Feisal Tuzo CHANFeisal Tuzo CHAN
  • Central African yaibana mbavu Tanzania kwenye mchezo wa CHAN 2024 kwa kugawana pointi mojamoja Uwanja wa Mkapa usiku.
  • Feisal Salum kiungo wa Tanzania nyota yake imezidi kumeta kutokana na uwezo wake uwanjani kwenye kutimiza majukumu.
  • Tanzania imetinga hatua ya robo fainali bila kupoteza mchezo ndani ya CHAN 2024.

Central African 0-0 Tanzania ni matokeo yakushangaza kwenye mchezo wa CHAN 2024 uliochezwa Uwanja wa Mkapa. Katika mchezo huo, Tanzania ilikuwa inapewa nafasi kupata matokeo mwisho ikagawana pointi mojamoja. Unakuwa ni mchezo wa kwanza kwa Central African kuvuna pointi moja katika kundi B.

Unasubiri nini? Vuna mamilioni sasa hivi

Kuna jambo umekwama kwa sasa kuhusu mkwanja? Usiogope, rubani ni jasiri na kazi yake ni kupaisha kindege cha SportPesa. Cheza sasa hivi Aviator uvune mamilioni.

SEO Banner LV

Huyu hapa Kocha Mkuu wa Tanzania Hemed Suleman

Hemed Suleman, Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania amesema watafanyia kazi makosa yaliyopita kuwa imara zaidi. Tanzania Agosti 16 2025 mchezo wa CHAN 2024 ilikwama kupata ushindi licha ya kutengeneza nafasi nyingi uwanjani.

“Nafikiri ilikuwa mechi nzuri. Tangu mwanzo nilikuwa ninasema kwamba utakuwa mchezo mgumu.Ninawashukuru wachezaji wamepambana. Tutafanyia kazi makosa kuwa bora zaidi hatua ya robo fainali.

“Nafikiri katika makundi yote hakuna kundi jepesi. Makundi yote ni magumu. Ninaangalia makundi yote na acha tuangalie nani tunakwenda kukutana naye. Sisi tupo tayari kwa ajili ya timu yoyote na hata ukiangalia kwenye kundi letu nalo ni gumu,” amesema Suleman.

Huyu hapa Feisal mchezaji bora wa mchezo

Kiungo Feisal Salum nyota wa Tanzania aliyechaguliwa kuwa mchezaji bora amesema malengo yalikuwa kupata matokeo.Kwa kilichotokea ni sehemu ya mpira ndani ya uwanja. Aliongeza kuwa watakuwa imara katika mechi zijazo.

Mchezaji bora wa mechi
Mchezaji bora wa mechi Feisal.

Soma hii: Tanzania kuikabili Madagascar CHAN 2024

“Haikuwa shida tumeenda na game plan yetu ya kile ambacho tulifundishwa mazoezini. Ambacho wamefanya wapinzani wetu ni kuziba nafasi ambazo tulizifanyia mazoezi. Mimi mchezaji katika matokeo tuliyopata hatujaridhika.

“Tulitegemea matokeo kwenye mchezo wetu. Wenzetu walituheshimu na kuja kwa umakini. Mchezo huu umepita tunaangalia mechi zijazo za hatua ya robo fainali. Tunaamini tutapambana kufanya vizuri zaidi, “ amesema Fei Toto.

Kikosi cha Tanzania ambacho kilianza

Yakoub Suleiman, Lusajo Mwaikenda, Pascal Msindo, Ibrahim Hamad. Dickson Job ambaye ni nahodha,Yusuph Kagoma, Sheikhan Khamis. Ibrahim Ahmada, Ahmed Pipino, Feisal Salum, Sopu walianza kikosi cha kwanza.

Aishi Manula, Hussen Masalanga, Nassor Saadun, Jammy Jammy, Mohamed Hussen, Wilson Nangu, Shomari Kapombe. Elias Lamek, Vedastus Masinde, Abdulazak Hamza na Mishamo Michael walikuwa wachezaji wa akiba.

Mechi 7 Tanzania, ushindi 6, sare moja kwa Tanzania

 Eswatini 1-2 Tanzania, mchezo huu ulichezwa Juni 11 2025. Tanzania 1-0 Uganda ulichezwa Julai 22 2025. Tanzania 2-1 Senegal ulichezwa Julai 27 2025.

Tanzania 2-0 Burkina Faso ulichezwa Agosti 2 2025. Huu ulikuwa ni mchezo wa ufunguzi wa CHAN 2024 Uwanja wa Mkapa. Mauritania 0-1 Tanzania, Agosti 6 2025. Tanzania 2-1 Madagascar. Agosti 16 2025, Central African 0-0 Tanzania.

Kwenye mechi saba, safu ya ushambuliaji ya Tanzania ilifunga mabao 10. Ukuta wa Tanzania umeruhusu mabao matano. Kwenye dakika 630 kocha Hemed Suleman mipango yake ilijibu kwa wachezaji kutimiza majukumu kwa umakini bila kupoteza.

Safu ya ushambuliaji ina wastani wakufunga bao moja kila baada ya dakika 63. Safu ya ulinzi ina wastani wakufungwa bao moja kila baada ya dakika 126.

Huu hapa msimamo wa Kundi B

Timu ya taifa ya Tanzania inaongoza Kundi B na pointi 10 baada ya kucheza mechi 4. Madagascar nafasi ya pili ikiwa na pointi 7 baada ya kucheza mechi nne.Mauritania nafasi ya tatu ina pointi 7 baada ya mechi nne. Burkina Faso nafasi ya tatu ina pointi 3 baada ya kucheza mechi nne.

Cental African Republic nafasi ya tano. Ina pointi moja kibindoni. Inaburuza kundi ikiwa imevuna pointi moja kwa Tanzania.

Wafungaji wa magoli kwa Tanzania CHAN 2024

Mzize CAF
Mzize CAF

Soma hii: Tanzania 2-1 Madagascar Mzize afunga magoli mawili

Mfungaji wa goli la kwanza CHAN 2024 kwa Tanzania ni Abdul Sopu. Kiungo huyo alifunga goli hilo kwenye mchezo dhidi ya Burkina Faso. Ilikuwa ni Agosti 2 2025, Uwanja wa Mkapa.

Mfungaji wa goli la pili kwa Tanzania ni Mohamed Hussen Zimbwe Jr. Beki huyo wa kushoto alifunga kwenye mchezo dhidi ya Mauritania. Ilikuwa ni kwa pigo la kichwa Uwanja wa Mkapa.

Goli la tatu lilifungwa na Shomari Kapombe. Beki huyo alifunga kwenye mchezo dhidi ya Mauritania. Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa Mkapa, Agosti 6 2025.

Kapombe alipachika goli hilo akiwa ndani ya 18. Ilikuwa dakika ya 90 akitumia mguu wa kulia kupachika bao la ushindi. Alitumia pasi ya kiungo Idd Nado.

Clement Mzize amefunga mabao mawili kwenye mchezo dhidi ya Madagascar. Mzize ni mshambuliaji wa kwanza kufunga kwa wachezaji wa Tanzania. Ikumbukwe kwamba kwenye mchezo dhidi ya Burkina Faso penati alisababisha Mzize.

Matokeo ya Tanzania CHAN 2024

Agosti 2 2025, Tanzania 2-0 Burkina Faso. Mauritania 0-1 Tanzania. Tanzania 2-1 Madagascar, Agosti 9 2025. Agosti 16 Central African 0-0 Tanzania.

Washindi wa Tuzo za CHAN

Mchezo dhidi ya Burkina Faso ni Feisal Salum alichaguliwa kuwa mchezaji bora. Mchezo dhidi ya Mauritania ni Mudathir Yahya alichaguliwa. Mchezo dhidi ya Madagascar ni Clement Mzize amechaguliwa. Mchezo dhidi ya Central African ni Feisal alichaguliwa.

Hitimisho

Tanzania imefuzu rasmi hatua ya robo fainali. Kutoka kundi B timu mbili zimefuzu jumlajumla. Madagascar imekata tiketi pia kufuzu robo fainali huku Mauritania ikiambulia nafasi ya tatu.

image

Share this: