- Simba SC haina bahati mbele ya Yanga SC, yapigwa nje ndani dakika 180. Matukio makubwa matatu mchezo namba 184 yaandikwa.
- Yanga SC bingwa 2024/25, taji la 31 ndani ya ligi namba nne kwa ubora Afrika ikitwaa mbele ya mtani wa jadi, Simba SC.
- Fadlu Davids Kocha Mkuu wa Simba SC awapa pongezi Yanga SC kwa kutwaa ubingwa wa ligi, mabao Simba SC yafungwa 13.
Simba SC haina bahati mbele ya Yanga SC ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara. Msimu wa 2024/25 Yanga SC imepata ushindi nje ndani katika mechi za ushindani kwenye ligi. Kwenye msako wa pointi sita muhimu, zote zimebebwa na Yanga SC inayonolewa na Kocha Mkuu, Miloud Hamdi.
Vuna mamilioni sasa hivi

Muda wakuvuna mamilioni ni sasa. Rahisi sana na unavuna mamilioni hapo ulipo. Paisha kindege sasa ushinde.

Soma hii: Kariakoo Dabi kuna vita nyingine kwa wachezaji
Mechi 10 za ligi Kariakoo Dabi, Yanga ushindi mechi 5
Rekodi zinaonyesha kuwa kwenye mechi 10 za Ligi Kuu Bara ambayo ni namba nne kwa ubora Yanga SC imeshinda mechi tano. Kuanzia msimu wa 2020/21-2024/25, ushindi kwa Yanga SC ni mechi 5 na Simba SC mechi moja. Sare kwa wababe hawa ni nne. Ushindi wa Simba SC ilikuwa ni msimu wa 2022/23 baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba SC 2-0 Yanga SC.
Safu ya ushambuliaji ya Yanga SC imefunga jumla ya mabao 13 kwenye Kariakoo Dabi. Safu ya ushambuliaji ya Simba SC imefunga jumla ya mabao 6. Kinara wa utupiaji kwenye Kariakoo Dabi ni Aziz Ki ambaye ana jumla ya mabao matatu na kwa Simba SC ni Kibu Dennis mkandaji mwenye mabao mawili.
Mechi namba 184, Yanga SC 2-0 Simba SC, tukio la kwanza
Juni 25 2025 mchezo wa Kariakoo Dabi ulishuhudia matukio makubwa matatu. Katika dakika 90 ubao ulisoma Yanga SC 2-0 Simba SC. Ushindi ukiwa ni mali ya Yanga SC na pointi tatu kuelekea Jangwani.
Yanga SC walisubiri mpaka dakika ya 66 kupachika bao la kwanza ambalo lilifungwa na Pacome kwa mkwaju wa penati. Kip namba moja wa Simba SC, Moussa Camara alikwamakuokoa pigo hilo. Ni mguu wa kulia ulifanya maamuzi kwenye pigo hilo lililowanyanyua mashabiki wa Yanga SC.
Pacome sasa anafikisha mabao 12 ndani ya ligi. Pasi za mabao ambazo anazo ni 10 hivyo kahusika kwenye mabao 22 kati ya 83 yaliyofungwa na Yanga SC. Alichaguliwa kuwa mchezaji bora kwenye mchezo wa Kariakoo Dabi.
Bao la pili lilifungwa na Clement Mzize. Mzize anafikisha mabao 14 ndani ya ligi akiwa ni mzawa namba moja mwenye mabao mengi. Mbali na kufunga ametoa jumla ya pasi tano za mabao kwenye ligi.
Mzize alipachika bao dakika ya 87 akiwa ndani ya 18 akitumia pasi ya Pacome. Camara aliyeanza langoni alikwama kuokoa hatari hiyo. Yanga SC mwisho ilivuna pointi tatu jumla.
Tukio la pili ni sherehe za ubingwa

Soma hii: Mwamuzi Yanga SC vs Simba SC balaa! kuna kadi nyukundu leo? – SportPesa Tanzania
Shere za ubingwa zilifanyika Uwanja wa Mkapa mara baada ya mchezo kukamilika. Yanga SC mbele ya mashabiki ambao walijitokeza kushuhudia mchezo huo walinyanyua makwapa mbele ya mashabiki wa Simba SC. Ni taji la 31 kwa Yanga SC kutwaa ndani ya ligi ikiwa nit imu inayoongoza kwa kutwaa mataji mengi ya ligi.
Tukio la tatu ushindi mbele ya mtani
Yanga SC inatwaa ubingwa kwa kupata ushindi mbele ya mtani wake wa jadi Simba SC. Ikumbukwe kwamba mchezo namba 184 uliahirishwa mara ya kwanza Machi 8 ukapangiwa Juni 15 2025 kisha ukasogezwa mbele Juni 25 2025 na Yanga SC ikaibuka na ushindi.
Huyu hapa nahodha msaidizi wa Yanga SC
Dickson Job nahodha msaidizi wa Yanga SC amesema kuwa walikuwa wanahitaji kuifunga Simba SC kwa namna yoyote ile ili kutwaa ubingwa wa msimu wa 2024/25 jambo ambalo lilifanikiwa Juni 25 2025 kwenye mchezo wa mzunguko wa pili.
“Tulikuwa tunatambua kwamba tukipata sare tutakuwa mabingwa wa ligi.Ila sisi hilo tulikuwa hatuhitaji malengo yetu ilikuwa ni kupata ushindi mbele ya Simba SC jambo ambalo limetimia,” alisema Job.
Huyu hapa Kocha Mkuu wa Yanga SC, Miloud Hamdi

Soma hii: Yanga SC vs Simba sc, Juni 25 2025 kivumbi kitawaka
Kocha Mkuu wa Yanga SC, Miloud Hamdi amewapa tano wachezaji wat imu hiyo kutokana na kufanya kazi kwa juhudi. Yanga SC ni mabingwa wa ligi msimu wa 2024/25.
Ushindi ambao walipata mbele ya Simba SC kwa mabao 2-0 unawafanya wakamilishe msimu wakiwa na pointi 82. Watani zao wa jadi ni pointi 78 wanazo kibindoni. Tofauti ya pointi nne baada ya mechi 30.
Miloud amesema: “Ninawapongeza wachezaji kwa kazi kubwa ambayo wamefanya. Kufuata maelekezo kwenye mechi ambazo tumecheza hili ni jambo la kujivunia. Haikuwa kazi rahisi lakini imefanikiwa.”
Huyu hapa Fadlu Davids, Kocha Mkuu wa Simba SC
Fadlu Davids, Kocha Mkuu wa Simba SC amewapongeza Yanga SC kwa kutwaa ubingwa. Amebainisha kuwa bado Simba SC ipo kwenye mwendelezo wa kujenga timu. Huku akiongeza kuwa watafanya maboresho kuwa imara zaidi.

Soma hii: Yanga SC 2-0 Simba SC mchezo wa Kariakoo Dabi
“Pongezi kwa Yanga SC kutwaa ubingwa. Unaona namna ambavyo wanacheza na wachezaji wao ni wale wenye uwezo kucheza katika mechi kubwa. Hilo kwetu linatupa uzoefu na tutafanyia kazi nitaongea na uongozi ili kuwa na wachezaji bora zaidi kwani bado tupo kwenye ujenzi wa timu.”
Simba SC msimu wa 2024/25 haijatwaa taji lolote lile. Imepishana na mataji matatu makubwa iliyokuwa inapambania. Kombe la Shirikisho Afrika ni nafasi ya pili na bingwa ni RS Berkane. Ligi Kuu Tanzania Bara bingwa ni Yanga SC. Taji lingine ambalo imepishana nalo ni CRDB Federation Cup ikigotea hatua ya nusu fainali.


