Ofa kubwa ya KihistoriaOfa kubwa ya Kihistoria
  • SportPesa yaipa Yanga SC Bilioni 21.7, huku historia ikiandikwa kwa ofa kubwa na ya kihistoria.
  • Ofa hii ni ya Mkataba mpya wa udhamini wa miaka 3.
  • Udhamini huu wa SportPesa utaifanya Yanga kuvuna zaidi ya Bilioni 7 kila mwaka.

Huku wakiendelea kutambia mafanikio makubwa ya msimu uliopita wa 2024/25. Uongozi wa Yanga SC umezidi kuneemeka, hii ni baada ya kufanikiwa kusaini mkataba mpya na uongozi wa Kampuni ya SportPesa kuendelea kuwa mdhamini mkuu. Mkataba huu mpya ni wa miaka 3 wenye thamani ya Shilingi Bilioni 21.7.

Shinda mamilioni ya kindege cha SportPesa kwa kubonyeza picha hii chini

Yanga SC wamevuna mabilioni ya SportPesa, nafasi ni yako cheza sasa ujishindie mamilioni ya kindege ‘Aviator’ kwa kubonyeza picha hii hapa chini.

SEO Banner LV

Uhusiano kati ya SportPesa na Yanga SC

Utiaji sahihi makubaliano
Utiaji sahihi makubaliano

Uongozi wa klabu ya Yanga SC umekuwa na mahusiano ya muda mrefu, wa takribani miaka 8 na Kampuni ya SportPesa. Ambapo SportPesa wamekuwa wadhamini wakuu wa Yanga kwa kipindi chote. Miaka hiyo 8 iliyopita, imegawanyika katika vipindi viwili. Mkataba wa kwanza wa SportPesa na Yanga ulikuwa wa miaka mitano, ambao ulimalizika mwaka 2022 ukiwa na thamani ya Bilioni 5.2.

SOMA HII PIA: Yanga SC kuitikisa Rwanda Pre-Season kuvaana na Rayon

Yanga yavuna Bilioni 17 kutoka SportPesa

Mwaka 2022, SporPesa na Yanga waliingia mkataba mwingine wa miaka mitatu wenye thamani ya Bilioni 12.33. Ambapo kila msimu Yanga wamekuwa wakivuna kiasi cha Shilingi Bilioni 4. Fedha hizi zimekuwa zikitumika kwa maendeleo ya timu hiyo. Katika kipindi cha miaka 8, Yanga wamevuna zaidi ya Bilioni 17.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi SportPesa Tanzania afichua kuhusu Ofa kubwa

Uongozi wa Yanga na SportPesa wakionyesha mikataba mipya
Uongozi wa Yanga na SportPesa wakionyesha mikataba mipya

Akizungumzia makubaliano hayo mapya Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya SportPesa Tanzania, Abbas Tarimba amesema: “Dhamira ya Sportpesa ilikuwa na ndoto kuingia kwenye mpira. Tuliwahi kudhamini Arsenal, Hully City, Everton na Ligi Kuu Kenya klabu kadhaa.

“Tulipotazama Tanzania tukabaini Yanga ni Klabu sahihi kutimiza nayo ndoto zetu. Yanga ina mashabiki wengi. Tuliwaamini sana viongozi wa Yanga kwamba tungeubadilisha mpira wa Tanzania. Baada ya sisi kuingia Yanga, tuliwapa nguvu ya kiuchumi.

“Yanga imekuwa na misuli ya kumsajili mchezaji kutoka klabu yoyote. Hii imefanya Yanga iwe na uwezo wa kumuuza mchezaji yoyote, kwa sababu ina uwezo wa kusajili mchezaji kokote. Tumesaini mkataba mpya wa miaka mitatu, mkataba huu una thamani ya Tshs bilion 21.7 ambapo utaifanya Yanga iwe na ndoto ya kuwa Bingwa wa AFRIKA. Nje ya udhamini huu, Sportpesa Tumeweka Bonasi Kubwa kwenye mechi za kimataifa.

“Watanzania wana matamanio makubwa ya kuleta kombe la Afrika. Kwa Uongozi huu sina mashaka kuwa hili linawezekana. Young Africans SC ina Wachezaji bora, kutoka kila kona la bara la Afrika. Niwatakie kila la kheri kwa msimu unaokuja na misimu mingine.”

SOMA HII PIA: Ali Kamwe: Kuna wachezaji wapya watatu kutambulishwa Yanga SC/ Zimbwe Jr usajili wa mkubwa

Rais wa Yanga SC, Hersi Said naye azungumzia ofa kubwa ya kihistoria

Kwa niaba ya uongozi wa Taasisi ya Yanga SC, Rais Hersi Said amesema naye amesema: “Kabla ujio wa Sportpesa Yanga ilikwama. Licha ya ukubwa na ukongwe wake, Yanga ilishindwa kupata wachezaji wazuri, Yanga ilishindwa hata kusafiri bila changamoto. Lakini leo hii Yanga inagombea wachezaji wazuri na klabu kubwa Afrika.

“Haya ni mafanikio makubwa sana kutokana na udhamini mkubwa kutoka kwa Sportpesa. Tunawapongeza sana Sportpesa kwa namna ambavyo wamekuwa bega kwa bega na sisi. Mkataba wetu na sportpesa, umekuwa mkataba wenye manufaa makubwa kwa pande zote. Tunayo furaha kubwa, kutangaza tumeongeza mkataba na mdhamini wetu mkuu Sportpesa kwa kipindi cha miaka mitatu.”

Ali Kamwe achombeza kuwapiga watu chenga ya mwili

SportPesa yaipa Yanga SC Bilioni 21.7
Ali Kamwe

Naye Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe alichombeza ishu ya kuwapiga watu chenga ya mwili kwa ofa kubwa ambapo amesema: “Tumeteka Taifa kwa vichwa vya habari. Tumetangaza kuwa tumepokea ofa na tumeikataa. Lakini baadaye tukatangaza tumepata ofa nyingine mpya kubwa na tumeikubali. Ofa hiyo ni udhamini mkubwa na wa kihistoria kutoka kwa mdhamini wetu mkuu Sportpesa.

“Haikuwa kazi rahisi, zilikuwepo kampuni nyingi, lakini ofay a SportPesa ndiyo ilikuwa bora zaidi. Kwanini SportPesa? Ni kwa sababu hii ni Kampuni ambayo haina longolongo, pia wanafanya mambo kwa kuzingatia taaluma. Lakini kubwa aidi tumepata mafanikio makubwa Pamoja.”

SOMA HII PIA: Usajili wa Yanga SC orodha ya wapya 11 msimu wa 2025/26 | Rekodi, magoli na timu walizotoka

Hitimisho: Naibu Waziri ‘Mwana FA’ aipongeza SportPesa

Akiiwakilisha Serikali, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’ amesema: “Niwapongeze Yanga na Sportpesa baada ya kudumu kama washirika kwa miaka nane. Mafanikio makubwa ya pande zote yametokana na ushirika huu ambao umekuwa na tija. Serikali inaendelea kutengeneza mazingira rafiki kwa wawekezaji ambayo wanayo dhamira ya kuingia kwenye mpira.”

Naibu waziri Mwana FA
Naibu waziri Mwana FA
Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.