Hamdi (-)Hamdi (-)
  • Yanga SC wanazitaka pointi tatu za Tanzania Prisons Juni 18 2025, mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
  • Tanzania Prisons wabainisha namna watakavyoizuia Yanga SC kwenye mchezo wa mzunguko wa pili.
  • Yanga SC ilipata ushindi wa 4-0 katika mchezo wa mzunguko wa kwanza, Maxi Nzengeli yupo kamili kwa kazi.

Yanga SC wanazitaka pointi tatu za Tanzania Prisons watakaokabiliana nao Juni 18 2025 Uwanja wa Sokoine, Mbeya ikiwa ni mzunguko wa pili kukamilisha dakika 180 ndani ya msimu wa 2024/25. Tanzania Prisons rekodi zinaonyesha kuwa katika mchezo wa mzunguko wa kwanza wakiwa ugenini, Uwanja wa KMC Complex walikwama kuvuna pointi tatu baada ya ubao kusoma Yanga SC 4-0 Tanzania Prisons.

Miloud Hamdi
Miloud Hamdi, Kocha Mkuu wa Yanga SC. Source: Yanga SC.

Soma hii: Tanzania Prisons vs Yanga SC Juni 18 2025 Uwanja wa Sokoine

Nafasi ambayo wapo Tanzania Prisons kwenye msimamo ni ya 13 huku Yanga SC wakiwa nafasi ya kwanza kwenye msimamo wanakimbizia malengo ya kutetea taji la ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo ni namba nne kwa ubora.

Huyu hapa kocha wa Yanga SC, Miloud Hamdi

Kocha Mkuu wa Yanga SC, Miloud Hamdi amesema kuwa wanawaheshimu wapinzani wao Tanzania Prisons ila wanachohitaji ni pointi tatu muhimu. Yanga SC itakaribishwa na Tanzania Prisons kwenye mchezo wa ligi unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Sokoine, Juni 18 2025 saa 10:00 ikiwa ni mzunguko wa pili. Utakuwa ni mchezo wa 28 kwa Yanga SC na 29 kwa Tanzania Prisons.

Maxi Nzengeli (-)
Maxi Nzengeli kiungo mshambuliaji wa Yanga SC kwenye maandalizi ya mwisho kuwakabili Prisons. Source: Yanga SC.

Soma hii: Yanga SC vs Simba SC kwenye msako wa pointi tatu ndani ya ligi Juni 18/ Mechi namba 184 kimbembe

“Tunawaheshimu sana Tanzania Prisons, lakini sisi ni Yanga SC. Nina wachezaji wenye uzoefu na uwezo mkubwa. Tunajua utakuwa mchezo mgumu lakini hatuna sababu ya kuwaza sana kuhusu hilo. Tumekuja kushindana kwa tahadhari kubwa na ambacho tunahitaji ni pointi tatu muhimu.

“Tumekuja Mbeya kusaka alama tatu tunawashukuru sana mashabiki, nimefanya kazi klabu mbalimbali kubwa lakini mashabiki wa Yanga SC ni mashabiki wa mfano. Naamini kwa mchango wao uwanjani basi tutakuwa na wakati mzuri. Niwaombe sana mashabiki wajitokeze kwa wingi.

“Maandalizi yetu yapo vizuri sana, tuna fainali nne za kucheza. Tupo tayari kuukabili mchezo wa kikamilifu. Kila mchezaji anajua kitu gani cha kufanya. Kikosi chetu kipo kamili hakuna majeruhi wapya. Hatuna presha yoyote na hatuna sababu ya kuwa na presha.”

Huyu hapa kocha wa Tanzania Prisons

Amani Josiah Kocha Mkuu wa Tanzania Prisons ameweka wazi kuwa wanatambua mchezo wao dhidi ya Yanga SC utakuwa na ushindani mkubwa jambo lililowafanya wafanye maandalizi mazuri kuwakabili mabingwa watetezi wa ligi katika Uwanja wa Sokoine, Mbeya saa 10:00 jioni.

“Hatkuwa na mwanzo mzuri kwenye mzunguko wa kwanza unaona wakati nakuja kulikuwa kuna shida kwenye eneo la kufunga mabao mengi na kwa sasa tunazidi kuimarika taratibu hivyo kueleke mchezo wetu dhidi ya Yanga SC tup tayari kwa ajili ya kupambana kupata pointi tatu muhimu.”

Huyu hapa Aziz Andambile mchezaji wa Yanga SC

Aziz Andambwile kiungo wa Yanga SC ameweka wazi kuwa watatumia akili kubwa na nguvu kuwakabili wapinzani wao Tanzania Prisons kwenye mchezo wa mzunguko wa pili. Nyota huyo amewaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi uwanjani.

KenGold FC vs Simba SC 'live'

“Ukweli usiopingika Prisons wana timu ngumu, sina shaka na uwezo wao. Wana timu imara na wanahitaji alama tatu kama sisi. Sisi kama Wachezaji lazima tuweke nguvu na akili maana tunajua tunachokitaka kwenye mchezo wetu muhimu.

 “Tunafahamu kuna mashabiki wengi sana wanatokea maeneo mbalimbali kuja Mbeya tunawashukuru sana na tuna matumaini watajaa kwa wingi uwanjani. Wachezaji tupo tayari kwa mchezo na tutapambana ili kupata matokeo mazuri.”

Matokeo ya mzunguko wa kwanza walipokutana

Mchezo wa Juni 18 2025 ambayo ni leo utakuwa ni mzunguko wa pili kwa wababe hawa kukutana ndani ya uwanja katika dakika 90 za kazi kwenye msako wa pointi tatu muhimu. Desemba 22 2024 walipokutana kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza ubao wa Uwanja wa KMC Complex ulisoma Yanga 4-0 Tanzania Prisons, hivyo mchezo wa leo utakuwa na ushindani mkubwa.

Msimamo wa Tanzania Prisons vs Yanga SC

Clement Mzize na Dube
Clement Mzize na Dube washambuliaji wa Yanga SC. Source: Yanga SC.

Soma hii:Ibenge & Maxi watikisa taarifa mpya usajili Bongo

Yanga SC kwenye msimamo ni namba moja ikiwa na pointi 73 baada ya kucheza mechi 27 inakutana na Prisons ambayo imecheza mechi 28. Tanzania Prisons ipo nafasi ya 13 ikiwa na pointi 30 inapambana kujinasua kwenye nafasi ya kucheza play off.

Safu ya ushambuliaji ya Yanga SC imefunga mabao 71 ikisa ni timu namba moja kufunga mabao mengi huku Prisons safu ya ushambuliaji imetupia mabao 23. Inakutana na Prisons ambayo haijawa kwenye ubora katika eneo la ufungaji. Prince Dube na Clement Mzize wa Yanga SC hawa wamefunga mabao 13 kila mmoja.

Share this: