Feisal na Mo HusseinFeisal na Mo Hussein
  • Tanzania vs Burkina Faso na Kenya vs DR Congo: Wenyeji waanza kwa moto wa kishindo CHAN 2024.
  • Tanzania imewachapa Burkina Faso 2-0, huku Kenya ikiwaduwaza DR Congo kwa kuwachapa bao 1-0.
  • Macho yote sasa ni kwa Uganda vs Algeria

Timu za Taifa za Tanzania na ile ya Kenya, zimeanza kwa kishindo kampeni zao za mashindano ya (CHAN). Hii ni baada ya Tanzania kuichapa Burkina Faso kwa mabao 2-0. Huku Kenya nao wakiwaduwaza DR Congo kwa kuicharaza bao 1-0. Hii imefanya timu mbili wenyeji wa mashindano hayo yanayoandaliwa kwa ushirikiano wa nchi tatu kuanza kwa rekodi ya pekee.

Cheza ‘Kindege’ cha Sportpesa uvune mamilioni leo

Ukiendelea kuhabarika na makala hii, kumbuka unaweza kushinda mamilioni muda huu. Cheza sasa mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kupitia Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa bonyeza picha hii chini.

SEO Banner LV

Kuhusu Tanzania 2-0 Burkina Faso

Tanzania vs Burkina Faso na Kenya vs DR Congo
Tanzania vs Burkina Faso

Katika mchezo huo uliochezwa usiku wa Jumamosi kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. Tanzania ilikuwa ikiungwa mkono na mashabiki wenye hamasa kubwa walioujaa uwanja huo wa kitaifa. Taifa Stars walidhibiti sehemu kubwa ya mchezo huo wa Kundi B ambao pia ulipata heshima ya kuwa mchezo wa ufunguzi.

Tanzania iliandika historia kwa kupata ushindi wa kwanza katika historia ya mashindano hayo. Hii ni baada kupoteza mechi zote mbili za ufunguzi kwenye mashindano yaliotangulia. Mkwaju wa penati uliopigwa kwa utulivu mkubwa na Abdul Sopu katika kipindi cha kwanza uliitanguliza Tanzania. Mohamed Hussein aliifungia Tanzania bao la pili kwa kichwa kizito katikati ya kipindi cha pili.

Tanzania ilianza kwa kasi, ambapo Clement Mzize na Feisal Salum walimpa wakati mgumu kipa wa Burkina Faso, Ladji Sanou. Hii ni baada ya kumwelekezea mashuti ya kutisha katika dakika za awali. Upande wa pili, kipa wa Tanzania Yakoub Suleiman alilazimika kuzuia mashambulizi ya Souleymane Sangaré na Papus Ouattara.

Dakika chache kabla ya mapumziko, Mzize alidondoshwa kwenye kisanduku na Frank Tologo. Hii ikampa, Sopu nafasi ya kukwamisha mkwaju wa penati wavuni. Burkina Faso walifanya mabadiliko matatu kipindi cha mapumziko, kwa kuwatambulisha wachezaji wenye uzoefu kama Patrick Malo na Yves Koutiama.

Baada ya kipindi cha shinikizo la mfululizo, Mudathir Yahya alipiga krosi hatari kutoka upande wa kulia. Mohamed Hussein akaruka juu zaidi ya walinzi wote na kufunga kwa kichwa safi katika dakika ya 71, akiweka bao la pili kambani. Burkina Faso walijaribu kujibu mapigo lakini ikashindikana.

SOMA HII ZAIDI: Tanzania 2-1 Senegal CECAFA 2025 Arusha | Maandalizi ya CHAN yapamba moto

Nafasi nzuri kwa Tanzania kufuzu kundi B

Mchezaji bora wa mechi
Mchezaji bora wa mechi

Matokeo hayo yanaiweka Tanzania katika nafasi nzuri ya kufuzu mapema. Katika kundi gumu linalojumuisha timu za Madagascar, Mauritania, na Jamhuri ya Afrika ya Kati. Kwa upande wa Burkina Faso kipigo hiko kinawafanya kuendelea kusubiri ushindi wao wa kwanza wa mashindano hayo.

SOMA HII PIA: Orodha ya wachezaji waliosajiliwa Yanga SC 2025/26 | Vita yao na Simba SC balaa zito

Kenya wawaduwaza DR Congo

Kenya Vs DR Congo
Kenya Vs DR Congo

Baada ya Tanzania, Kenya nao yapata ushindi wa kihistoria dhidi ya Mabingwa wa mara wa mashindano hayo DR Congo. Hii ni katika mchezo ambao umepigwa leo Jumapili kwenye Uwanja wa Kasarani Kenya. Wakenya wameandika historia kwa ushindi wa bao 1-0. Goli pekee la Austin Odhiambo liliamua matokeo ya mchezo huu mkali wa Kundi A.

Ikumbukwe mashindano ya TotalEnergies CHAN hufanyika kila baada ya miaka miwili. Hii pia ni kwa ajili ya wachezaji wanaoshiriki ligi za ndani pekee. Hii ni kwa ajili ya kutoa jukwaa kwa vipaji vya ndani kung’ara.

SOMA HII PIA: Simba SC yasajili mashine hizi mbili kwa mpigo, kuelekea Ligi Kuu ya NBC 2025/26

Hitimisho: Kuhusu Kenya 1-0 DR Congo

DR Congo walidhani wamefungua ukurasa mapema dakika ya tano kupitia Jephté Kitambala, lakini bao hilo lilikataliwa kwa kuotea baada ya ukaguzi wa VAR. Tukio hilo liliipa Kenya muda wa kutulia na kuingia kwenye mchezo. Wakenya walikuwa na motisha kubwa kutoka kwa mashabiki takribani 60,000 waliokuwa uwanjani.

Licha ya DR Congo kumiliki mpira kwa kiasi kikubwa mwanzoni mwa mchezo, Kenya walibaki kuwa na nidhamu na mpango Madhubuti ya kusaka ushindi. Bao la ushindi lilikuja muda mfupi kabla ya mapumziko, yaani dakika ya 45+2. Hii ni baada ya David Sakwa kumpasia Odhiambo, ambaye alimalizia kwa utulivu kwa mguu wa kushoto.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.