Makabidhiano ya HundiMakabidhiano ya Hundi
  • SportPesa yaipa Yanga SC Milioni 262.5: Makombe matano yaendelea kuleta neema kama mvua Yanga.
  • SportPesa na Yanga SC wamekuwa na mahusiano ya muda mrefu yanayokaribia kufikia miaka 8.
  • Mkataba wa udhamini wa SportPesa umefanya Yanga kuvuna zaidi ya Bilioni 17.

Mara baada ya kuwa na mafanikio makubwa kwa msimu wa 2024/25 wakizoa makombe matano uongozi wa Kampuni ya SportPesa yaipa Yanga SC Milioni 262.5 ambazo ni sehemu ya kukamilisha takwa la kimkataba kwa kutoa gawio la Tsh milioni 262.5 kama sehemu ya hongera kwa mafanikio bora yaliyopatikana ndani ya timu hiyo.

Uhusiano kati ya SportPesa na Yanga SC

SportPesa yaipa Yanga SC Milioni 262.5: Makombe matano yatajwa
Mataji matano ya Yanga

Uongozi wa klabu ya Yanga SC umekuwa na mahusiano ya muda mrefu yanayokaribia kufikia miaka 8 na Kampuni ya SportPesa ambao ni wadhamini wakuu wa Yanga katika kipindi hiko chote. Miaka hiyo 8 inagawanyika katika vipindi viwili. Mkataba wa kwanza wa SportPesa na Yanga ulikuwa wa miaka mitano ambao ulimalizika mwaka 2022 ukiwa na thamani ya Bilioni 5.2.

Shinda mamilioni ya kindege cha SportPesa kwa kubonyeza picha hii chini

SEO Banner LV

Yanga yavuna Bilioni 17 kutoka SportPesa

Mwaka 2022 SporPesa na Yanga waliingia mkataba mwingine wa miaka mitatu wenye thamani ya Bilioni 12.33, ambapo kwenye kila msimu Yanga wamekuwa wakivuna kiasi cha Shilingi Bilioni 4 ambazo zimekuwa zikitumika kwa maendeleo ya timu hiyo. Mkataba wa udhamini wa SportPesa katika kipindi cha miaka 8 umeifanya Yanga kuvuna zaidi ya Bilioni 17. Hii imefanya timu hiyo kuwa na jeuri ya kununua mastaa wakubwa kama Aziz Ki na Pacome.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi SportPesa Tanzania afunguka mazito

Abbas Tarimba
Abbas Tarimba

Akizungumzia makabidhiano hayo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya SportPesa Tanzania, Abbas Tarimba amesema: “Sportpesa tunachukua nafasi hii adhimu kuwapongeza sana Viongozi wa Young Africans SC kwa namna ambavyo wameibadilisha hii Klabu. Young Africans SC imepata mafanikio kwenye msimu ambao ulikuwa mgumu sana. Kubeba mataji matano sio jambo dogo kabisa katika historia ya nchi hii.

“Huu ndio mwaka bora kabisa katika historia ya Klabu hii. Kwenye mkataba wetu tulikubaliana kuwa na zawadi ya gawio kama sehemu ya matokeo haya ya kuwa na msimu bora na wenye mafanikio. Leo tutakabidhi hundi ya Tsh 262.5m kwa Young Africans SC kwa kufikia mafanikio haya. Kampuni ya SportPesa kwa kipindi cha miaka saba hatujawahi kukosa kutimiza sharti letu la kimkataba.

“Watanzania wana matamanio makubwa ya kuleta kombe la Afrika. Kwa Uongozi huu sina mashaka kuwa hili linawezekana. Young Africans SC ina Wachezaji bora kutoka kila kona la bara la Afrika. Niwatakie kila la kheri kwa msimu unaokuja na misimu mingine.”

SOMA HII PIA: Kabla ya Ikulu Makombe 5 ya Yanga yatua mjengoni SportPesa

Huyu hapa Rais wa Yanga SC, Hersi Said

Hersi Said
Hersi Said

Kwa niaba ya uongozi wa Taasisi ya Yanga SC, Rais Hersi Said amesema: “Leo tumekuja kuwaonesha wadhamini mafanikio makubwa ambayo tumeyapata kwa msimu wa 2024/25. Vile vile tumekuja kupokea gawio letu kutoka kwa mdhamini mkuu.

“Kimsingi tunawapongeza sana SportPesa kwa mchango wake mkuu. Kwa kipindi cha miaka nane tunajivunia mafanikio makubwa. Tumeshinda mataji ya ligi kuu na FA mfululizo tukiwa na mdhamini mkuu bora.”

SOMA HII PIA: Yanga SC haina utani kuwapa mikataba mastaa hawa wa kazi 2025/26

SportPesa na Yanga bado wapo pamoja, agusia mazungumzo ya mkataba mpya

Makabidhiano ya Hundi
Makabidhiano ya Hundi

Rais wa Yanga, Hersi aliendelea kusema: “Mahusinao ya Young Africans SC na Sportpesa yamekuwa mahusiano yenye afya. Tupo kwenye mazungumzo ya mkataba mpya. Tumeona dhamira yao na sisi tusingetamani kwenda kwa mdhamini mwingine hivyo huenda tukafikia pazuri. Sportpesa hawajawahi kuwa na shaka katika kutekeleza yale ambayo tumekubaliana.

“Kwa kuwa tumekuwa wote pamoja na tunatamani tuendelee kuwa na mdhamini huyu ambaye ni bingwa. Niwapongeze sana wanahabari ambao wamekuwa wakifanya kazi nzuri ya kuhabarisha. Wanahabari wamekuwa chachu ya kuboresha mahusiano yetu sisi na wadhamini wetu.

“Uzalishaji wa maudhui bora pia umeongeza chachu ya kuitangaza Klabu yetu kwa walaji wao. Hongereni sana wanahabari kwa kazi nzuri na naendelea kuwasisitiza muendelee kufanya kazi yenu nzuri kwa weledi wa kutosha.”

Hitimisho

Hatimaye msimu wa Ligi Kuu Bara umefikia tamati kwa Yanga kushinda ubingwa, huku Wananchi wakiishukuru SportPesa mdhamini kuu na kuendelea kujivunia kuwa sehemu ya kampuni hii bora ya michezo ya kubashiri Tanzania, ambayo pia imekuwa ikibadilisha maisha ya watu.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.