Hatuchezi ya Yanga SC imehamia Simba SC kuelekea Juni 15Ali Kamwe (-)
  • Mechi Yanga SC vs Singida Black Stars Juni 28 2025 inazidi kuingia moshi wa sintofahamu kama utachezwa.
  • Yanga wasisitiza ‘Dawa ya deni ni kulipa’
  • Kikao kingine kizito kufanyika Jumatano hii ofisi za TFF

Dawa ya deni ni kulipa ndiyo msisitizo wa uongozi wa Yanga kuhusu kulipwa kwa madai yao, kabla ya kushiriki katika mchezo wa Fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB mechi ya Yanga SC vs Singida Black Stars Juni 28, mwaka huu.

Hali tete Yanga dhidi ya TFF, Bodi ya Ligi

Katika kipindi cha siku mbili zilizopita, Umma wa soka Tanzania umeshuhudia sarakasi za matatamko baina ya Taasisi zinazosimamia soka Tanzania, yaani Shirikisho la Soka TFF na Bodi ya usimamizi wa Ligi Kuu Tanzania TPLB dhidi ya timu ya Yanga.

Chanzo kilianzia kwenye mchezo namba 184 kati ya Yanga SC vs Simba SC kuahirishwa Machi 8, 2025 kwa sababu zenye utata huku mchezo huo ukipangwa tena Juni 15, 2025 na Yanga kugomea wakiwasilisha matakwa manne ambayo wanataka yafanyiwe kazi kabla ya kucheza.

Kuhusu Yanga SC vs Singida Black Stars Juni 28 2025

Siku chache zilizopita Bodi ya Ligi ilitangaza rasmi kuwa Fainali ya Kombe la CRDB kati ya Yanga SC vs Singida Black Stars itapigwa Juni 28, mwaka huu kwenye Uwanja wa Amaan Zanzibar, kabla ya Yanga hawajaibuka na madai mapya.

Yanga SC kupitia kwa Ofisa habari wao, Ali Kamwe wamebainisha kuwa mpaka watakapopewa hela ya ubingwa wa misimu mitatu iliyopita ya mashindano hayo, hawatacheza fainali jambo ambalo limewaibua wadhamini na mamlaka ya soka Tanzania, (TFF).

Ikumbukwe Yanga ndio mabingwa watetezi wa mashindano hayo, ambapo imetwaa taji hilo mara nne na msimu huu wamefanikiwa kutinga kwenye fainali yake ya tano baada ya kuwafungashia virago JKT Tanzania kwa ushindi wa mabao 2-0.

SOMA HII PIA: Yanga SC vs JKT Tanzania Mei 18 2025 Kariakoo Dabi yanukia

Kumbukumbu ya alichosema Kamwe

Kuhusu sakata hilo Ofisa habari wa Yanga, Ali Kamwe alisema:” Taarifa hii iwafikie ofisi ya Katibu Mkuu wa TFF na wadhamini wa mashindano ya Kombe la Shirikisho la CRDB kuwa hatutacheza fainali ya CRDB siku ya tarehe 28 mpaka tutakapolipwa hela ya ubingwa wa msimu uliopita.

“Tumevumilia dharau hizi kutoka kwa mamlaka za soka kwa muda mrefu sana. Sasa hii imefika mwisho. Hii ya Zanzibar pia hatuchezi. Kamwe aliongeza kuwa hawatakuwa tayari kucheza ligi msimu wa 2025/26 na hawatayumba kwa lolote lile kwa kuwa ni msimamo wao.

“Napenda kuwajuza waandishi wa Habari yasipofanyiwa kazi matakwa yetu matatu kwa uharaka Yanga SC hatutakuwa tayari kucheza mchezo namba 184, mechi zote mbili za ligi zilizobaki na hatutashiriki Ligi Kuu msimu ujao. Huu ndio msimamo wetu na hatutayumba kwa lolote.

SOMA HII PIA: KVZ FC vs Yanga patachimbika Muungano Cup 2025

TFF wafunguka kuidai Yanga, wataka Yanga kutuma mtaalamu wao wa fedha kukagua deni

Kufuatia taarifa hiyo ya Ofisa habari wa Yanga, uongozi wa TFF kupitia kwa Ofisa Habari wake, Clifford Ndimbo wakawajibu Yanga kuwa TFF ndiyo inayoidai Yanga SC ambao waliomba kwa barua fedha zao za zawadi zitumike kulipa malipo wanayotakiwa kulipa kwa TFF.

Sehemu ya Taarifa hiyo imeeleza: “Tunapenda kuuthibitishia umma kuwa benki ya CRDB ndiyo mdhamini mkuu wa mashindano ya Kombe la Shirikisho la TFF, na inatekeleza ipasavyo majukumu yake. Kwa msimu wa 2023/24 benki hiyo ililipa milioni mia mbili na Hamsini kwa ajili ya uendeshaji wa mashindano hayo.

“Tumemskia Meneja Habari wa Yanga SC, kupitia vyombo vya habari akidai kuwa klabu inaidai TFF milioni mia mbili ambayo ni zawadi ya ubingwa wa Kombe la Shirikisho la benki ya CRDB. Hivyo ili kutoendelea kusababisha sintofahamu kwa umma.

“Tumeiandikia barua Yanga SC kutuma kwetu mtaalamu wao wa fedha kesho saa 4 asubuhi kuhakiki deni la klabu hiyo akiwa na vielelezo vyote ofisi za TFF.”

Hitimisho, CEO Yanga aibuka na ‘DAWA YA DENI NI KULIPA’

Kufuatia barua hiyo ya TFF, Yangakupitia kwa Ofisi ya Mtendaji Mkuu wao (CEO), wamechapisha taarifa nyingine kama inavyosomeka hapo juu.

SOMA HII PIA: Timu bora zilizofunga ndani ya boksi la 18 Ligi kuu ya NBC Tanzania 2024/2025- Azam FC, Simba SC na Yanga Sc ni balaa

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.