- Timu tano zilikuwa na maajabu ya sabasaba kwenye matokeo ya msako wa ushindi katika mechi za ushindani ndani ya NBC 2024/25.
- Yanga SC na Simba SC zatuma ujumbe maalumu kwa mashabiki wao kuhusiana na Sabasaba.
- Mashujaa FC ya Kigoma mwisho wa reli yamaliza ikiwa nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi.
Kuna timu tano zilikuwa na maajabu ya sabasaba kutokana na mwendo ambao walikuwa nao ndani ya ligi. Wakati Tanzania Julai 7 ikiwa ni maadhimisho ya Sikukuu ya Sabasaba zipo timu ambazo namba hizo kwao zilikuwa ni rekodi katika msako wa pointi ndani ya dakika 90. Ipo wazi kwamba bingwa wa ligi 2024/25 ni Yanga SC iliyokuwa inanolewa na Kocha Mkuu, Miloud Hamdi.
Vuna mamilioni sasa

Ni muda wako wa kuvuna mamilioni. Rahisi sana ukirusha kindege kwa kuwa zamu yako imefika leo.Kila siku yanavunwa mamilioni hivyo cheza sasa uvune mkwanja wako.

Soma hii: Dickson Job kusaini mkataba mpya
Hapa tunakuletea timu tano ambazo zilikuwa na maajabu kwenye namba saba. Ni timu moja pekee ipo ndani ya tano bora na timu moja iligotea nafasi ya mwisho hivyo itashiriki Championship msimu wa 2025/26 hizi hapa:-
Singida Black Stars-7

Soma hii: Aziz Ki atarejea Yanga SC
Singida Black Stars inayotumia Uwanja wa Liti kwa mechi za nyumbani ilipoteza mechi 7. Miongoni mwa mechi ilizopoteza ilikuwa dhidi ya Yanga SC iliyotwaa ubingwa.
Katika mechi mbili ambazo ni dakika 180, Singida Black Stars haikuvuna pointi mbele ya Yanga SC. Mchezo wa kwanza uliochezwa Zanzibar, baada ya dakika 90 ilikuwa Singida Black Stars 0-1 Yanga SC. Mzunguko wa pili ilikuwa Uwanja wa KMC Complex. Baada ya dakika 90 ilikuwa Singida Black Stars 1-2 Yanga SC.
Kwenye msako wa pointi sita, Singida Black Stars iliacha zote kwa Yanga SC. Mabao iliyofungwa ni matatu. Staa wa Singida Black Stars, Jonathan Sowah alifunga bao moja kwenye mchezo wa mzunguko wa pili.
Mbele ya Simba SC iliyomaliza ikiwa nafasi ya pili Singida Black Stars ilipoteza mechi zote mbili. Kwenye mchezo wa kwanza Uwanja wa Liti ilikuwa Singida Black Stars 0-1 Simba SC. Bao la ushindi kwa Simba SC lilifungwa na Fabrince Ngoma.
Dodoma Jiji sare 7
Wakati Singida Black Stars ikiwa ni timu pekee iliyopoteza mechi saba kwenye ligi. Zipo timu nyingine ambazo ilikuwa ni mwendo wa sabasaba kwenye kupata pointi moja. Katika orodha ya timu zilizoambulia sare 7 zipo tatu.
Wakulima wa Zabibu, Dodoma Jiji kutoka makao makuu ya Tanzania, waliambulia sare 7. Dodoma Jiji baada ya kucheza jumla ya mechi 30 ambazo ni dakika 2,700 iligotea nafasi ya 12.
Pointi zake ambazo ilikusanya kwenye msimamo wa ligi ya NBC ni 34. Timu hiyo haikuwa kwenye mwendo mzuri ndani ya ligi hasa kwenye eneo la ulinzi. Ni mabao 49 safu ya ulinzi iliruhusu kufungwa.
Ukiweka kando kuruhusu mabao 49, kwenye eneo la ushambuliaji bado haikuwa bora zaidi. Ni mabao 31 safu ya ushambuliaji ilifunga kwenue mechi za ushindani. Ikiwa na wastani wa kufunga bao moja kila baada ya dakika 87.
Ina uhakika wa kushiriki Ligi Kuu Bara msimu ujao wa 2025/26. Kazi kubwa itakuwa kwenye maboresho eneo la ushambuliaji na ulinzi pia. Ushindi kwa Dodoma Jiji ilikuwa kwenye mechi 9.
Tanzania Prisons-7
Kutoka Mbeya na inatumia Uwanja wa Sokoine kwa mechi za nyumbani. Tanzania Prisons iliambulia sare kwenye jumla ya mechi 7 kati ya 30 ilizoshuka uwanjani.
Msimu wa 2024/25 haukuwa bora kwa Prisons kutokana na mwendo wake kutokuwa imara. Ilicheza mchezo wa mtoano dhidi ya Fountain Gate. Ilipata ushindi hivyo ina uhakika wa kucheza ligi ya NBC kwa kuwa ilishinda nje ndani.
Mbele ya Yanga SC mzunguko wa pili ikiwa Uwanja wa Sokoine ubao ulisoma Tanzania Prisons 0-5 Yanga SC. Ilikuwa ni Juni 18 2025. Ilipoteza pointi tatu mzunguko wa pili mbele ya Yanga SC ambao ni mabingwa wa ligi msimu wa 2024/25.
KenGold-7
Haitakuwa ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara ya NBC 2025/26. Imeshuka daraja jumlajumla kwa kukusanya pointi 16 baada ya mechi 30 za ligi. Timu hiyo ilikuwa inatumia Uwanja wa Sokoine kwa mechi za nyumbani.
Mbali na kukusanya sare kwenye mechi saba, ni timu namba moja kufungwa mabao mengi. Ni mabao 62 timu hiyo ilifungwa kwenye ligi. Ikifuatiwa na Fountain Gate ambayo nit imu namba mbili kufungwa mabao mengi.
Fountain Gate iliyomaliza ligi ikiwa nafasi ya 14 ni mabao 58 ilifungwa. KenGold ya Mbeya ilikuwa na wastani wakufungwa bao moja kila baada ya dakika 43.
Mashujaa FC-7
Timu ambayo ilimaliza kwenye msimamo ikiwa nafasi ya saba ni Mashujaa FC. Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma unatumiwa na timu hii kwa mechi za nyumbani.Inaingia kwenye orodha ya timu ambazo zipo ndani ya 10 bora.
Mpango mkubwa kuelekea msimu ujao wa 2025/26 ni kuongeza nguvu kubwa kwenye usajili. Eneo la ulinzi ilikuwa imara ikiruhusu kufungwa mabao 29. Safu yake ya ushambuliaji ilifunga mabao 33 na ilikusanya jumla ya pointi 35.

Soma hii: Kabla ya Ikulu Makombe 5 ya Yanga yatua mjengoni SportPesa – SportPesa Tanzania
Hitimisho
Timu nyingi ziliwatakia mashabiki wao kheri ya Sabasaba ikiwa ni sikuu kubwa Tanzania. Sio Simba SC na Yanga SC pekee ambazo ziliwatakia mashabiki wao kheri mpaka Fountain Gate pia ilituma salamu kwa mashabiki.


