- Clatous Chama kiungo wa Yanga SC huenda akaongezewa mkataba kusalia Jangwani kwa msimu ujao wa 2025/25.
- Dickson Job beki wa kati chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Miloud Hamdi mkataba wake kufanyiwa maboresho makubwa andelelee kusalia hapo.
- Jean Ahoua wa Simba SC mwenye mabao 15 kwenye ligi anatajwa kuwekewa mezani ofa na timu kutoka Afrika Kusini.
Clatous Chama kiungo wa Yanga SC kuongezewa mkataba wa mwaka mmoja kusalia ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Miloud Hamdi ikiwa mazungumzo yatakwenda vizuri. Chama ni mchezaji wa kwanza kutambulishwa ndani ya Yanga SC, msimu wa 2024/25 alitambulishwa akitokea ndani ya Simba SC ambapo alikuwa ni mchezaji huru baada ya mkataba wake kugota mwisho.

Soma hii: Chama kutua Yanga, Ali Kamwe atangaza kuna mtu atakula 10
Inaelezwa kuwa alisaini kandarasi ya mwaka mmoja kuwa ndani ya kikosi cha Yanga SC ambacho kinaongoza ligi kwa sasa ikiwa na pointi 73 baada yakucheza mechi 27 msimu wa 2024/25. Taarifa zinaeleza kuwa Chama ameitwa na mabosi wa Yanga SC ili kumpa kandarasi yam waka mmoja kuendelea kusalia ndani ya kikosi cha Yanga SC.
Ikumbukwe kwamba kiungo huyo raia wa Zambia Clatous Chama hakuwa na nafasi kikosi cha kwanza msimu wa 2024/25 kutokana na uwepo wa Aziz Ki ambaye amepewa Thank You na kutambulishwa Wydad Casablanca. Mbali na Chama wapo wachezaji wengine ambao wanatajwa kuitwa mezani kuongezewa kandarasi na wengine wakitajwa timu nyingine namna hii:
Dickson Job naye aitwa mezani
Dickson Job beki wa Yanga SC anatajwa kuitwa mezani kuzungumza kuhusu suala la kuongeza mkataba wake na maboresho kwenye mkataba wake ambao unatarajiwa kugota mwisho msimu utakapoisha ili aendelee kuwatumikia mabosi wa Jangwani.

Job alitambulishwa ndani ya Yanga SC akitokea Mtibwa Sugar, wakati wa usajili wake kulikuwa na mvutano mkubwa kwa mapacha hawa wa Kariakoo ambapo ilikuwa inatajwa kuwa Simba SC nao walikuwa kwenye hesabu za kuinasa saini yake.
Jean Ahoua anawindwa Afrika Kusini
Jean Ahoua kiungo mshambuliaji wa Simba SC anatajwa kuwa kwenye rada za mabosi wa Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini ambayo inahitaji kupata huduma ya kiungo huyo kinara wa utupiaji mabao ndani ya ligi. Ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo ni namba nne kwa ubora Afrika, Ahoua ni namba moja kwenye chati ya wakali wakufunga mabao mengi kwenye mechi za ushindani msimu wa 2024/25.

Soma na hii:Wachezaji wa Simba SC watakao achwa msimu wa 2025/26
Ahoua mwenye mabao 15 ni miongoni mwa viungo ambao hawana mengi uwanjani. Rekodi zake zinaonyesha kuwa ni mchezaji aliyehusika kwenye mabao mengi ndani ya ligi kwa wachezaji wote. Mabao yake 15 na pasi 8 ambazo ametoa zinamfanya ahusike kwenye mabao 23. Simba SC ni namba mbili kwa timu ambazo zimefunga mabao mengi ambayo ni 63 na vinara ni Yanga SC ambao wamefunga mabao 71.
Hussen Kazi wa Simba SC huyo Mbeya City
Beki wa kati wa Simba SC, Hussen Kazi huenda akaibukia ndani ya Mbeya City baada ya kushindwa kupata nafasi ndani ya kikosi cha Simba SC kinachonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids. Nyota huyo kwa msimu wa 2024/25 hajaanza kikosi cha kwanza kwenye mechi za ligi.
Gibrli Sillah anatajwa Yanga SC
Kiungo mshambuliaji wa Azam FC ambaye yupo kwenye viunga vya matajiri wa Dar, anatajwa kuwa kwenye rada za mabosi wa Jangwani, Yanga SC. Sillah ni mkali kwenye kufunga na kutengeneza nafasi za mabao ambapo kwa msimu wa 2024/25 kafunga mabao 9 na kutengeneza pasi mbili za mabao amekuwa akitajwa kuwa katika hesabu za Yanga SC.
Keita wa TP Mazembe awaingiza vitani Yanga SC, Singida
Ibrahim Keita ni mlinzi wa kulia ambaye mkataba wake na timu ya TP Mazembe unakaribia kufika mwisho na inaelezwa kuwa hayupo tayari kuongeza kandarasi nyingine. Singida Black Stars walianza kuulizia saini ya nyota huyo kisha Yanga SC wakafuata kuulizia ili kuinasa saini yake.
Feisal Salum wa Azam FC anatajwa Simba SC na Yanga SC
Mkali wa pasi za mwisho ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara, Feisal Salum maarufu kwa jina la Fei Toto anatajwa kuwa kwenye rada za mabosi wa Kariakoo Yanga SC na Simba SC. Huyu ni mzawa ambaye alikuwa anatajwa kuwa katika rada za Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.

Fei Toto ambaye aliibuka ndani ya Azam FC 2023 akitokea Yanga SC kwa kandarasi ya miaka mitatu ametengeneza jumla ya pasi 13 za mabao kwenye ligi na kafunga mabao manne yote akitumia mguu wa kulia.
Nyota huyu anatajwa kuwa kwenye hesabu za mabosi wa mitaa ya Kariakoo ambao kwa ukaribu wanafuatilia kupata saini ya kiungo huyo ambaye mguu wake wenye nguvu ni ule wa kulia katika kutimiza majukumu yake.
Elvis Rupia anatajwa Yanga SC
Mkali kwenye kucheka na nyavu ambaye yupo Singida Black Stars, Elvis Rupia anatajwa kuwa kwenye rada za mabosi wa Jangwani Yanga SC ambao wanahitaji saini yake kwa ajili ya msimu mpya wa 2025/26. Rupia ndani ya ligi katupia mabao 10 akiwa namba mbili kwenye eneo hilo ndani ya Singida Black Stars na kinara ni Jonathan Sowah mwenye mabao 11.
Singida Black Stars inatarajiwa kucheza fainali ya CRDB Federation Cup dhidi ya Yanga SC mchezo unaotarajiwa kuchezwa Juni 28 2025. Yanga SC wanatajwa kuwa kwenye mpango wakufanya maboresho kwenye kikosi hicho kuongeza ushindani kitaifa na kimataifa.

