- Offen Chikola atambulishwa Yanga SC hivyo kwa sasa ni Mwananchi kuelekea msimu wa 2025/26.
- Green & Yellow itakuwa ni rangi atakazovaa kwenye mechi za ushindani katika mechi za kitaifa na kimataifa.
- Mguu wake wa kushoto una uwezo mkubwa kwenye kufunga magoli akiwa uwanjani, Simba SC walitajwa kuiwinda saini yake.
Offen Chikola ni kijani na njano baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili. Kiungo huyo mshambuliaji anajua kufunga na mguu wake wenye nguvu ni ule wa kushoto. Kipa namba moja wa Yanga SC, Djigui Diarra anamtambua vema kwa kuwa alikutana na balaa lake.

Paisha kindege uvune mamilioni sasa hivi

Ni muda wakuvuna mamilioni sasa hivi. Cheza na ushinde bila tabu yoyote ile. Ni mchezo wa Aviator ambao ni habari ya mjini.
Ni mchezaji wa pili kutambulishwa ndani ya kikosi cha Yanga SC ambao ni mabingwa msimu wa 2024/25. Offen Chikola anaungana na Balla Conte ambaye alikuwa mchezaji wa kwanza kutambulishwa. Ilikuwa ni Julai 18 2025 Yanga SC ilimtambulusha Moussa Balla Conte.
Kiungo Balla Conte alikuwa anacheza ndani ya Klabu ya CS Sfaxien ya Tunisia. Conte yeye ni raia wa Guinea alisaini dili la miaka mitatu. Msimu wa 2025/26 atakuwa kwenye changamoto mpya.
Wote walitajwa kutakiwa na Simba SC
Katika dirisha la usajili kuna mengi ambayo yanatokea. Wachezaji hawa wote wawili walikuwa wanatajwa kutakiwa na watani zao wa jadi Simba SC. Mipango imekwenda tofauti kwa kuwa nyota hawa wametambulishwa Jangwani.

Soma hii: Balla Conte amesaini rasmi Yanga SC na kutambulishwa kuelekea Ligi Kuu NBC 2025/26
Ikumbukwe kwamba Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC aliwahi kuweka wazi kuhusu hilo. Alipokuwa akizungumza katika mahojiano kupitia Crown FM. Ahmed alisema kuwa Conte ni moja ya wachezaji wenye ubora.
“Conte ni mchezaji mwenye ubora na anajua mpira. Ikiwa tutampata Simba SC kutakuwa na kazi kubwa itakayofanyika uwanjani na furaha kwa mashabiki. Kocha Mkuu, Fadlu Davids anakubali uwezo wake na anapenda kufanya naye kazi,” ilikuwa ni nukuu ya Ahmed kabla ya mchezaji kutambulishwa Yanga SC.
Rekodi za Offen Chikola
Kiungo mshambuliaji aliyekuwa Tabora United, Offen Chikola alitambulishwa Yanga SC Julai 22 2025 kwa kandarasi ya miaka miwili. 2024/25 akiwa na Tabora United alifunga mabao 8 kati ya 28 yaliyofungwa na timu hiyo. Ni nafasi ya tano kwenye msimamo pointi 38 baada ya mechi 30 ilikusanya Tabora United.
Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza, Uwanja wa Azam Complex 1-3 Yanga SC, Novemba 7 2024 mwamuzi alikuwa Nassoro Mwinchui. Chikola alifunga bao dakika ya 19 kwa mguu wa kushoto akitumia pasi ya Yacouba akiwa nje ya 18 na dakika ya 45 alifunga bao la pili kwa mguu wa kushoto akiwa ndani ya 18.
Dakika ya 77 ni Nelson Lunganga kwa mguu wa kulia akiwa ndani ya 18. Bao pekee la kufuta machozi kwa Yanga SC lilifungwa na Clement Mzize dakika ya 90 kwa mguu wa kulia akiwa nje ya 18 akitumia pasi ya Prince Dube.
Aziz Ki alikosa penati iliyosababishwa na Andy Bikoko baada ya kumchezea faulo Pacome. Kwenye mchezo huo dakika ya 45 Hussen Masalanga aliyeanza langoni alionyeshwa kadi ya njano kwa tafsri yakupoteza muda na aliokoa mkwaju wa penati ya Aziz Ki.
Tuzo mbele ya Yanga SC
Offen Chikola alitwaa tuzo ya mchezaji bora mbele ya Yanga SC. Kwenye mchezo huo wa mzunguko wa kwanza alichaguliwa kuwa mchezaji bora. Mabao mawili aliyofunga kwa mguu wa kushoto yalikuwa ni muhimu kwa Tabora United.

Soma hii: Usajili mpya Yanga balaa! Sowah, Bada, Chikola kwenye Yanga mpya
Aliwashinda wachezaji wengine ikiwa ni Pacome wa Yanga SC, Aziz Ki ambaye kwa sasa hatakuwa ndani ya Yanga SC kwa kuwa yupo Wydad Casablanca. Prince Dube wa Yanga SC na Yacouba ambaye alikuwa akimtengenezea pasi kwenye mchezo huo.
Kipigo kikubwa kwa Yanga SC
Yanga SC msimu wa 2024/25 kipigo kikubwa ilipata mchezo mmoja pekee. Katika mchezo dhidi ya Tabora United. Baada ya dakika 90 ubao uliposoma Yanga 1-3 Tabora United ilikuwa ni kipigo cha kwanza kikubwa na cha mwisho kwa msimu.
Katika mchezo wa mzunguko wa pili, Yanga SC ililipa kisasi. Baada ya dakika 90 ubao ulisoma Tabora United 0-3 Yanga SC. Katika msako wa pointi sita ndani ya dakika 180 wababe hawa waligawana tatutatu, kila timu ilitwaa pointi tatu ikiwa ugenini.
Gamondi alikutana na Thank You
Mara baada ya mchezo dhidi ya Tabora United, Yanga SC haikudumu na kocha Miguel Gamondi. Kocha huyo alikutana na Thank You ikiwa ni mzunguko wa kwanza. Kwa sasa Gamondi ni alipata kazi Singida Black Stars atakuwa hapo msimu wa 2025/26.
Hitimisho
Yanga SC inafanya maboresho ya kikosi kuelekea msimu wa 2025/26. Ni mashindano makubwa mawili itashiriki Ligi Kuu Bara inayodhaminiwa na NBC na Ligi ya Mabingwa Afrika. Katika ligi wao ni mabingwa watetezi wanakibarua kusaka ubingwa wa 32 msimu ujao.


