga SC walitwaa taji hilo mwanzo wa msimu wa 2024/25. Mchezo wa fainali ilichezwa Agosti 11 2024 Uwanja wa Mkapa. Baada ya dakika90 ubao ulisoma Yanga SC 4-1 Azam FC.
Ni mabao 5 yalifungwa kwenye fainali huku kila bao likitoka kwa mfungaji mmojammoja. Fainali hiyo ilikuwa yakukata na shoka. Azam FC walikuwa wakipambana kufungua kabati kutwaa taji ambalo Yanga SC walikomalia.
Bao pekee la Azam FC lilifungwa na Feisal Salum. Mwanzo kabisa kipindi cha kwanza dakika ya 13 bao hilo lilifungwa likiwa ni pekee kwa Azam FC. Lilidumu kwa dakika tano pekee.
Yanga SC ikiwa chini ya Miguel Gamondi ilipata bao kupitia kwa Prince Dube. Nyota huyo aliwahi kucheza Azam FC alifunga dakika ya 18. Chadrack Boka alifunga dakika ya 27, Aziz Ki dakika ya 30. Msumari wa mwisho ni kazi ya Clement Mzize dakika ya 90.
Simba SC iliishia kwenye Ngao ya Jamii
Simba SC ilianza msimu wa 2024/25 bila taji. Katika Ngao ya Jamii iliishia nafasi ya tatu. Nafasi ya pili ilikuwa mikononi mwa Azam FC na ile ya nne ni Coastal Union.
Kwenye mchezo wa kusaka mshindi wa tatu bao pekee la ushindi kwa Simba SC lilifungwa na Saleh Karabaka. Dakika ya 10 Uwanja wa Mkapa bao hilo lilifungwa na lilidumu mpaka mwisho wa mchezo. Ndani ya dakika 80 Coastal Union walikwama kupata bao mbele ya Simba SC.
Nusu fainali Kariakoo Dabi Simba SC walipoteza
Simba SC itaingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu mbaya mbele ya Yanga SC. Kwenye mchezo wa nusu fainali ufunguzi wa 2024/25 ilipoteza. Mchezo huo ulichezwa Agosti 8 2024.
Yanga SC 1-0 Simba SC ilikuwa. Jitihada za kupata ushindi mbele ya watani zao wa jadi mwanzo wa msimu ziligonga mwamba. Wakati huo timu ilikuwa chini ya Kocha Mkuu, Fadlu Davids ambaye yupo na timu mpaka sasa.
Ni Maxi Nzengeli alikuwa mfungaji wa bao la ushindi kwa Yanga SC. Dakika ya 44 alipachika bao hilo Uwanja wa Mkapa. Mpaka zinagota dakika 90 Simba SC ilikwama kupata bao na kupoteza nafasi kutinga hatua ya fainali.
Itakumbukwa kwamba kwenye mechi mbili za Ngao ya Jamii ni bao moja Simba SC ilifunga. Ndani ya dakika 180 safu ya ushambuliaji iliyokuwa na Steven Mukwala, Mashaka, Jean Ahoua ilikuwa haijawa imara kwenye kucheka na nyavu. Septemba 16 2025 inatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
H2h Yanga SC vs Simba SC 2024/25

Msimu wa 2024/25 Simba SC haikuwa na bahati kwenye mechi za ligi. Katika dakika 180 walizokutana nje ndani ilipoteza. Yanga SC walikuwa wababe mbele ya Simba SC.
Ndani ya dakika 180 Yanga SC ilivuna pointi sita.Kwenye mechi 30 ambazo Simba SC ilipoteza ilikuwa mbele ya Yanga SC. Mzunguko wa kwanza ilikuwa Simba SC 0-1 Yanga SC. Mchezo wa mwisho uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Yanga SC ilishinda mabao 2-0 ikitangazwa kubwa bingwa wa ligi.
Hitimisho
Kariakoo Dabi ni mchezo mkubwa Afrika ambao unasubiriwa kwa shauku kubwa. Simba SC haina bahati mbele ya Yanga SC kwa hivi karibuni. Hivyo Septemba 16 2025 itaamua nani ataanza kwa kicheko.


