Mligo (-)Mligo (-)
  • Simba SC yatambulisha mchezaji mwingine mpya ambaye ni beki wa kushoto kutoka Namungo.
  • Usajili wake ndani ya kikosi cha Simba SC ulikuwa na mvutano mkubwa ambapo inatajwa wapo ambao waligomea jina lake kupitishwa.
  • Ana jukumu zito kubeba mikoba ya Mohamed Hussen Zimbwe Jr ambaye ni beki bora wa muda wote alipokuwa katika kikosi cha Simba SC upande wa kushoto.

Simba SC imemtambulisha beki wa kushoto Antony Mligo aliyekuwa ndani ya Namungo FC. Beki huyo ana kibarua cha kuvaa viatu vya Mohamed Hussen Zimbwe Jr ambaye ni beki bora wa muda wote upande wa kushoto. Zimbwe amewaaga Simba SC huku tetesi zikieleza kuwa huenda atatambulishwa Yanga SC.

Vuna mamilioni sasa hivi ukipaisha Kindege cha SportPesa

Ni sasa hivi unavuna mamilioni ukipaisha Kindege cha SportPesa. Ni rahisi sana hasa ukizingatia Marubani wapo makini. Cheza Aviator upate mgao wako.

SEO Banner LV

Inaelezwa kuwa Mligo ni chaguo la Kocha Mkuu wa Simba SC, Fadlu Davids ambaye amepewa jukumu la kusajili wachezaji. Kabla mchezaji huyo hajatambulishwa kulikuwa na sekeseke kuhusu usajili wake. Taarifa zinaeleza kuwa wapo waliokuwa wanahitaji beki huyo asajiliwe na wengine walikuwa wanahitaji beki mwingine.

Anthony (-)
Anthony beki mpya wa Simba SC msimu wa 2025/26 akitokea Namungo.

Soma hii: Simba SC yasajili mashine hizi mbili kwa mpigo, kuelekea Ligi Kuu ya NBC 2025/26

Beki ambaye alikuwa anatajwa kuhitajika na mabosi wengine anaitwa Miraj Mohamed maarufu kwa jina la Zambo Jr. Huyu ni nahodha wa Coastal Union. Inaelezwa kuwa alipewa mkataba asaini mwisho akaacha kwa kile kilichoelezwa kuwa ni maslahi yake.

Utambulisho wa beki Mligo

Utambulisho wa Mligo umefanyika Agosti 5 2025. Beki huyu ni mzawa mwenye uwezo wa kupanda na kushuka akiwa uwanjani. Agosti 4 2025 alituma ujumbe kuwashukuru mashabiki na viongozi wa Namungo FC kabla ya kutambulishwa Simba SC.

Beki mpya Simba SC aliwaaga mabosi Namungo FC

“Kwanza kabisa natoa shukrani zangu za dhati kwa wachezaji wenzangu kwa ushirikiano mzuri ndani pamoja na nje ya Uwanja. Tulikuwa pamoja na kupambana kwa hali na mali katika kila nyakati. Furaha na huzuni tulivuka pamoja tukiwa imara.

“Napenda kulishukuru benchi la ufundi, viongozi wa timu. Mashabiki na wapenzi wa Namungo FC kwa kuwa pamoja ndani ya mwaka mmoja tukiipambania nembo ya timu, pamoja na malengo ya timu iliyojiwekea katika msimu mzima. Asante.

“Inaniwia ugumu kuiaga familia niliyoishi nayo vizuri kwa upendo na amani wakati wote. Lakini sina jinsi kwenda kupata changamoto sehemu nyingine naamini tutakutana wakati mwingine. Nawatakia kila lenye kheri katika msimu ujao 2025/2026, asante.”

Huyu hapa aliyetajwa kukataliwa na Simba SC

Nahodha na beki wa pembeni wa Coastal Union, Miraji Mohammed ‘Zambo Jr’ ameibuka na kutamka kuwa ni yeye alichukua maamuzi ya kuachana na Simba SC. Zambo Jr amebainisha kuwa kuna mengi ambayo yapo hivyo hatazungumza yote. Taarifa hiyo alizungumza kwenye moja ya Chombo cha habari alipokuwa akihojiwa na Jembe FC kwa mujibu wa mchambuzi Hans Rafael.

 “Mimi ndio nimeamua kutoendelea na Simba SC ila watu wengi hawajui. lla nimeachana nao kwasababu ya maslahi yangu lakini pia kesho yangu. Kuna vitu havikukidhi ila sio kwamba kocha alinikataa bali viongozi kuna vitu havikwenda sawa. Kuna mambo mengi humo ndani ila nisingependa kutoa password za watu ila sitaki migogoro isiyo na faida ila kuna mengi ya ndani Watu wasioyajua.”

Huyu hapa Meneja wa Idara ya Habari Simba SC

Med Kicheko
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari Simba SC. Source: Simba SC.

Soma hii: Baada ya Rushine Simba yamshusha Allasane Kante huyu hapa: Tetesi usajili Ligi Kuu NBC 2025/26

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC ameweka wazi kuwa wanafanya usajili makini. Ally ameweka wazi kuwa kila kitu kipo kwenye mipango makini.Baada ya utambulisho wa Mligo ametamba kuwa ni beki wa kushoto mwenye uwezo mkubwa.

“Kwa upande wa Mligo huyu ni mbavu ya kushoto. Yenyewe imetua kwenye timu ya ndoto yake. Na timu yenyewe ni Simba SC.

“Usajili wa msimu huu ni makini kwelikweli. Tunatambua kuwa msimu uliopita hatukuwa na furaha hasa kwa kukosa makombe. Wanasimba msiishiwe pawa bado tupo imara.

“Benchi la ufundi lilifanya kazi kubwa msimu uliopita na sasa tunafanya maandalizi kuelekea msimu mpya. Kazi kubwa itafanyika na kikubwa ni kupata matokeo. Inawezekana na tunaamini itakuwa hivyo.

“Wachezaji ambao tumewatambulisha na wengine ambao bado wote ni wazuri. Ni kutoka pande zote za Afrika. Na viongozi wapo kila kona kufanya ukamilisho wa wachezaji wetu watakaopambania nembo kwenye mechi zote kitaifa na kimataifa.”

Hitimisho

Simba SC imeweka kambi nchini Misri kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa 2025/26. Katika kambi hiyo wapo wachezaji wapya na wale waliokuwa katika kikosi msimu wa 2024/25. Miongoni mwa wachezaji hao ni Kibu Dennis, Leonel Ateba, Jean Ahoua na Moussa Camara.

Usajili Simba SC
image

Share this: