- Timu ya taifa ya Tanzania ina kibarua cha kuikabili Madagascar kwenye mchezo wa CHAN 2024 hatua ya makundi huku joto la pointi tatu likizidi kupanda.
- Mohamed Hussen Zimbwe Jr na Shomari Kapombe kwenye mechi mbili zilizopita walikuwa na bahati kufunga mabao muhimu CHAN 2024.
- Kundi B Tanzania inaongoza ikiwa imetanguliza mguu mmoja kutinga hatua ya robo fainali inakabiliana na Madagascar iliyo nafasi ya tatu.
Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars leo Agosti 9 2025 inakibarua cha kusaka pointi tatu dhidi ya timu ya taifa ya Madagascar. Huu ni mchezo wa Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN 2024. Tanzania inaongoza Kundi B ikiwa na pointi 6 itakabiliana na Madagascar iliyo nafasi ya tatu ikiwa na pointi moja.
Wikiendi isiende kinyonge vuna mamilioni sasa hivi
Ni muda wakukataa unyonge kabisa wikiendi ukipaisha kindege cha SportPesa. Kuna mamilioni yanakusubiri hivyo cheza sasa Aviator. Mgao upo kila siku.

Mechi mbili kuchezwa Uwanja wa Mkapa

Soma hii: Tanzania vs Madagascar Agosti 9 2025 CHAN 2024
Mechi mbili za CHAN 2024 zinatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa. Itakuwa saa 2:00 usiku Tanzania vs Madagascar. Pia saa 11:00 jioni itakuwa ni kete ya pili kwa Jamhuri ya Afrika Kati dhidi ya Mauritania waliotoka kupoteza dhidi ya Tanzania, mchezo huu utachezwa Uwanja wa Mkapa pia.
Robo fainali yanukia kwa Tanzania
Ikiwa Tanzania itapata pointi tatu leo mbele ya Madagascar itakuwa na uhakika kutinga robo fainali. Kwenye mechi mbili ilipata ushindi na kukusanya pointi tatu. Hivyo pointi tatu za leo zinamaana kubwa kwa Tanzania. Tanzania inapewa nafasi kubwa kushinda licha ya kuwa mchezo wa mpira wa miguu huwa na matokeo yakushangaza.
Mashabiki kutoka pande zote wameitwa kujitokeza uwanjani. Cliford Ndimbo, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) amesema kila kitu kipo vizuri. Ndimbo ameongeza kuwa kila mmoja anatambua uwepo wa CHAN Tanzania na mashabiki wamekuwa wakijitokeza kwa wingi.
“Kuna jambo kubwa la Tanzania ambalo linaendelea kwa sasa. Agosti 9 2025 kwenye mchezo kati ya Tanzania vs Madagascar hili sio la kukosa. Mechi kubwa itachezwa Uwanja wa Mkapa.
“Mchezo wetu dhidi ya Madagascar ni muhimu kwa mashabiki kujitokeza kwa wingi. Uwepo wao utawafanya waone namna gani tunapata pointi tatu. Kwanza tumevuka rekodi kwenye CHAN kwa kuvuna pointi nyingi zaidi hivyo inamaanisha tupo vizuri.
“Mashabiki wanapokuwa wengi ile morali inazidi kuwa kubwa zaidi. Kwenye mchezo dhidi ya Mauritania kulikuwa kuna presha kwa nini hatupati goli na goli lilipofugwa kila mmoja alifurahi. Hii inamaanisha kwamba timu ya taifa ya Tanzania ipo kwenye mioyo yetu,” alisema Ndimbo.
Mechi tano zilizopita za Tanzania

Soma hii: Mauritania 0-1 Tanzania CHAN 2024
Eswatini 1-2 Tanzania, mchezo huu ulichezwa Juni 11 2025. Tanzania 1-0 Uganda ulichezwa Julai 22 2025. Tanzania 2-1 Senegal ulichezwa Julai 27 2025.
Tanzania 2-0 Burkina Faso ulichezwa Agosti 2 2025. Huu ulikuwa ni mchezo wa ufunguzi wa CHAN 2024 Uwanja wa Mkapa. Mauritania 0-1 Tanzania, Agosti 6 2025.
Kwenye mechi tano, safu ya ushambuliaji ya Tanzania ilifunga mabao 8. Ukuta wa Tanzania umeruhusu mabao manne. Kwenye dakika 450 Suleman mipango yake ilijibu kwa wachezaji kutimiza majukumu kwa umakini.
Safu ya ushambuliaji ina wastani wakufunga bao moja kila baada ya dakika 56. Safu ya ulinzi ina wastani wakufungwa bao moja kila baada ya dakika 112.
Hali ya Kundi B ilivyo kwa sasa
Timu ya taifa ya Tanzania inaongoza Kundi B na pointi 6, Burkina Faso iafuata nafasi ya pili ina pointi 3. Madagascar na Mauritania hawa kila timu ina pointi moja.
Jamhuri ya Kati haijakusanya pointi na mchezo ujao itacheza na Mauritania. Agosti 9 2025 Tanzania itakuwa uwanjani kusaka pointi dhidi ya Madagascar. Vinara hao wa Kundi watacheza mchezo huo saa 2:00 usiku Uwanja wa Mkapa.
Wafungaji wa magoli kwa Tanzania CHAN 2024

Soma hii: Tanzania vs Burkina Faso na Kenya vs DR Congo: Wenyeji waanza kwa kishindo CHAN 2024.
Mfungaji wa goli la kwanza CHAN 2024 kwa Tanzania ni Abdul Sopu. Kiungo huyo alifunga goli hilo kwenye mchezo dhidi ya Burkina Faso. Ilikuwa ni Agosti 2 2025, Uwanja wa Mkapa.
Mfungaji wa goli la pili kwa Tanzania ni Mohamed Hussen Zimbwe Jr. Beki huyo wa kushoto alifunga kwenye mchezo dhidi ya Mauritania. Ilikuwa ni kwa pigo la kichwa Uwanja wa Mkapa.
Goli la tatu lilifungwa na Shomari Kapombe. Beki huyo alifunga kwenye mchezo dhidi ya Mauritania. Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa Mkapa, Agosti 6 2025.
Kapombe alipachika goli hilo akiwa ndani ya 18. Ilikuwa dakika ya 90 akitumia mguu wa kulia kupachika bao la ushindi. Alitumia pasi ya kiungo Idd Nado.
Matokeo ya Tanzania CHAN 2024
Agosti 2 2025, Tanzania 2-0 Burkina Faso. Mauritania 0-1 Tanzania. Mechi mbili dakika 180 mabao matatu.
Tanzania kwenye mechi mbili haijapoteza. Mchezo dhidi ya Mauritania ilipata ushindi katika dakika za lalasalama. Imetanguliza mguu mmoja robo fainali CHAN.
Hitimisho
Kwenye upande wa vikosi hakutakuwa na mabadiliko makubwa kwa timu zote mbili. Upande wa Tanzania hueda Ahmed Pipino akakosekana alipata maumivu ya jicho mchezo uliopita. Shomari Kapombe na Mohamed Hussen wapo kamili.


