Yanga SC 2-0 Simba SC: SportPesaMwamuzi Yanga vs Simba
  • Moto utawaka leo kwenye Kariakoo dabi Uwanja wa Benjamin Mkapa kuanza saa 11:00 jioni.
  • Namba za Mwamuzi wa derby, Amin Omar kwenye utoaji wa kadi ni hatari kiasi kwamba kuna uwezekano mkubwa wa kupatikana kwa kadi nyekundu.
  • Mpaka sasa amechezesha jumla ya mechi (239), kwenye hizo mechi ametoa kadi za njano (823), ametoa jumla ya kadi nyekundu (47).

MOTO utawaka leo kwenye Kariakoo dabi Uwanja wa Benjamin Mkapa ambapo mjadala mkubwa ni Mwamuzi Yanga SC vs Simba SC kutoka Misri, Amin Omar na jopo lake kuchezesha mchezo huo mkubwa ambao unatarajia kuanza saa 11:00 jioni.

Historia yaandikwa Mwamuzi Yanga SC vs Simba SC

Mwamuzi Yanga vs Simba
Mwamuzi Yanga vs Simba

Historia inatarajiwa kuandikwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa leo Jumatano, ambapo Yanga wanatarajia kuwa wenyeji wa Simba katika mchezo mkubwa wa Kariakoo Dabi, ambao unatarajiwa kuamua bingwa kwa matokeo yoyote ambayo yatapatikana.

Jambo jingine la kihistoria ni kuwa katika mchezo huu ni matumizi ya waamuzi wa kigeni ambapo jopo zima la waamuzi watakaosimamia mchezo wanatokea nje ya Tanzania likiongozwa na waamuzi wanne wa Misri na mmoja wa Somalia huku Kamishina wa mechi akitokea Tanga.

SOMA HII PIA: Simba SC haina bahati mbele ya Yanga SC/ Yafungwa 13/ Yapigwa nje ndani

Mwamuzi anamwaga kadi, kuna kadi nyekundu?

Namba za Mwamuzi wa derby, Amin Omar kwenye utoaji wa kadi ni hatari kiasi kwamba kuna uwezekano mkubwa wa kupatikana kwa kadi nyekundu, ambapo amechezesha jumla ya mechi (239), kwenye hizo mechi ametoa kadi za njano (823) ametoa jumla ya kadi nyekundu (47).

Hawa hapa mastaa wa kuchungwa Yanga SC vs Simba SC

Pacome Zouzoua

Yanga vs Prisons
Pacome Zouzoua

Staa wa kimataifa wa Ivory Coast na kiungo mshambuliaji wa Yanga SC, Pacome Zouzoua ni mchezaji mwenye hatari. Kasi yake kwenye kufunga na kuwa na jicho lakuona hatari ni kubwa. Kwenye mchezo dhidi ya Tanzania Prisons alifunga mabao mawili huku Juni 18, 2025 na alichaguliwa kuwa mchezaji bora.

Pacome mpaka sasa amefanikiwa kufunga mabao 11 na kutoa pasi 9 za mabao hivyo mpaka sasa msimu huu amefanikiwa kahusika kwenye mabao 20 kati ya 81 yaliyofungwa na timu hiyo inayoongoza ligi kwa msimu wa 2024/25.

SOMA HII PIA: Jean Ahoua kubeba tuzo kiatu cha ufungaji bora 2024/25/ Orodha ya wafungaji

Clement Mzize

Mpaka sasa huyu ndiyo straika Mtanzania Clement Mzize mwenye magoli mengi zaidi na uwezo mkubwa wa kuasisti ambapo katika mechi mbili mfululizo amekuwa akitoa pasi za mabao. Mchezo dhidi ya Tanzania Prisons Juni 18 2025 na mchezo dhidi ya Dodoma Jiji, Juni 22 2025. Pasi zote za alimpa Clatous Chama.

Mzize kafunga mabao 13 ndani ya Yanga SC kati ya mabao 81. Huku akiwa amefanikiwa kutoa pasi tano za usaidizi wa mabao hivyo kufanya ahusike kwenye jumla ya mabao 18. Kwa sasa amekuwa akihusishwa kujiunga na Zamalek ya Misri.

Maxi Nzengeli

Amekuwa na wastani mzuri wa kuiadhibu Simba katika michezo mfululizo ambayo timu hizo zimekutana katika mashindano mbalimbali, huyu ni mfungaji wa bao la kwanza kwenye ligi ndani ya Yanga SC ilikuwa dhidi ya Kagera Sugar. Katika mchezo wa raundi ya 30 alifunga bao moja dhidi ya Dodoma Jiji.

Clatous Chama

Yanga SC vs Simba SC
Yanga SC vs Simba SC

Kiungo mshambuliaji wa Yanga SC aliyejiunga nao kutoka Simba. Amekuwa na mwendelezo wa kufunga mabao katika michezo ya hivi karibuni ambapo kwenye mchezo dhidi ya Tanzania Prisons alianzia benchi na alipoingia alifunga. Mchezo dhidi ya Dodoma Jiji alianza kikosi cha kwanza na alifunga.

Shomari Kapombe

Anatajwa kuwa beki bora zaidi wa kulia nchini kutokana na kucheza kwa kiwango bora kwa muda mrefu, amekuwa na hatari kwenye kusababisha penati ndani ya uwanja. Mchezo dhidi ya JKT Tanzania dakika ya 90 alichezewa faulo ndani ya 18. Faulo hiyo ilileta penati iliyofungwa na Ahoua.

Steven Mukwala

KenGold FC vs Simba SC
KenGold FC vs Simba SC

Akiwa kwenye msimu wake wa kwanza tu ndani ya Simba ameonyesha kuwa miongoni mwa mstaa hatari, Katika mchezo dhidi ya Kagera Sugar dakika ya 17 alifunga bao la ushindi ukiwa ni mchezo wa mwisho kabla ya leo. Pasi ya Duchu aliitumia vizuri akiwa ndani ya 18, Uwanja wa KMC Complex.

Nyota huyo mbali na kufunga anajua kutengeneza pasi za mabao. Ni pasi tatu za mabao katengeneza akiwa amefunga jumla ya mabao 13 hivyo kahusika kwenye mabao 16 ya Simba SC iliyofunga mabao 69 baada ya mechi 29.

Jean Ahoua

Anapigiwa chapuo la kubeba tuzo ya mchezaji bora MVP kwa msimu huu, hii ni baada ya kuhusika kwenye mabao mengi zaidi, ambapo amehusika kwenye mabao 25 kati ya 69 yaliyofungwa na timu hiyo iliyo nafasi ya pili. Alianza kikosi cha kwanza mchezo dhidi ya Kagera Sugar.

Ahoua kafunga mabao 15 akitumia mguu wa kulia. Kafunga bao moja kwa pigo la kichwa ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya Pamba Jiji alipotumia pasi ya Ellie Mpanzu. Kwenye mchezo huo Ahoua alifunga hat trick yake ya kwanza.

Ellie Mpanzu

KenGold FC --- Simba SC
Mpanzu

Kama kuna staa ambaye anatazamwa sana leo, Ellie Mpanzu ambaye tangu ajiunge na Simba ameonekana kuwa na athari Chanya kwenye michezo mingi aliyocheza. Kwenye mchezo dhidi ya KenGold alifunga bao moja akiwa nje ya 18 na alitoa pasi kwa Leonel Ateba.

Ni miongoni mwa wachezaji wenye uwezo kwenye mechi kubwa. Hatari yake akiwa nje ya 18 ama ndani ya 18 katika kufanya maamuzi. Hakuanza kikosi cha kwanza dhidi ya Kagera Sugar.

Hitimisho

Huu ni mchezo wa kihistoria na matumizi ya jopo hili la waamuzi linatarajia kuleta funzo kubwa na ladha ya kipekee, dakika 90 ndizo zinatarajia kutoa majibu ya nini kitatokea na taswira ya nani anakwenda kuwa bingwa wa ligi kwa msimu huu 2025/26

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.