Luoga Mshindi Mid Week JackpotLuoga Mshindi Mid Week Jackpot
  • SportPesa mshindi mid-week jackpot milioni 367 asepa na kitita cha milioni 367 za ushindi.
  • Romanus Patrick Luoga kutokea Mbeya ambaye ni mkulima, ndiye amefanikiwa kuondoka na mzigo wa mamilioni.
  • Hii ni baada ya kufanikiwa kubashiri kwa usahihi mechi zote 13.

Dar es Salaam, Kampuni inayoongoza ya michezo ya kubashiri na burudani, SportPesa imeendelea kutoa tabasamu kwa wateja wake. Hii ni baada ya Julai 28, mwaka huu kumpata rasmi mshindi wa Mid-Week Jackpot. Mshindi huyo ni Romanus Patrick Luoga ambaye anajishughulisha na kilimo jijini Mbeya. Luoga ameibuka na ushindi huo, mara baada ya kubashiri kwa usahihi mechi zote 13.

Paisha ‘Kindege’ cha Sportpesa ushinde mamilioni sasa

Wakati ukiendelea kuhabarika na makala hii, kumbuka unaweza kushinda mamilioni muda huu. Cheza sasa mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kupitia Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa bonyeza picha hii chini.

SEO Banner LV

Mshindi anasemaje?

Akizungumza mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi, Luoga amesema: “Nimekuwa nikicheza na SportPesa kwa zaidi ya miaka nane sasa. Niliifahamu kampuni hii kwa mara ya kwanza nikiwa Mwanza, lakini sijawahi kupata ushindi mkubwa kama huu. Nimewahi kushinda zaidi ya Milioni mara kadhaa.

“Ushindi huu niliokuwa naupata ulizidi kunihamasisha kuendelea kubashiri kwa kuwa nafasi ya kushinda ni kubwa. Mara nyingi nilikuwa nikitumia muda mwingi kuchambua matokeo ya mechi kabla ya kuweka ubashiri wangu. Na kwakuwa nafanya uchambuzi kwa makini, imenisaidia kuwa kwenye nafasi nzuri ya kushinda.

“Nakumbuka ushindi wangu wa kwanza mkubwa ulikuwa Shilingi Laki 6. Baada ya kushinda fedha hizo nilienda kununua simu janja, ili kuweza kunisaidia kubashiri zaidi. Simu janja imenisaidia kufanya uchambuzi wangu wa mikeka vizuri, na kwa usahihi zaidi.”

Ushindi huu ataufanyia nini?

Luoga alipokutana na mastaa wa Yanga
Luoga alipokutana na mastaa wa Yanga

Ushindi huu utanisaidia kutimiza malengo yangu ya kukuza shughuli zangu za kilimo, lakini pia kwenye shughuli za ujenzi. Naikubali sana SportPesa kwa kunipa nafasi ya kubadilisha maisha yangu, hii ndiyo kampuni inayoaminika zaidi hapa Tanzania. Hawana longolongo, ukishinda unapewa fedha zako.”

SOMA HII PIA: SportPesa watoa shilingi Bilioni 1.028 wiki hii kwa washindi wa bonasi ya SupaJackpot huku Mshindi wa Jackpot akiondoka na Sh.265,780,681.

Bosi SportPesa naye afunguka

Luoga Mshindi Mid Week Jackpot
Luoga Mshindi Mid Week Jackpot akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi SportPesa Tanzania

Kufuatia ushindi huo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa SportPesa, Tarimba Abbas naye amesema: “Bwana Luoga mkazi wa Mbeya tarehe 28 Julai mwaka huu, amefanikiwa kushinda Jackpot yetu ya katikati ya wiki. Kufuatia ubashiri huo amejishindia Milioni 367. Huyu ni mmoja wa wachezaji wetu wazuri kutoka Mbeya.

“Ikumbukwe mpaka sasa takribani watu 16 wamefanikiwa kujishindia Jackpot mbalimbali. Hii ni namba ya ushindi mkubwa zaidi katika makampuni ya kubeti. Kwanini SportPesa tunapata washindi wengi wa Jackpot? Hii ni kwa sababu huwa tunaweka mechi ambazo si kali sana.

“Kama mnakumbuka tumewahi kupata mshindi wa Bilioni 1, ikiwa ni Kampuni ya kwanza Tanzania kufikia mafanikio hayo. Kwa niaba ya SportPesa, tunayo furaha kumpongeza Bw. Romanus Luoga kwa ushindi huu mkubwa wa Mid-Week Jackpot. Ushindi huu ni uthibitisho wa dhamira yetu ya kuleta fursa za kipekee kwa wateja wetu, ili kubadilisha maisha yao kupitia michezo yetu.

“Ni matumaini yetu kuwa zawadi hii itakuwa mwanzo mzuri wa masiha mapya na nafuu ya kiuchumi kwake. Lakini pia ushindi huu unaifaidisha Serikali kwani asilimia 12 ya ushindi ni kodi anayokatwa mshindi. Lakini mnafahamu kuwa asilimia 25 ya fedha yote ya washiriki baada ya ushindi, Kampuni yetu inachangia Serikali hivyo kuchangia maendeleo.”

SOMA HII PIA: Milioni 18,004,468 za Jackpot ya SportPesa zaenda Ruvuma.

Mkuu Kitengo cha Masoko ahimiza wengine kushiriki

SportPesa mshindi mid-week jackpot milioni 367
Luoga na mastaa Yanga

Naye Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa SportPesa, Tracy Humplick, aliongeza: “Tangu kuanzishwa kwetu, SportPesa imefanikiwa kutangaza washindi 16 wa Mid-Week Jackpot na kulipa zaidi ya TZS 5 Bilioni. Tuna furaha kumsherehekea Luoga kama mshindi wetu wa 16. Tunawahakikishia pia wateja wetu kwamba ushindi upo na kila mmoja ana nafasi ya kushinda”

SOMA HII PIA: Jumanne Aibuka Mshindi wa Bonus ya SportPesa…TZS 8,154,788

Hitimisho

Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa SportPesa, Tracy Humplick aliendelea kueleza, juu ya utaratibu wote wa mshindi kupokea zawadi yake. Hii ni katika kutoa fursa kwa wote wanaotaka kufuatilia mchakato wa makabidhiano na kujiridhisha kuwa wanaweza kufuatilia kupitia akaunti rasmi za SportPesa.

“Kwa taarifa zaidi kuhusu bidhaa, na kuona jinsi mshindi wetu alivyokabidhiwa zawadi yake, tembelea kurasa zetu rasmi za mitandao ya kijamii na tovuti ya SportPesa,” amesema Tracy.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.