Yanga SC vs Simba SC taarifa muhimu kuhusu waamuzi wa mchezo wa Juni 15 2025, viingilio, waamuzi, zinatarajiwa kutolewa muda wowote kuanzia sasa kuelekea kwenye mchezo huo wa watani wa jadi ambao unatarajiwa kuchezwa Juni 15 2025, Uwanja wa Mkapa.

Soma hii:Yanga SC vs Simba SC hawa wachezaji wakuchungwa Juni 15 2025
Huu ni mchezo wa mzunguko wa pili ambao umekuwa na mvutano mkubwa ambapo awali ulitarajiwa kuchezwa Machi 8 2025 ila uliahirishwa na tarehe mpya ilipotolewa Yanga SC walibainisha kuwa hawatacheza mchezo huo mpaka matakwa yao manne yatimizwe.

Ofisa Habari wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania, (TPLB) Karim Boimanda kupitia Azam TV ameweka wazi kuwa maandalizi kuelekea mchezo wa Kariakoo Dabi unaotarajiwa kuchezwa Juni 15 2025 yapo vizuri na kuna taarifa nyeti na muhimu zitatolewa muda wowote kuanzia sasa.
Yanga SC ni wenyeji wa mchezo huo namba 184 ambao unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa ambapo watakipiga dhidi ya Simba SC ambao katika mchezo wa mzunguko wa kwanza walipoteza pointi tatu muhimu ubao uliposoma Simba SC 0-1 Yanga SC.
Boimanda ameweka wazi kuwa maandalizi kuelekea mchezo huo yanaendelea vizuri kutokana na ukubwa wa mchezo ambao unatoa taswira ya ligi ambayo ni namba nne kwa ubora Afrika. Yanga SC ni wenyeji ambapo watawakaribisha Simba SC.
“Maandalizi yapo vizuri lakini pia ni vizuri nikitoa taarifa kuwa kuna baadhi ya taarifa nyeti na muhimu kwa ajili ya mchezo huo zitatolewa muda wowote kuanzia sasa hivyo zitakuwa zinakwenda kutamatisha kuhusu maandalizi ya mchezo nadhani wadau wanapaswa kusubiri kusikia kutoka bodi ya ligi kusikia kuhusunia na mchezo huo.
“Tumekuwa tukisisitiza kuwa maandalizi yanaendelea. Tunaamini kwamba wadau wengine zikiwemo hizo timu mbili Yanga SC na Simba SC wanaendelea na maandalizi mchezo ambao ni mkubwa mchezo namba 184 ambao ni kioo cha ligi yetu mchezo ambao umekuwa ukivuta hisia za watu wengi.
“Ni matumaini yetu kwamba wadau wote wanaendelea na maandalizi yao. Na kwamba kwa maana ya ujumbe kutoka bodi ya ligi ni kwamba ili tukio hili kubwa lifane kila mmoja lazima ashiriki kwa ukamilifu kwa ajili ya tukio hili ili kufikia siku tukiwa tayari kubwa ambalo limekuwa likivutia hata watu wa nje kwa ajili ya mchezo huu muhimu.
“Kuna baadhi ya taarifa muhimu zitatolewa muda mfupi kuanzia sasa zinatarajiwa kutolewa hivi karibuni ikiwa ni kama vile maofisa wa mchezo, kwa maana ya waamuzi, viingilio masuala ya uuzwaji wa tiketi zitatolewa hivi karibuni.
Mzunguko wa 29 na 30 mpango upo namna hii

Soma na hii: Hatuchezi ya Yanga SC imehamia Simba SC kuelekea Juni 15, Mambo yazidi kuharibika
Kuhusu mechi za raundi mbili za mwisho ambazo hutoa picha kamili ya timu ambazo zitashuka jumlajumla na zile ambazo zitacheza mchezo wa mtoano Boimanda ameweka wazi kuwa mchezo wa raundi ya 29 Juni 18 na raundi ya 30 Juni 22.
“Viwanja vyote ambavyo awali kulikuwa na changamoto tuliwasiliana na vilabu vyote kwa ajili ya maboresho na kwa asilimia kubwa tayari vimekamilika. Michezo ya raundi mbili ya 29 na 30 kila kitu kipo sawa na tusubiri burudani yakutamatisha msimu wa 2024/25.”
Taarifa ya Simba SC kuhusu Kariakoo Dabi
Juni 12 2025, Simba SC ilitoa taarifa kuwa ikiwa mchezo huo utabadilishwa tarehe nyingine wao hawatakuwa tayari kushiriki mchezo ujao kwa namna yoyote kwa kuwa maandalizi yao yapo tayari na watapeleka timu uwanjani.

“Klabu ya Simba inauarifu umma, wanachama na wapenzi wake kuwa itaingia uwanjani siku yavJumapili, Juni 15 2025 kushiriki mchezo namba 184 kama ilivyopangwa na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania. Mabadiliko yoyote ya kujaribu kuahirisha mchezo huo ni batili na kinyume na taratibu za uendeshaji wa mpira wa miguu. Kwa msingi huo.
Klabu ya Simba haitashiriki mchezo wowote wa namba 184 isipokuwa ule uliopangwa kuchezwa siku ya Junapili Juni 15 2025. Tunawaomba wanachama na wapenzi wa klabu yetu kujitokeza kwa wingi kuijaza Benjamini Mkapa siku hiyo muhimu ili kuiunga mkono timu yetu. Ilieleza taarifa hiyo ya Simba SC, Juni 12 2025.
Yanga SC msimamo wao

Soma na hii: Yanga SC wametoa matakwa manne yakitimizwa Kariakoo Dabi kuchezwa
Yanga SC msimamo wao ni kutoshiriki mchezo namba 184 mpaka matakwa yao manne yatakapofanyiwa kazo haraka na ikishindikana wameweka wazi kuwa hawatakuwa tayari kushiriki Ligi Kuu Bara msimu wa 2025/26 kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga SC, Ali Kamwe.

