- Simba Day 2025/26 inatarajiwa kufanyika Septemba 10 ikiwa inamaanisha pazi la msimu mpya linakwenda kuanza.
- Wachezaji wapya watatambulishwa kwa mashabiki na wale waliokuwa katika kikosi kwa msimu wa 2024/25 chini ya benchi la ufundi linaloongozwa na Fadlu Davids.
- Ubaya Ubwela unasubiriwa huku King Kiba akitarajiwa kutoa burudani kwenye tamasha hilo kubwa Afrika.
Tamasha la utambulisho wa wachezaji na benchi la ufundi kwa Simba SC maarufu kwa jina la Simba Day ni Septemba 10 2025. Ni moja ya tamasha kubwa la michezo Afrika. Linatarajiwa kufanyika katika Uwanja wa Mkapa.
Rubani bingwa vuna mamilioni sasa hivi
Ni muda wakuvuna mamilioni sasa hivi ukipaisha kindege cha SportPesa. Ushindi ni kwa ajili yako unakusubiri. Cheza Aviator upate mgao wako.

Malengo ya Simba Day

Soma hii: Baada ya Rushine Simba yamshusha Allasane Kante huyu hapa: Tetesi usajili Ligi Kuu NBC 2025/26
Historia inasema kuwa mwanzo lengo kubwa ilikuwa ni kupata fedha za usajili na gharama nyingine. Muasisis wa tamasha hilo wakati ule ni Hassan Dalali ambaye alikuwa ni mwenyekiti. Tarehe rasmi ilikuwa ni Agosti 8 sikukuu ya wakulima.
Kutokana na mabadiliko ya ratiba kila msimu, siku hiyo nayo imekuwa ikibadilika. Wachezaji wapya wamekuwa wakitambulishwa na benchi la ufundi. Katika tamasha hilo malengo ya msimu mzima huwekwa hadharani mbele ya mashabiki ambao hujitokeza kwa wingi.
Mbali na utambulisho huwa kunakuwa na burudani mbalimbali. Wasanii hufanya maonyesho yao ya kuimba na kucheza. Miongoni mwa wanaotarajiwa kuwa katika tamasha hilo ni Ali Kiba, King Kiba ambaye wimbo wa Mnyama ulioachiwa Agosti 2 2023 bado unaishi.
Orodha ya wachezaji wapya watakaotambulishwa hii hapa
Rushine

Rushine De Reuck ni mchezaji wa kwanza kutambulishwa ndani ya Simba SC. Haya ni maandalizi kuelekea Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2025/26. Huyu ni beki alitambulishwa Julai 29 2025. Beki huyu yupo nchini Misri ambapo timu hiyo imeweka kambi.
Kante
Nyota Alassane Kante ambaye ni kiungo alikuwa anacheza CA Bizertin ya Tunisia. Atakuwa ndani ya Simba SC msimu wa 2025/26. Alitambulishwa Julai 30 2025.
Morice
Morice Abraham alitambulishwa ndani ya Simba SC Julai 31 2025. Nyota huyo amesema kuwa kuna kazi kubwa yakufanya katika changamoto mpya. Yupo kambini Misri kwa maandalizi ya msimu mpya.
Semfuko
Hussein Daudi Semfuko alitambulishwa Simba SC, Julai 31 2025 kuwa ni mali ya Simba SC. 2024/25 alikuwa akicheza Coastal Union ya Tanga. Atakuwa kwenye changamoto mpya.
Sowah
Jonathan Sowah alitambulishwa Simba SC, Agosti Mosi 2025. Msimu wa 2024/25 alikuwa Singida Black Stars alifunga mabao 13.
Bajaber
Agosti 2 2025 Simba SC ilimtambulisha Mohamed Bajaber. Kiungo mshambuliaji alikuwa anacheza Polisi ya Kenya. Nyota huyu ana uwezo wakufunga na kutengeneza nafasi za kufunga ndani ya uwanja.
Mligo
Antony Mligo beki wa kushoto alitambulishwa ndani ya Simba SC Agosti 5 2025 alikuwa Namungo FC. Kandarasi ya miaka mitatu. Beki huyo ni mrithi wa mikoba ya Mohamed Hussen Zimbwe Jr ambaye yupo ndani ya kikosi cha Yanga SC.
Camara
Ni Naby Camara alitambulishwa rasmi kuwa nyekundu na nyeupe Agosti 14 2025. Nyota huyo aliwahi kucheza Klabu ya Al Waab ya Qatar na CS Sfaxien.
Camara ana umri wa miaka 23 ana uwezo wa kucheza nafasi ya kiungo wa kati na beki wa kushoto. Anasajiliwa ili kuongeza nguvu kwenye upande wa kushoto wa ulinzi, nafasi iliyoachwa wazi na Mohammed Hussein Zimbwe Jr, ambaye amejiunga na watani wa jadi, Yanga SC.
Camara aliwahi kuichezea Klabu ya CS Sfaxien ya Tunisi. Msimu uliopita alikuwa akiitumikia Al-Waab Sporting Club ya nchini Qatar. Kwa sasa ni Mnyama yupo kambini nchini Misri.
Kaulimbiu Ubaya Ubwela ilikimbiza 2024/25
Msemo wa Ubaya Ubwela ulikimbiza kwa msimu wa 2024/25. Ulikuwa unatumika na Simba SC kwenye matamasha na hata mechi. Ilikuwa ni kaulimbiu pendwa kwa Simba SC hivyo kwa sasa itakuwa inawapasua kichwa waje na kaulimbiu ipi itakayobamba.
Ambacho kinasubiriwa kwa msimu mpya kutakuwa na kipi kipya? Ahmed Ally ambaye ni Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano kitengo chake kinasubiriwa. Pengine inaweza kuwa ni mwendelezo wa hii ama kuja na nyingine mpya.
Nahodha mpya kujulikana

Soma hii: Simba SC inasukwa upya kuelekea 2025/26
Kwa wakati huu bado nahodha mkuu wa Simba SC hajajulikana. Ikumbukwe kwamba awali alikuwa ni Mohamed Hussen Zimbwe Jr. Beki huyo wa kushoto kwa sasa ni mali ya Yanga SC.
Shomari Kapombe ambaye ni beki wa kulia anapewa chapuo kuwa huenda akapewa kitambaa. Hivyo mbivu na mbichi zitajulikana Septemba 10 2025. Mbali na Kapombe Mzamiru Yassin jina lake linatajwa pia.
Hitimisho
Kikosi cha Simba SC kwa sasa kipo nchini Misri chini ya Kocha Mkuu, Fadlu Davids kwa maandalizi ya msimu mpya. Kinatarajiwa kurejea mapema Tanzania kwa ajili ya Simba Day. Tamasha hilo linasubiriwa kwa shauku na familia ya michezo.


