Yanga vs Simba Juni 15Yanga vs Simba Juni --
  • Yanga SC vs Simba SC iliyopangwa Juni 15, 2025 mchezo namba 184 ngoma imezidi kuwa ngumu huko.
  • Yanga wamesisitiza tena msimamo wa kutoshiriki mchezo huo na hata ligi ya msimu ujao 2025/26 kabla ya maombi yao kufanyiwa kazi.
  • Hiyo ikiwa haitoshi Yanga wametishia kutocheza mchezo wa Fainali wa Kombe la Shirikisho la CRDB siku ya tarehe 28.

Kuhusu kuchezwa kwa mchezo namba 184 wa Ligi Kuu Bara Yanga SC vs Simba SC iliyopangwa Juni 15, 2025 hali imezidi kuwa tete, ambapo leo Jumatatu uongozi wa Yanga umeendelea kusisitiza msimamo wa kutoshiriki mchezo huo na hata ligi ya msimu ujao kabla ya maombi yao kufanyiwa kazi.

Nini kimetokea kuhusu mchezo namba 184 wa Yanga SC vs Simba SC iliyopangwa Juni 15, 2025?

Kabla ya kupangwa kwa Juni 15, kuwa tarehe mpya ya Kariakoo Dabi, ikumbukwe awali mchezo huu ulipangwa kufanyika tarehe 8 Machi 2025, lakini uliahirishwa kutokana na mivutano iliyozuka kabla ya pambano hilo lilipoangwa kupigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Chanzo cha mgogoro huo ni Machi 7, mwaka huu ambapo kikosi cha Simba SC kilitangaza rasmi kutoshiriki mchezo huo baada ya kudai kilizuiwa kufanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, tofauti na matakwa ya kanuni ya 17(45) ya Ligi inayoiruhusu timu ngeni kufanya mazoezi kabla ya mechi.

Simba ilidai kuwa wachezaji wake walizuiwa kuingia uwanjani na walinzi wa Yanga SC, jambo lililozua mgogoro mkubwa. Katika kujibu tuhuma hizo, Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB), ilifanya uchunguzi na kubaini kuwa Simba SC ilishindwa kufuata utaratibu sahihi wa kuomba ruhusa ya kufanya mazoezi uwanjani.

Hata hivyo, TPLB ilithibitisha kuwa wachezaji wa Simba walizuiwa kuingia uwanjani na walinzi wa Yanga SC, jambo ambalo lilikiuka Kanuni ya 17(45), Kwa hiyo, TPLB iliamua kuahirisha mchezo huo ili kuchunguza.

SOMA HII PIA: Mechi ya Tanzania Prisons vs Yanga SC itawaka Juni 18 2025 live, uchanganuzi, H2H | Kutawaka Mbeya na Aucho awashtua!

Yanga wacharuka wakataa katukatu kucheza

Kufuatia maamuzi hayo, uongozi wa Yanga ulicharuka na kuweka wazi hautakuwa tayari kucheza mchezo huo siku nyingine na kwamba huo mchezo ulipaswa kuchezwa kama ulivyopangwa. Kama hiyo haitoshi Yanga waliweka wazi kuwa hawana imani na baadhi ya watendaji wakuu wa Bodi ya Ligi hivyo wajiuzulu.

Kikao kizito chaitwa leo Jumatatu kuujadili mchezo wa Yanga SC vs Simba SC iliyopangwa Juni 15, 2025?

Kufuatia sintofahamu ya kutocheza mchezo huo, uongozi wa Bodi ya Ligi Kuu Bara chini ya Mwenyekiti wake, Steven Mguto leo Jumatatu Juni 9, 2025 uliwaita viongozi wa Yanga kujaribu kupata suluhu ya jambo hilo kupitia kikao maalum kilichofanyika makao makuu ya bodi, Dar es Salaam.

Mara baada ya masaa kadhaa ya kikao hiko, uongozi wa Bodi ukatoa mrejesho wa kikao ikiwemo kuweka wazi kuwa wamepokea mapendekezo ya bodi na watayafanyia kazi, huku wakitangaza mchezo upo palepale.

SOMA HII PIA: Yanga SC vs Simba SC inayodhamiriwa Juni 15 2025 Dabi ya Kariakoo mechi ipo, au haipo?

Yanga walipuka tena, sasa wagomea mechi zote zilizobaki, watishia kujitoa kwenye ligi

Kufuatia mrejesho wa Bodi ya Ligi uongozi wa Yanga umewaka upya, ambapo kupitia Ofisa habari wao Ali Kamwe umesema: “Ni kweli tulipokea barua ya wito Juni 7 na leo tumeshiriki kikao kama tulivyoombwa na bodi ya Ligi, kwenye kikao hiki maalum kujadili sintofahamu ya mchezo namba 184 wa Ligi Kuu.

“Kwenye kikao chetu tuliuliza pia kuhusu ripoti ya kilichotokea Machi 8, na CEO wa Bodi ya Ligi, Almasi Kasongo akakiri kuwa ripoti wanayo na kuna kiongozi mkubwa wa Serikali alipiga simu kuzuia geti la uwanja lisifunguliwe, lakini hawawezi kumtaja hadharani.

“Nashangaa hili hajalisema kwenye tuliyoyazungumza leo, tumshauri akiamua kusema aseme yote asibakishe, tumetoa matakwa manne. Tunaamini yakifanyiwa kazi hayo matatu ya kwanza, tutakuwa tayari kucheza mechi hiyo kwa tarehe nyingine itakayopangwa.

 “Takwa letu la kwanza na la pili linahusu ukiukwaji wa kanuni uliofanyika Machi 8. Tunataka Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi pamoja na CEO wa Bodi ya Ligi Almasi Kasongo wawajibike kwa kujiuzulu, kwa kushindwa kusimamia kanuni na kuutia doa mpira wetu.

“Takwa letu la tatu ni kujiuzulu kwa Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao kwa kushindwa kuchukua hatua dhidi ya maamuzi mabovu ya mara kwa mara ya waamuzi. Kamati ya waamuzi ipo chini ya TFF kwa Katibu Mkuu, unashangaa ni mwamuzi anafanya makosa yakujirudia na bado anaendelea kupangwa.

SOMA HII PIA: Wachezaji wa Simba SC watakao achwa msimu wa 2025/26 | Aishi Manula, Che Malone, Hussein Kazi wamepewa thank you

Yanga kutoshiriki Ligi Kuu msimu ujao!

Kamwe aliendelea kusema: “Napenda kuwajuza waandishi wa Habari, yasipofanyiwa kazi matakwa yetu matatu kwa uharaka, Yanga hatutakuwa tayari kucheza mchezo namba 184, mechi zote mbili za Ligi zilizobaki na hatutashiri Ligi Kuu Msimu ujao. Huu ndio msimamo wetu na hatutayumba kwa lolote lile.

Kuhusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB

“Taarifa hii iwafikie ofisi ya Katibu Mkuu wa TFF na Wadhamini wa mashindano ya Kombe la Shirikisho la CRDB, kuwa HATUTACHEZA mchezo wa Fainali wa CRDB siku ya tarehe 28, mpaka tutakapolipwa hela yetu ya Ubingwa kwa msimu uliopita. Tumevumilia dharau kwa muda mrefu, sasa imefika mwisho.

“Kama wanafikiri tunatania waendelee kupuuza, katika hili Klabu ya Yanga tuko serious zaidi ya wanavyodhani na tuko tayari kwa lolote litakalotokea. Na kama yuko mmoja wao anadhani kupunguza pointi ya Yanga ni rahisi, na ajaribu kufanya hivyo na asuburi aone NGUVU YA WANANCHI,” Kamwe.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.