- CHAN 2024 ni moto kwa kila mechi huku Kenya ikiushangaza ulimwengu wa mpira kwa kuvuna pointi tatu mbele ya Morocco wakiwa pungufu.
- Kenya imekata tiketi kufuzu hatua ya robo fainali ikiwa inaongoza kundi lenye timu ngumu na bora kila idara.
- Tanzania imetakata CHAN 2024 imefuzu robo fanali kwa ushindi kwenye mechi zake zote tatu mfululizo.
Kenya 1-0 Morocco ni matokeo yakushangaza yakimaanisha mpira una matokeo yasiyotarajiwa. Ni kwenye Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN 2024). Agosti 10 2025 pointi tatu zilibaki Kenya baada ya dakika 90.
Mamilioni yanakusubiri sasa hivi
Ushindi wamamilioni upo kwa ajili yako. Unachotakiwa kufanya ni kupaisha kindege upate mgao wako. Cheza Aviator sasa rubani makini hana mashaka ni kicheko tu.

Huyu hapa mfungaji wa goli la ushindi

Soma hii:Tanzania vs Burkina Faso na Kenya vs DR Congo: Wenyeji waanza kwa kishindo CHAN 2024.
Ryan Ogam dakika 42 ya mchezo. Goli hilo lilidumu mpaka mwisho wa mchezo. Licha ya Kenya kuwa pungufu kwa kuwa mchezaji mmoja alionyeshwa kadi nyekundu walikomaa mpaka mwisho.
Dakika 48 walifanya kazi kubwa wachezaji wa Kenya kulinda ushindi huo. Malengo hayo yalitimia kwa kuwa hawakuruhusu goli. Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa Kasarani ulikuwa na ushindani mkubwa.
Pointi hizo tatu zinawapa uhakika wa kutinga hatua ya robo fainali. Kwenye Kundi A, Kenya wanaongoza Kundi. Pointi zao kibindoni ni pointi 7.
Huu hapa msimamo kwa Kundi A

Soma hii: Tanzania vs Madagascar Agosti 9 2025 CHAN 2024
Kenya inaongoza Kundi baada ya mechi 3 imekusanya jumla ya alama 7. Angola ni nafasi ya pili ikiwa na pointi 4 kibindoni. Congo Dr ipo nafasi ya tatu ina pointi tatu.
Nafasi ya nne ni Morocco ikiwa na pointi tatu ilizokusanya. Ni mechi mbili imecheza ambazo ni dakika 180. Zambia inaburuza mkia baada ya mechi mbili haijakusanya pointi.
Zambia mchezo wake uliopita ilipoteza pointi tatu jumla. Baada ya dakika 90 ilikuwa Zambia 1-2 Angola. Hivyo katika pointi 4 za Angola, tatu ilivuna kwa Zambia.
Tanzania na Kenya ni kicheko CHAN 2024

Soma hii: Tanzania kuikabili Madagascar CHAN 2024
Timu mbili kwa sasa ni kicheko ikiwa ni uhakika kwenye hatua ya robo fainali. Tanzania ilipata ushindi kwenye mchezo wake wa tatu ikiwa Uwanja wa Mkapa. Katika mchezo uliopita walipata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Madagascar.
Magoli yaliyofungwa mchezo wa Uwanja wa Mkapa
Magoli yote ya Tanzania yalifungwa na Clement Mzize dakika ya 13 na 20. Mzize alifunga mabao yote mawili ndani ya dakika 6 akiandika rekodi yakishujaa. Mshambuliaji huyo yupo kwenye ubora wake kwenye mechi za ushindani.
Goli la Madagascar lilifungwa na Nantenaina Razafimahatana dakika ya 34. Ni goli la kwanza kwa Tanzania kufungwa. Katika mechi mbili mfululizo ambazo ni dakika 180 ukuta wa Tanzania ulikuwa haujaruhusu kufungwa.
Magoli yote matatu kwenye mchezo huo uliochezwa Agosti 9 2025 yalifungwa kipindi cha kwanza. Ni mchezo wa kwanza kukusanya mabao matatu ndani ya dakika 90 kwa mechi ambayo Tanzania ilicheza. Licha ya kuruhusu goli bado pointi zilibaki kwa Tanzania.
Harambee Stars na Taifa Stars hao robo fainali
Timu ya taifa ya Kenya maarufu kwa jina la Harambee Stars imekata tiketi robo fainali. Timu ya taifa ya Tanzania maarufu kama Taifa Stars imekata tiketi robo fainali. Timu hizi zote zinaongoza makundi yao.
Tanzania kwenye mwendo wa ushindi
Eswatini 1-2 Tanzania, mchezo huu ulichezwa Juni 11 2025. Tanzania 1-0 Uganda ulichezwa Julai 22 2025. Tanzania 2-1 Senegal ulichezwa Julai 27 2025.
Tanzania 2-0 Burkina Faso ulichezwa Agosti 2 2025. Huu ulikuwa ni mchezo wa ufunguzi wa CHAN 2024 Uwanja wa Mkapa. Mauritania 0-1 Tanzania, Agosti 6 2025. Tanzania 2-1 Madagascar.
Kwenye mechi sita, safu ya ushambuliaji ya Tanzania ilifunga mabao 10. Ukuta wa Tanzania umeruhusu mabao matano. Kwenye dakika 540 kocha Hemed Suleman mipango yake ilijibu kwa wachezaji kutimiza majukumu kwa umakini.
Safu ya ushambuliaji ina wastani wakufunga bao moja kila baada ya dakika 54. Safu ya ulinzi ina wastani wakufungwa bao moja kila baada ya dakika 108.
Kundi B lipo namna hii kwa sasa

Soma hii: Tanzania 2-1 Madagascar Mzize afunga magoli mawili
Timu ya taifa ya Tanzania inaongoza Kundi B na pointi 9 baada ya kucheza mechi 3. Mauritania nafasi ya pili ina pointi 4 baada ya mechi tatu. Burkina Faso nafasi ya tatu ina pointi 3 baada ya kucheza mechi tatu. Madagascar nafasi ya nne ikiwa na pointi moja baada ya kucheza mechi mbili.
Jamhuri ya Kati haijakusanya pointi baada ya kucheza mechi mbili. Mchezo wake wa leo Agosti 9 2025 ilipoteza pia. Hivyo ipo inaburuza Kundi.
Matokeo ya Tanzania CHAN 2024
Agosti 2 2025, Tanzania 2-0 Burkina Faso. Mauritania 0-1 Tanzania. Tanzania 2-1 Madagascar, Agosti 9 2025.
Tanzania kwenye mechi tatu haijapoteza. Mchezo dhidi ya Mauritania ilipata ushindi katika dakika za lalasalama. Imeandika rekodi ya kutinga hatua ya robo fainali ikiwa na mechi moja mkononi.
Hitimisho
CHAN 2024 inaandaliwa na mataifa matatu. Tanzania, Kenya na Uganda. Ni Agosti 2 michuano hii mikubwa ilianza na inatarajiwa kufika kikomo Agosti 30.


